Kuvuja damu nyepesi isiyojaza pedi kwa siku moja ama mbili sio kisa cha shaka katika safari yako ya ujauzito. Ila, kuvuja damu huku kunapozidi kwa zaidi ya siku mbili na kwa kiwango kikubwa, ni muhimu kwenda kwenye kituo cha afya.
Sababu za kutoka damu wakati wa mimba changa

- Damu baada ya yai kujipachika kwenye uterasi
Kitendo hiki kwa Kisayansi kinafahamika kama implantation. Ambapo yai lililorutubishwa linajipandikiza kwenye ukuta wa kizazi. Kutoa damu nyepesi kati ya siku 6 - 12 baada ya kufanya kitendo cha ngono ni ishara kuwa yai limejipandikiza kwenye ukuta wa uterasi. Damu ya kujipachika kwa yai huwa nyepesi na huisha ndani ya siku tatu. Tazama tofauti kati ya damu ya hedhi na ya implantation hapa.
2. Kuvuja damu baada ya tendo la ndoa
Kitu chochote kinachoingia ukeni wa mwanamke anapokuwa na mimba kinaweza kumjeruhi na kumfanya avuje damu. Kwa baadhi ya wanawake, wanapofanya tendo la ndoa, wao huvuja damu nyepesi. Huisha baada ya muda mfupi.

3. Kuharibika kwa mimba
Nafasi za kupoteza mimba huwa zaidi katika mimba ya chini ya miezi mitatu. Kuvuja damu inayogeuka na kuwa mabonge makubwa ni ishara kuwa mama anapoteza ujauzito. Kutokwa na mabonge ya damu kuna ambatana na maumivu makali ya mgongo na tumbo ya chini, na kuhisi kichefuchefu.
4. Mimba kutunga nje ya kizazi
Mimba ya ectopic inafanyika pale ambapo yai linajipandikiza nje ya mji wa mimba na mara nyingi kujipandikiza kwenye mirija ya uzazi. Ishara za kuwa na mimba ya ectopic ni kama vile kutokwa na damu nyepesi, kuumwa na tumbo vikali na maumivu ya mara kwa mara.
5. Kuwa na mimba ya mapacha
Mama aliye na mimba ya mapacha ana nafasi zaidi za kutokwa na damu nyepesi. Damu hii huisha baada ya muda.
Kutoka damu nyepesi wakati wa mimba changa sio chanzo cha wasiwasi. Lakini kuwa makini, damu inapogeuka na kuanza kutoka kwa matone makubwa, ni ishara kuwa kuna jambo lisilokuwa sawa. Enda ukaguliwe kwenye kituo cha matibabu.
Soma Pia: Vitu 6 Vinavyo Fanya Safari Ya Ujauzito Iwe Rahisi Zaidi