Kutoka nje ya katika ndoa kuna ongezeka mahitaji ya kihisia na kifizikia yasipo timizwa katika ndoa.
Sababu Kwa Nini Visa Vya Kutoka Nje Katika Ndoa Vimeongezeka

Huenda ukaona wanandoa wakiwa katika ncha ya kutengana kufuatia visa vilivyo ongezeka vya kuwa na wachumba nje ya ndoa.
Mojawapo ya sababu kuu zinazo changia kutoka nje ya ndoa ni kuongezeka katika kuto jali kati ya wanandoa na kupuuza mahitaji ya kihisia na kifizikia.
Katika ndoa zilizo fuzu, wanandoa wanaelewa kuwa kuna uraibu wa kutoka nje kwa hivyo wanafanya wawezavyo kuepuka hayo.
1.Wanandoa wanapo fikiria kuwa hawatawahi shikwa wakitoka nje
Nafasi za kupatikana ukidanganya katika ndoa zimeongezeka ikilinganishwa na hapo awali ambapo huenda ikawa ilikuwa vigumu kidogo. Wanandoa wanapo kosa kujali, wazo la kupatikana huwa haliwakujii na kwa hivyo inakuwa rahisi kufikiria kuwa kuna mtu anaye washuku.
2. Athari za kutoka nje ya ndoa hazijawahi kukutendekea
Kusalitiwa na mwenzi wako sio wazo rahisi. Mtu uliye mwamini zaidi alidanganya na hauoni ndoa yenu itakavyo endelea kuwa. Hakuna anaye penda kupitia hilo.

3. Kudhania kuwa mchumba wako hajali
Maisha huenda yaka ingilia kati maisha yenu, watoto na kazi zinaweza washika, huenda mkakosa wakati tosha wa kuwa pamoja. Wanandoa wanapaswa kutenga wakati tosha wa kuwa pamoja na wanandoa wao.
4. Tabia ya kutoka nje iko kwenye familia
Ikiwa kuna historia ya kuwa na wachumba nje ya ndoa, huenda ukajipata ukifuata mkondo huo na kuwa na mchumba zaidi ya mmoja. Ni vyema kumjuza mchumba wako na kujua mawazo yake kuhusu kutoka nje.
5. Nafasi za kudanganya
Ni vigumu kuepuka majaribio, lakini kuna njia ambazo unaweza jitenga na majaribio haya. Hakikisha kuwa mna wasiliana wakati ambapo mmoja wenu ako mbali.
Kumbuka kuwa ndoa ni uamuzi wa watu wawili kuanzia familia pamoja. Uaminifu ni muhimu katika ndoa ili maisha yenu yawe ya kupendeza. Hakikisha kuwa mna zungumza mnapo kuwa na suala lolote linalo wasumbua ili kuepuka majaribio ya kutoka nje ya ndoa.
Soma Pia: Wanadada: Mambo Haya 5 Unayo Yafanya Yana Wafukuza Wanaume