Sababu 6 Za Kutoa Damu Katika Wiki Za Kwanza Za Mimba

Sababu 6 Za Kutoa Damu Katika Wiki Za Kwanza Za Mimba

In the early weeks of pregnancy, a little spotting or bleeding is very common. But before you relax, just how much is the bleeding?

Unapo kuwa na mimba, ishara yoyote ya kutoa damu ni ya kuogofya. Ila, usiwe na shaka: kutoa damu unapokuwa na mimba ni kawaida kuliko unavyo dhani, wakati mwingi, sio jambo la kukutia shaka. Kwa mfano, huenda ukawa una dhani, niko wiki ya nane ya ujauzito na bado nashuhudia kutokwa na damu ukiwa na mimba, nitafanyaje? Tulia. Hivyo ndivyo unavyo paswa kufanya.

Hata kama kutokwa na damu siku za kwanza za mimba ni maarufu na huenda kukawa kawaida, huenda kukamfanya mama mwenye mimba kutia shaka. Kutokwa na damu kuna tarajiwa kwa kisa chochote na ni kawaida. Nyakati zingine, huenda kukawa ishara ya mimba inayo haribika, kuanguka ama tatizo la placenta, ama uchungu wa uzazi wa mapema.

Ni wazo bora kumwona daktari wako wakati wowte unapo shuhudia kutokwa na damu. Unataka kuhakikisha kuwa wewe na mtoto wako mko salama. Ila, kabla ya kufikiria ni jambo mbaya lililo tendeka, hapa kuna baadhi ya sababu za kutokwa na damu ungali mjamzito.

Wiki 8 Za Ujauzito Na Bado Natokwa Na Damu: Sababu Za Kutokwa Na Damu Ukiwa Na Mimba

Kiinitete kina jishikilia

kutokwa na damu ukiwa na mimba

Mojawapo ya ishara za mapema zaidi za mimba ni kutokwa na kiasi kidogo cha damu. Utaona unapo jipanguza. Kwa hivyo iwapo una tumaini kutunga na ugundue kuwa unatokwa na kiasi kidogo cha damu karibu na wakati unao tarajia kipindi chako cha hedhi, kuna uwezekano kuwa umefanikiwa. Kutokwa na damu huku mara nyingi huwa kwa sababu kiinitete kinajishikilia kwenye kuta za uterasi siku 10-12 baada ya kutunga. Kutunga kwa kiinitete hutendeka kati kati ya kipindi cha hedhi cha mwanamke cha siku 28. Kisha kujishikilia maarufu kama implantation hutendeka baada ya siku 10-12. Kwa hivyo kutokwa na damu huku hudhaniwa kuwa hedhi. Tofauti ni kuwa damu ya implantation huwa chache na huja kwa angalau siku mbili ikilinganishwa na hedhi yenye damu nyingi na huwa kwa siku 5 to 7.

Una hedhi nyepesi

Hata kama huenda ikakutia shaka, unaweza kuwa na kipindi chako cha hedhi ukiwa na mimba -  ina maana kuwa utashuhudia damu. Kutokwa na damu hutendeka kati ya wiki ya 6 ama ya 8 ya gestation. Huu ndiyo wakati ambapo hedhi ya mwanamke hutendeka katika mwezi wa pili. Hata baadhi ya wanawake wiki chache baada ya menopause huendelea kuwa na hedhi. Ni sawa hata kwa mimba, kutokwa na damu hutendeka wiki ya 8 kwa sababu mwili umezoea kutoa damu kila mwezi. Lakini tofauti na hedhi ya kawaida, hedhi hii huwa nyepesi na sio ya siku nyingi.

Ulifanya mapenzi

Kufanya mapenzi ama ngono unapokuwa mjamzito huenda kukawa na furaha na kwa kusisimua sana, na kuna himiziwa sana! Ila, ukishuhudia kutokwa na damu, huenda ikawa sio kitu kikubwa. Kadri ujauzito unavyo zidi, wanawake wengi wata shuhudia kutokwa na damu baada ya kufanya mapenzi. Hii ni kawaida na kunatendeka kwa sababu uke unakuwa vascular. Na kuupiga kufuatia ngono huenda kukasababisha kutokwa na damu. Wanawake wengi hushuhudia jambo hili baada ya kufanya mapenzi ila sio damu nyingi na hakuna kitu cha kukutia shaka.

Umefanya kipimo cha pelviki

Iwapo una shaka kuhusu kutoa damu baada ya kumtembelea daktari, usiwe na shaka. Kutokwa na damu huenda kukatendeka baada ya kufanyiwa kipimo cha sonogram ama cha pelviki na daktari wako. Jambo hili linafanyika kufuatia ongezeko la damu kwenye uterasi hadi kwa kizazi ambalo ni kawaida.

Una maambukizi

Wakati wa kutia shaka

Kutokwa na damu kwa ujumla huwa na hofu inapokuwa nyingi (kuliko ile ya kipindi chako cha hedhi cha kawaida), kisha kufuatiwa na uchungu wa tumbo.

Wakati ambapo kutokwa na damu huenda kukafanya mama atie shaka na kuhusishwa na kupoteza mimba, iwapo damu ni nyepesi, haihusishwi na kupoteza mimba.

Fahamu: Iwapo unashuhudia kutokwa na damu ukiwa na mimba na unahisi uchungu mwingi , unapaswa kuona daktari bila kupoteza wakati. Ni vyema kuwa makini na kuangalia rangi ya damu, na kiwango chake, ishara nyingine yeyote ambayo huenda ikaandamana nauo na umjulishe daktari wako.

Written by

Risper Nyakio