Njia 5 Kuu Za Kutuliza Vidonda Vya Tumbo Kutumia Matibabu Ya Kinyumbani

Njia 5 Kuu Za Kutuliza Vidonda Vya Tumbo Kutumia Matibabu Ya Kinyumbani

Hakuna matibabu kamili ya kuponya vidonda vya tumbo maarufu kama ulcers, ila kuna njia ambazo unaweza tumia kutuliza uchungu. Ulcers ni vidonda vinavyo ibuka kwenye kuta ya tumbo ama sehemu ya matumbo.

Vidonda hivi vya tumbo vina sababishwa na:

  • Maambukizi ya bakteria H. pylori
  • Kutumia ibuprofen ama dawa za nonsteroidal anti-inflammatory kwa muda mrefu

Fikira nyingi na kula chakula chenye viungo vingi vikali pia kunaweza ibua ishara za vidonda vya tumbo. Hata kama haviwezi sababisha ulcers, vinaweza fanya hali iwe mbaya zaidi kwa kuongeza kiwango cha asidi inayo tolewa tumboni.

kutuliza vidonda vya tumbo

Vyakula vya kutuliza vidonda vya tumbo

 

  1. Asali

vyakula usivyofaa kuhifadhi kwenye jokofu

Asali asili ina viungo vilivyo muhimu katika kutibu vidonda vya tumbo. Asali ni maarufu katika kuongeza ladha asali duniani kote. Watu wanao kula asali wana pata faida nyingi za kiafya. Ikiwemo kuponya vidonda, kama vile vya tumbo, vya kuchomeka na vinginevyo.

2. Kitunguu saumu

Garlic

Kitunguu saumu kinasifika kwa manufaa yake ya kiafya duniani kote. Kimetumika kwa miaka mingi kuongeza ladha kwenye chakula. Pia, kina faida za kupigana dhidi ya maambukizi na kukifanya bora kwa watu wanao tatizika na hali ya vidonda vya tumbo.

3. Aloe vera

kutuliza vidonda vya tumbo

Mmea huu una mahitaji mengi na unatumika sana kwenye mafuta ya kujipaka na bidhaa za urembo za wanawake. Masomo yaliyo fanyika kudhibitisha athari zake kwa vidonda vya tumbo yali onyesha kuwa mmea huu una tibu ulcers kwa njia sawa na baadhi ya dawa za ulcers.

4.  Tangawizi

health benefits of ginger

Kufuatia utafiti mwingi ulio fanyika kwa wanyama, tangawizi ime dhihirishwa kuwa na matokeo chanya. Hata kama sio wazi kana kwamba athari zitakuwa sawa kwa wanadamu wote. Tangawizi ina athari chanya kutibu hali tofauti za tumbo ikiwemo gastritis.

5. Probiotics

Hivi ni viumbe vinavyo saidia kusawasisha bakteria kwenye mfumo wa kuchakata chakula. Na pia kusaidia kuwa na afya bora ya gut na kutibu ulcers. Zinapo chukuliwa pamoja na matibabu mengineyo, probiotics zina saidia kutoa bakteria mbaya mwilini. Zina patikana kwenye bidhaa kama vile maziwa ya bururu, tembe za probiotics.

Soma PiaDumisha Afya Ya Mwili Wako Kwa Kula Vyakula Hivi Kama Kiamsha Kinywa Chako

Written by

Risper Nyakio