Jinsi Ya Kutumia Kipimo Cha Mimba Kupima Iwapo Una Mimba

Jinsi Ya Kutumia Kipimo Cha Mimba Kupima Iwapo Una Mimba

Watu wengi hutumia kifaa hiki cha kupima mimba mara kwa mara. Na huenda tukadhania kuwa kila mtu anajua jinsi ya kukitumia. Kwa wale wanao kitumia kwa mara ya kwanza, huenda wakaona haya kuuliza jinsi kifaa hiki kina tumika wanapo kinunua. Wauzaji pia wanaweza puuza na kuona kana kwamba kila mtu anajua kukitumia. Kuna sababu nyingi ambazo huenda zika fanya mwanamke ajipime ili kujua hali yake, iwapo ana mimba ama la. Lakini lazima aweze kutumia kipimo cha mimba inavyo paswa ili kupata matokeo sahihi.

jinsi ya kutumia kipimo cha mimba

Kipimo cha mimba hupima kuwepo kwa homoni ya human chorionic gonadotropin ambayo inajulikana kama HCG kwa mkato. Homoni hii inatolewa mwilini baada ya yai kutunga na kujishikilia kwenye kuta za uterasi. Ili kupata matokeo sahihi, kipimo hiki kinapaswa kufanyika baada ya kukosa kipindi chako cha hedhi.

Jinsi ya kutumia kipimo cha mimba

Kuna aina tofauti ya vipimo ila zote zina tumia utaratibu sawa.

  1. Jambo la kwanza kufanya ni kuweka mkojo kwenye kijikontena. Una shauriwa kutumia mkojo wa kwanza wa siku. Punde tu baada ya kuamka kabla ya kunywa kiamsha kinywa chako.
  2. Toanisha kipimo cha mimba kutoka kwa karatasi iliyo tumika kufunga.
  3. Kua makini kukitumia. Kuna alama ama laini nyeusi kwenye upande wa chini ya kipimo hicho.
  4. Hakikisha kuwa unapo tumbukiza kifaa hicho kwenye mkojo, haupitishi laini hiyo nyeusi. Kwani huenda ikafanya matokeo yasiwe sahihi.
  5. Baada ya kutumbukiza kwenye mkojo, shika kifaa hicho kwa sekunde kama 2 kisha uweke kifaa hicho pembeni kwa dakika 2.

Matokeo.

  • Iwapo una mimba, kutakuwa na mabadiliko ya rangi ya kifaa hicho, laini mbili zita onekana.
  • Kwa vipimo vingine kutakuwa na alama chanya (+) ama itoe jina (pregnant).
  • Ikiwa hauna mimba, kutakuwa na laini moja, ama alama hasi (-) ama jina (not pregnant).

jinsi ya kutumia kipimo cha mimba

Ni sababu zipi zinazo mfanya mtu kutumia kifaa cha kupima mimba?

Kukosa kipindi cha hedhi

Mojawapo ya ishara maarufu zaidi za kuwa na mimba ni kukosa kipindi chako cha hedhi. Ingawa kukosa kipindi chako cha mwezi huweza kuka sababishwa na vitu tofauti, ni vyema kuchukua kipimo ili kuhakikisha kuwa hauna mimba.

Mabadiliko ya mwili

Ishara nyingine ya mapema ya mimba ni kuhisi uchovu ama hata kuumwa na mwili. Huenda ukahisi kuumwa na tumbo mara kwa mara. Baadhi ya wanawake huanza kutamani vyakula fulani na kuchukia vingine. Kuhisi kutapika kwa sababu ya harufu ya vyakula fulani. Kuwa makini kusikiza mwili wako iwapo utasikia ama kuona mabadiliko yoyote.

Kuhisi kutapika

Hii ni ishara maarufu ya kuwa na mimba. Kuna magonjwa ambayo huenda yaka kufanya uhisi kutapika mbali na kuwa mjamzito. Ili kuwa na uhakika, ni vyema kufanya kipimo cha mimba kutoa shaka zote.

vomiting in pregnancy signs of high IQ

Kuumwa na chuchu

Ili kuanza kujitayarisha kubeba maziwa ya mama, chuchu huanza kuwa kubwa, na kuuma. Huenda hii ikawa ishara kuwa ni wakati wa kudhibitisha iwapo una mimba kwa kweli.

Iwapo una shaka kuwa huenda ukawa mjamzito, tumia maarifa yetu ya jinsi ya kutumia kipimo cha mimba kuwa na uhakika iwapo una mimba ama la. Baada ya kujua hali yako, iwapo una mimba, enda hospitalini ili upate ushauri kutoka kwa wataalum jinsi ya kuanza kujitayarisha. Iwapo utapata matokeo hasi, usiwe na shaka, mbali endelea kujaribu hadi pale utakapo fanikiwa.

Kumbukumbu:

Soma pia: Jinsi Tofauti Za Kupima Mimba

Written by

Risper Nyakio