Mabadiliko ya mwili kwa wanawake huwa ndio ishara za kwanza za ujauzito. Hizi ishara huwa hata katika hatua za mwanzo za mimba. Huwa kama vile Kukosa hedhi, matiti na chuchu nyeti na kichefuchefu. Kuna vipimo vingi vya mimba nyumbani ila leo tunaangazia kutumia sukari kupima mimba.
Kutumia Sukari Kupima Mimba

Baada ya yai na manii kukutana maumbile mbalimbali yanaunganika kutengeneza seli mpya. Hivyo mwanamke husemakana kushika mimba. Pindi baada ya haya, seli mpya ndani ya maumbile hukua na kufanyika plasenta ya mtoto. Hizi plasenta huanza kutengeneza homoni Human Chorionic Gonadotropin( hcg).
Hii huwa kwa viwango vidogo hata kabla ya kujipandikiza kwenye uterasi. Baada ya kujipandikiza kwenye uterasi viwango vya hcg huongezeka. Pia hii homoni huamrisha mwili kuachisha hedhi. Kipimo cha mimba hulenga kutambua hii homoni aidha kwenye mkojo au damu.
Sukari ni kitu cha kawaida katika kila nyumba. Hii sukari ya kawaida unaweza kuitumia katika mtihani wa ujauzito. Weka vijiko kadhaa vya sukari kwenye bakuli lako. Ongeza mkojo kidogo ndani. Tafuta uundaji vitu kama vile cubes. Ikiwa sukari inaganda, ni ishara kwamba wewe ni mjamzito. Ikiwa sukari inayeyuka kama maji kwenye mkojo basi hauna ujauzito.
Vipimo vyote vya ujauzito, pamoja na hii ya sukari ni bora kufanya kwanza asubuhi unapoamka. Kwa njia hii mkojo utakuwa umejilimbikiza zaidi. Ikiwa haiwezekani kufanya jaribio asubuhi, chaguo moja ni kuweka mkojo kitu cha kwanza asubuhi kwenye chombo kisichopitisha hewa na ufanye baadaye.
Lini Kufanya Kipimo Cha Nyumbani?

Muda mzuri wa kufanya kipimo hiki ni baada ya hedhi yako kuchelewa. Hii itakusaidia kuepuka majibu ya uongo. Kufanya kipimo cha mimba mapema kinaweza kukupa majibu hasi ata kama una ujauzito.
Pia utaweza kupata majibu ya uhakika kabisa kama utafanya kipimo chako asubuhi. Mkojo wako wa kwanza wa asubuhi utakuwa na viwango vikubwa vya hcg. Hii ni kama hujakunywa maji mengi usiku ama kuamka mara nyingi usiku kujisaidia.
Sababu Ya Kutumia Sukari Kupima Mimba
Ingawa ni kweli kwamba jambo la kwanza ni kushauriana na daktari wako kwa wanawake wajawazito ili kuhakikisha afya yako na mtoto wako. Kuna sababu nyingi kwa nini hautaki kutumia huduma za mtaalamu wa matibabu au duka la dawa kuthitibisha ujauzito wako. Baadhi ya sababu hizi ni:
- Mtihani wa ujauzito unaweza kuwa ghali sana
- Inaweza kuwa ngumu kufika kwa daktari au kutembelea duka la dawa ikiwa unaishi katika mji wa mbali
- Kwenda kwa daktari kupima damu au mkojo kungemaanisha kusubiri
- Unaweza kutaka kuweka ujauzito kuwa siri kwa sasa
- Pia unaweza kuwa wataka faragha yako na ni rahisi
Vipimo Vingine Vya Nyumbani
Kufanya huu mtihani unahitaji dawa ya meno nyeupe nyeupe. Isiwe na gel ama rangi iliyokolea. Kuna mambo mawili ambayo yanaweza onyesha ikiwa una mjamzito. Ukiongeza mkojo kwenye dawa ya meno nyeupe igeuke kuwa nyepesi au ianze kutoa povu sana inaweza kuonyesha kuwa wewe ni mjamzito.
Kupima mimba unaweza kutembelea hospitali ama kufanya mtihani huu nyumbani kwa kutumia kits. Hizi unaweza kununa kwa duka la dawa bila uelekezaji wa daktari. Ila pia kuna vipimo asili kama kutumia sukari kupima mimba.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Jinsi Ya Kuongeza Nafasi Ya Kushika Mimba Kwa Urahisi Katika Miaka Ya 30’s