Mitandao ya kijamii imekuwa na mjadala moto kuhusu wanasiasa na wasanii. Haya ni baada ya Azimio la Umoja ambacho ni chama cha kisiasa nchini Kenya kucheza wimbo wa Sauti Sol katika kampeni zao. Sauti Sol ni mojawapo ya boy band maarufu zaidi na duniani kote. Wanafahamika na kusifika kwa nyimbo za maana na za kupendeza wanazoimba kuwatumbuiza watu. Nyimbo kama Suzanna, Rhumba Japani, Lazizi, Short N Sweet na kadhalika.
Kikundi cha Sauti Sol
Kikundi kinachotukuka, kuheshimika na kuzungumziwa kwa hadhi kwani kwa muda mrefu kimefanya bendera ya nchi ya Kenya kupepea duniani kote wanapoenda kuimba.
Sauti Sol walivunja kimya chao kwa kuzungumzia hisia zao baada ya chama cha Azimio la Umoja kutumia wimbo wao katika kampeni bila kulipia leseni. Walitishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya chama hiki.
Muwania kiti cha urais wa chama cha Azimio la Umoja, mmoja Raila Odinga kupitia kwa chama chake cha Orange Democratic Movement (ODM), alisema kuwa, kucheza wimbo wao katika kampeni ilikuwa ishara ya mapenzi.
Katika ujumbe wake kwenye Twitter Raila Odinga aliandika, “Tungependa kuiashiria timu yetu ya muziki inayosherehekewa @sautisol kuwa tunawapenda na kuthamini muziki wao sana. Kikundi hiki kimebeba bendera yetu juu sana duniani kote na kila mwanaKenya anathamini jambo hili. Kucheza wimbo wao jana ilikuwa ishara ya kupenda kazi yao.”

Siku ya Jumatatu tarehe 16, 2022, chama cha Azimio la Umoja kilicheza wimbo wa Sauti Sol wa Extravaganza walipokuwa wakitangaza naibu wa rais wa chama chao katika kampeni za kirais. Hatukukipatia chama chochote kibali cha kutumia wimbo wetu katika uvumbuzi wa mgombeaji kiti cha naibu rais katika chama chao. Sauti Sol walisema.
Sauti Sol waliashiria kuwa utumizi wa wimbo wao bila kibali chao ni kuenda dhidi ya hakimiliki kama ilivyoandikwa kwenye Section 35, CAP 170 ya hakimiliki za Kenya.
Kikundi hiki kilijitenga na chama chochote cha kisiasa, Azimilio la Umoja na vikundi vingine vya kisiasa na wanasiasa wowote nchini.
Chanzo: Africaparent
Soma Pia:Mulamwah Kwenye Redio: Mulamwah Apata Kazi Milele FM