Sababu Kwa Nini Kutunga Mimba Katika Kuarantini Sio Wazo La Busara

Sababu Kwa Nini Kutunga Mimba Katika Kuarantini Sio Wazo La Busara

About that baby boom...you might want to hold off on trying for a baby during this pandemic.

Kadri dunia inavyo zidi kupigana na usambaaji wa COVID-19, shule zimefungwa, biashara zikafungwa; watu wana fanya kazi kutoka manyumbani mwao na wengine wana likizo za kazi bila malipo, na ukuaji wa nambari ya nchi zilizo piga marufuku umati wa watu. Huku kuna maana kuwa wachumba wanapata wakati zaidi kuwa pamoja, iwapo wanaishi pamoja. Na kwa njia ya asili kuwa pamoja na kukumbatiana kwingi kunapelekea kupata watoto. Mtandao unafurahikia kuwa na ibuko la kuzaliwa kwa watoto katika mwisho wa mwaka. Ila, kunapaswa kuwa na kutunga mimba katika kuarantini?

coronavirus and pregnancy

Hili ni swali lenye maana sana la kujiuliza kwa sababu kwanza, wataalum wanajua habari chache sana kuhusu virusi hatari vya homa ya corona; kwa hivyo hata wataalum wa afya hawana maswali yote. Pia, dunia yote ina inabadilika kwa hali hii mpya tuliyomo. Uchumi pia unabadilika na pia biashara na kwa muda, hakuna kitu kitakuwa hakika. Kwa hivyo ni vyema kuwaza kwa umakini kuhusu kupata mtoto katika janga hili.

Ukweli ni kuwa jibu ambalo unaweza kujibu kuhusu fikira zisizo za kweli kuhusu karantini. Kwa hivyo ni uamuzi wa kibinafsi kwa hivyo ni jukumu lako na mwenzi wako. Ila, iwapo kiwango cha uamuzi sio kikubwa cha ujumbe unao kuwa nao. Kwa hivyo, tunapozidi kungoja wataalum wa afya waelewe maradhi haya, huenda ukalazimika kuangalia kwa umakini jinsi ya kufanya kufuatia hali hii. Angalia baadhi ya ukweli ulioko.

Kutunga Mimba Katika Kuarantini: Wataalum Wana Yapi Ya Kusema

conception in quarantine

Kama tulivyo sema hapo awali, wataalum wana habari chache sana kuhusu virusi hivi; na nambari chache sana ya vipimo vinavyo fanyika, huenda ikawa vigumu kujua nambari ya watu walio na virusi hivi; ni watu wangapi hatimaye watapata virusi hivi, na jinsi vituo vyetu vya afya vimejazwa na watu wengi na matokeo yatakuwa yepi. Ila hapa kuna ukweli.

  • COVID-19 haisambai kwenye uterasi

Hivi majuzi, utafiti kutoka Uchina umetoa maoni kuwa COVID-19 haisambai kwenye kiinitete unapokuwa mjamzito. Virusi hivi haviko kwenye amniotic fluid, cord blood ama kwenye maziwa ya mama baada ya kujifungua. Kwa hivyo sayansi inasema kuwa wanawake wajawazito hawawezi sambaza virusi hivi kwa kiinitete kwenye uterasi yake. Hilo ni mbao la kwanza la habari njema, sio?

  • CDC inasema kuwa virusi vya homa ya corona haviongezi visa vya kupoteza mimba ama kushuhudia still births

Kulingana na Kituo cha Kudhibiti Magonjwa na Kuyaepuka (CDC) hakuonekani kuwa na  hatari za kupoteza mimba ama stillbirth iwapo mwanamke mjamzito anaugua virusi vya COVID-19. Jambo la pili kwa habari njema.

Na kwa sasa, kwa habari ambazo hazina uhakika.

  • Wataalum wa afya hawana uhakika iwapo kuwa mjamzito kuna ongeza hatari zako za kuambukizwa

Kulingana na CDC, hakuna anaye jua iwapo wanawake wajawazito wako katika hatari zaidi ya kuugua virusi hivi. Hivi majuzi, waziri mkuu wa UK Boris Johnson alitangaza kuwa watu wajawazito wameongezwa katika orodha ya watu walioko katika hatari ya kuugua virusi vya COVID-19. Aliwahimiza kukaa nyumbani kwa angalau wiki 12. Inapofika ni kwa virusi sawa ama maradhi ya mfumo wa kuugua, wanawake wajawazito wako katika hatari zaidi kwa hivyo kama mtu yeyote mwingine katika wakati huu, iwapo utapata mimba, unapaswa kunawa mikono. Epuka kugusa uso wako na ukae mbali na mtu yeyote anaye kohoa ama anaye onyesha athari za COVID-19, na uangazie umbali wa mtengano.

Baadhi ya Sababu za Kutia Maanani Unapo Amua Iwapo Ungetaka Kupata Mimba Katika Janga Hili

conception in quarantine

Utunzaji wa Kiafya unawezekana, ila sio kwa hakika

Mfumo wetu wa utunzaji wa afya kabla ya janga hili haukuwa mwema na sasa, ni mbaya zaidi. Hatuna uhakika ni watu wangapi wana virusi hivi vya corona kwa sababu ni upimaji mdogo sana unaendelea. Wataalum wanasema kuwa iwapo unahisi kana kwamba u-mgonjwa unapaswa kujitenga na watu hadi upimwe. Wana himiza watu kukaa mbali na hospitali, kwa hivyo hakuna aliye na uhakika wa utunzaji kabla na baada ya kujifungua utakavyo kua.

Na iwapo utafanya uamuzi wa kujifungua ukiwa nyumbani, kuna hatari nyingi sana. Wataalum wana himiza watu kuepuka hospitali, ila kwa wanawake wanao kuwa na uchungu wa uzazi, hapo hauna hiari. Kulingana na ujumbe ulio thibitiwa ulioko, wana kliniki hawa amini kuwa watoto waliozaliwa wako katika hatari zaidi za kupata virusi zaidi ya vile ambavyo wangefanya na maradhi mengine; na hata kama mtoto alizaliwa na mama aliye athirika na virusi vya COVID-19, sio jambo la busara kumtenganisha mtoto na mamake.

  • Fikiria jinsi kutunga mimba katika kipindi hiki cha kuarantini kutahisi ama kukaa.

Iwapo unajaribu kutunga mimba sasa, nafasi nyingi ni kuwa unajitayarisha kujifungua wakati ambapo kwa matumaini, janga hili litakuwa limepungua; ila, hakuna anayejua wakati ambao janga hili litachukua. Serikali imeshauri pia, kwa wakati huu, kuwa wa wavyele wakae mbali na wajukuu wao; wame ahirisha sherehe za kutarajia kuzaliwa kwa watoto, na kupunguza matembezi kuona watoto walio zaliwa hivi majuzi na familia zao kwa ujumla. Kujenga mfumo wa kuegemea ambao uko umbali wa rununu, kutembelea katika wakati huu huenda kukawa vigumu sana.

Hatimaye uamuzi unaafikiana na historia yako ya afya, ushauri kutoka kwa daktari wako, na afya yako ya kiakili. Kujaribu kutunga mimba ni jambo la kuchosha- kifizikia, kiakili na kihisia- kila kwa njia yake na bila ya kukwaza kiakili na mawazo ya mazingara yetu.

Ukweli, hakuna kitu kama "wakati unaofaa" wa kupata mtoto. ila, kuna wakati ambao huenda ukawa mzuri kuliko mwingine. Mwishowe, wewe na mwenzio ndio watu peke yake ambao wanaweza fanya uamuzi wa wakati sawa wa kupata mtoto.

CNN

Soma pia: Here's Everything You Need To Know About Coronavirus And Pregnancy

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Ayeesha kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio