Mwanamke anaweza kujifungua kupitia njia mbili. Njia ya kawaida, anapojifungua kupitia kwa uke wake, ama kujifungua kupitia upasuaji wa C-section. Haijalishi njia ambayo mwanamke anapata mtoto wake kupitia, mama wote ni sawa na ni baraka kupata mtoto salama. Kwa wanawake wanaojifungua kupitia kwa upasuaji, wanahitaji utunzaji zaidi. Kuhakikisha kuwa kidonda kinapona kwa kasi na kuepuka kukishinikiza. Makala haya yana angazia jinsi ya kutunza kidonda cha upasuaji wa c-section.
Utunzaji kwa kidonda cha upasuaji wa c-section

Usafi. Mama anastahili kuhakikisha kuwa kidonda hicho ni kisafi wakati wote. Jaribu kukiosha mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni. Kidonda hiki bila shaka kinauchungu, kwani kingali kinapona. Mama anaweza kutumia nguo safi ama pamba na maji kukiosha kwa utaratibu, kisha kukipanguza kuhakikisha kuwa hakuna maji yaliyo baki.
Kukipaka mafuta. Baada ya kusafisha kidonda kile, ni vyema kwa mama kukipaka mafuta kwa utaratibu kukifunika kwa kitambaa safi. Hata hivyo, kuna baadhi ya madaktari wanaoshauri mama kutopaka chochote kwenye kidonda hicho. Ni vyema kuzungumza kuhusu jambo hili na daktari wako.
Kujitenga na mazoezi. Bila shaka mazoezi yana anuwai ya faida kwa mwili. Ila, kuyafanya mazoezi baada ya upasuaji wa c-section sio jambo la busara. Kidonda hiki kinahitaji muda zaidi kipone, na kufanya mazoezi kunakishinikiza zaidi. Epuka kucheka kwa nguvu, kupanda kazi na kuinama. Daktari atakushauri wakati bora wa kurejelea mazoezi.
Kutembea mara kwa mara. Kutembea ni zoezi rahisi na nyepesi, inasaidia kuboresha mzunguko wa damu mwilini, na kuepusha damu kuganda mwilini.

Usikibane kidonda hicho. Mama anastahili kuvalia mavazi yasiyo kibana kidonda chake. Kukibana na kukishinikiza huenda kukafanya kiume ama kuongezeka. Kukiwacha wazi na kuvalia mavazi wazi kunasaidia kipone kwa kasi.
Mbali na hayo, mama anastahili kurudi kumwona daktari kama alivyoshauriwa kuhakikisha kuwa nyuzi zinabadilishwa kwa wakati ufao. Katika kipindi hiki ambapo mama hafanyi mazoezi sana, ni vyema kuhakikisha kuwa anakula chakula bora na chenye afya. Ili kuepuka kuongeza uzani wa mwili kwa kasi. Mama anastahili kufuata vidokezo hivi ili kutunza kidonda cha upasuaji wa c-section.
Chanzo: healthline
Soma Pia: Vidokezo 3 Muhimu Kwa Mama Anaye Pona Baada Ya Upasuaji Wa C-section