Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Jinsi ya Kutunza Mama Mpya Baada ya Kujifungua

3 min read
Jinsi ya Kutunza Mama Mpya Baada ya KujifunguaJinsi ya Kutunza Mama Mpya Baada ya Kujifungua

Kutunza mama mpya baada ya kujifungua kwa kumsaidia na kazi za kinyumbani na kumpa lishe bora kuna dumisha afya yake na ya mtoto.

Kipindi cha baada ya kujifungua huanzia punde tu baada ya mama kujifungua hadi wiki sita ama nane baada ya kujifungua. Katika kipindi hiki, ni muhimu kutunza mama mpya baada ya kujifungua.

Katika kipindi hiki baada ya mama kujifungua, kuna mabadiliko mengi yanayofanyika maishani mwake. Mbali na kuwa na mabadiliko ya kihisia na kifizikia, wazazi wapya wanasoma jinsi ya kumtunza mtoto wao.

Mama anapaswa kutunzwa na kupata usaidizi mwingi awezavyo katika wiki hizi za kwanza.

Kutunza mama mpya baada ya kujifungua

  1. Mapumziko

kutunza mama mpya baada ya kujifungua

Kila mzazi mpya anafahamu kuwa anapojifungua maisha yake yatabadilika. Atahitajika kuamka usiku kumlisha mtoto na hatakuwa na wakati tosha wa kulala. Mtoto mchanga anapaswa kulishwa baada ya kila masaa matatu, kwa hivyo mama atakuwa macho wakati mwingi. Itakuwa vigumu kwake kupata masaa manane ya usingizi kwa wiki nyingi zijazo. Katika kipindi hiki, ni vyema iwapo anaweza pata mtu wa kumsaidia na kazi za kinyumbani. Kwa njia hii, mtoto anapolala, ataweza kupata masaa machache ya kujilaza na kupumzika.

2. Lishe bora na yenye afya

Mwili wa mama hupitia mabadiliko mengi anapokuwa mjamzito. Katika mchakato wa kujifungua, mwili wa mama hutumia nishati nyingi. Anahitaji kula chakula bora kitakachosaidia kuregesha nguvu na nishati na kuuponya mwili. Chakula cha mama kinachangia pakubwa katika mama kuwa na maziwa tosha ya kumlisha mtoto. Sahani ya mama inapaswa kuwa na:

Protini: Bidhaa za maziwa, mayai, nyama ya kuku, ng'ombe, njugu na maharagwe.

Bidhaa za maziwa: Kama vile maziwa ya bururu na maziwa zina wingi wa kalisi muhimu mwilini wa mama aliyejifungua.

Nafaka: Kama vile oats, wali wa hudhurungi na ngano nzima

Matunda: Matunda hasa freshi yaliyotoka shambani. Kama vile ndizi, machungwa, parachichi na tufaha.

Mboga: Mboga zinasaidia kuongeza damu mwilini. Kabeji, sukuma wiki, kunde na malenge ni bora.

3. Fanya mazoezi

kutunza mama mpya baada ya kujifungua

Daktari atamshauri mama wakati bora wa kuanza kufanya mazoezi. Kabla ya kurudi darasani la mazoezi, mama anaweza kufanya mazoezi mepesi kama kutembea kwenye nyumba. Hata hivyo, ni muhimu kwa mama kutojishinikiza.

4. Pata usaidizi

Wiki chache baada ya kujifungua, marafiki na jamii watajaribu kumsaidia mama kumtunza mtoto na kufanya kazi za nyumbani. Kama vile kusafisha nyumba, mavazi na vyombo. Kubali usaidizi huu ili upate wakati zaidi wa kuwa na mtoto wako. Mwili wa mama unahitaji kupumzika ili upone kutokana na mchakato wa kujifungua.

Kwa wanawake wasio na watu wa kuwasaidia, wanaweza kuwaajiri watu wa kazi.

Ikiwa mama anatatizika na kusombwa na mawazo baada ya kujifungua, ni vyema kuwasiliana na wataalum wa afya kupata usaidizi mapema iwezekanavyo.

Chanzo: WebMD

Soma Pia:Jinsi Ya Kuongeza Maziwa Ya Mama: Vidokezo Kwa Mama Mpya

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Becoming a Mama
  • /
  • Jinsi ya Kutunza Mama Mpya Baada ya Kujifungua
Share:
  • Vidokezo 5 vya Kupata Mimba kwa Wanandoa Wanaolenga Kuwa Wazazi

    Vidokezo 5 vya Kupata Mimba kwa Wanandoa Wanaolenga Kuwa Wazazi

  • Njia 5 za Kujitayarisha kwa Uchungu wa Mama

    Njia 5 za Kujitayarisha kwa Uchungu wa Mama

  • Vitu Vya Kufanya Kabla ya Kuenda Hospitali Kujifungua

    Vitu Vya Kufanya Kabla ya Kuenda Hospitali Kujifungua

  • Vidokezo 5 vya Kupata Mimba kwa Wanandoa Wanaolenga Kuwa Wazazi

    Vidokezo 5 vya Kupata Mimba kwa Wanandoa Wanaolenga Kuwa Wazazi

  • Njia 5 za Kujitayarisha kwa Uchungu wa Mama

    Njia 5 za Kujitayarisha kwa Uchungu wa Mama

  • Vitu Vya Kufanya Kabla ya Kuenda Hospitali Kujifungua

    Vitu Vya Kufanya Kabla ya Kuenda Hospitali Kujifungua

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it