Jinsi Ya Kutunza Watu Walio Na Covid-19 Nyumbani Bila Kuambukizwa Maradhi Haya

Jinsi Ya Kutunza Watu Walio Na Covid-19 Nyumbani Bila Kuambukizwa Maradhi Haya

Japo nchi ya Nigeria na ndugu zake wa Kiafrika wanapo anza hatua za kuweka lockdowns kama njia ya kuthibiti kusambaa kwa virusi vya corona, tunafanya juhudi zetu za kubaki manyumbani mwetu. Huku tukiwa na matumaini kuwa hamna kati ya jamaa zetu watakao pata virusi hivi hatari. Walakini, kwa sababu ishara hizi hazionekani mbio, kuna uwezekano kuwa mwana familia huenda akawa amepata virusi hivi kabla ya lockdown. Na watu wengi wanao pata virusi hivi wanapata dalili nyepesi tu, na wataalum wanasema kuwa watu kama hawa wanapaswa kubaki nyumbani na kutoka pale tu wanapozidiwa na wanahitaji matibabu. Kwa hivyo, unafanya nini iwapo mwana jamii wako ameathiriwa na virusi vya corona? Fahamu jinsi ya kutunza mtu aliye na Covid-19 nyumbani.

Jinsi ya kutunza mtu aliye na Covid-19 nyumbani

how to care for a person with coronavirus

Picha: Shutterstock

Kufuatia vituo vya matibabu kuwa na wagonjwa wengi zaidi hadi vinakosa nafasi za watu wengine, wataalum wanashauri kuwa wagonjwa wanapaswa kubaki nyumbani ikiwa dalili zao si mahututi. Hospitali nyingi zimajazana na wagonjwa wengi walio na dalili zilizo zidi za virusi vya corona. Huenda ikawa ni kielezo dhabiti kwa nini mwanamme kutoka New York aliweza kuficha dalili zake ili aweze kupita kumwona bibi yake aliyekuwa amejifungua katika Hospitali ya Strong Metropolitan iliyoko Rochester. Kutoka wakati huo, hospitali hiyo imeweka thibiti zaidi kwa wageni wanao ingia hospitalini hiyo.

Katika nchi ya Nigeria, wataalum tayari wanabashiri kuwa utunzaji wao wa afya utakuwa na idadi nyingi ya visa vya wagonjwa wa virusi vya corona kupiku uwezo wao. Hii ina maana kuwa ni muhimu kutunza walio na dalili nyepesi nyumbani. Iwapo yeyote kati ya wanajamii wako anaugua virusi hivi, ama anaanza kuonyesha ishara, Kituo cha Kuthibiti Magonjwa (CDC) kina shauri kufuata hatua zifuatazo:

  • Angalia dalili

Watu huenda wakawa wagonjwa na virusi hivi kati ya siku 1-14 kabla ya kuonyesha dalili. Baadhi ya dalili zilizo kawaida zaidi za maradhi ya virusi vya corona ni kama vile joto jingi, uchovu na kikohozi kilicho kauka. Na karibu asilimia 80 ya watu wanapona kutokana na virusi hivi bila matibabu ya kinyumbani wakati ambapo asilimia 1 ya watu wanaugua zaidi. Kesi dharura kwa mara nyingi zina ongezeka na kuwa mbaya zaidi baada ya siku 5 hadi 10 baada ya kuonyesha dalili. Kwa hivyo angalia mgonjwa aliye athirika kwa umakini na iwapo hali yao inazidi kudhoofika, mpigie daktari wako. Uchungu ama shinikizo kwenye kifua, upungufu wa pumzi na kuchanganyikiwa ni ishara za mtu anaye hitaji matibabu ya dharura.

care covid-19 home

Image: Shutterstock

  •  Epuka kusambaa kwa virusi hivi

Kitu cha kwanza unacho paswa kufanya iwapo mtu aliye karibu nawe anathibitisha ishara za homa ya corona, watenge kwenye chumba kimoja. Huku kuna maana kuwa umweke mgonjwa huyo kwenye chumba tofauti cha kulala. Hakikisha kuwa chumba hicho kina hewa tosha. Walakini, huenda ikawa kuwa nyumba yenu sio kubwa kiasi hicho na inawabidi kutumia bafu moja. Katika kesi hii, hakikisha unaisafisha bafu ile baada ya mwanajamii aliye athirika kuitumia. Pia, epuka kutumia vitu kama kitambaa cha kujipanguzia, sahani ama blanketi na mtu mgonjwa.

coronavirus care

Picha: Pixabay

  • Tibu dalili

Kutibu dalili nyumbani kunahusisha kupata muda tosha wa kulala, kuepuka kutumia vileo na kunywa maji tosha ili mkojo wako uwe na rangi nyeupe. Usimkubalishe mtu aliye mgonjwa kufanya kazi nzito katika wakati huu. Pia, baadhi ya madawa ya kununua kwenye maabara yanaweza tumika kutibu dalili hizi. Ila, utahitajika kumwuliza mwuguzi wako kuhusu matibabu haya.

sanitizer lysol coronavirus

Picha: Unsplash

  • Amua wakati wa kuacha kumtenga

Kulingana na CDC, unapaswa kungoja siku tatu baada ya joto jingi ambayo mwathiriwa alikuwa akishuhudia kupungua bila kutumia dawa zozote. Pia, ngoja dalili kama vile kupunguka kwa pumzi kuimarika na ungoje siku saba baada ya kuthihirika kwa dalili. Kwa mfano, iwapo joto jingi ya mtu yule iliisha Ijumaa ila dalili zake za kwanza zilionekana Juma nne, unapaswa kungoja 7 ziishe baada ya Jumapili na ila sio Ijumaa.

kutunza mtu aliye na covid-19 nyumbani

Picha: Shutterstock

Moja wapo kati ya vitu ambavyo haviongelelewi unapo kuwa karantini ni upweke. Kwa hivyo unapo tunza mgonjwa, tafuta njia za kutangamana kijamii ili kuhakikisha hawahisi upweke.

Iwapo unagundua moja kati ya dalili hizi za COVID-19, tafadhali wasiliana na wizara ya afya kwa kutumia mojawapo ya nambari hizi.

  • Nambari sare: 0800 721 316
  • Whatsapp: +254 729 471 414
  • Nambari ya ujumbe mdogo: +254 732 353 535

Hakikisha unazingatia umbali unaotakikana unapokuwa kati ya watu na uwe salama. Je, una maswali yoyote? Tujulishe kwa kuwacha ujumbe mfupi.

Soma piaCoronavirus Survivor Stories: Nigerian Lady Shares Her Experience

Vyanzo: CDC , People

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Lydia Ume kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio