Sababu Kwa Nini Chuchu Zako Zinauma Zisizo Husika Na Saratani

Sababu Kwa Nini Chuchu Zako Zinauma Zisizo Husika Na Saratani

Wanawake wa umri nyingi wameshuhudia kuumwa na chuchu katika hatua moja ama nyingine maishani mwao kufuatia sababu ambazo wengi wao hawakufahamu.

Wanawake wa umri nyingi wameshuhudia kuumwa na chuchu katika hatua moja ama nyingine maishani mwao kufuatia sababu ambazo wengi wao hawakufahamu.

Ni kawaida kwa mwanamke kutia shaka anapo hisi uchungu kwenye chuchu zake. Unashauriwa kumwona daktari wako unapo hisi uchungu wa aina yoyote ile. Kwani huenda ukawa na tatizo sugu na kulipuuza kunaweza ibua matatizo zaidi. Ikiwa unahisi uchungu kwenye chuchu zako mara kwa mara, usiwe na shaka, kwani makala haya yata kuelimisha kuhusu vitu ambavyo vinasababisha uchungu huu.

Vyanzo Vya Kuumwa Na Chuchu

Uchungu wote kwenye chuchu haumaanishi kuwa uko katika hatari ya kupata ama una saratani. Lakini ni vyema kufanyiwa vipimo kudhibitisha chanzo chake.

  1. Homoni

kuchelewa kwa kipindi chako cha hedhi

Kwa wanawake, ni kawaida kushuhudia wakati ambapo homoni zinabadilika kwa sana. Kuna sababu nyingi zinazo wafanya wanawake kuhisi uchungu kwenye sehemu ya matiti. Kama vile vipindi vya hedhi, mbinu za kupanga uzazi ama hata kuwa na mimba.

Unapo kuwa katika kipindi chako cha hedhi, utagundua kuwa chuchu zako zinaanza kufura hasa siku ya tatu ama ya tano kabla ya kipindi chako kuanza. Na uchungu huu huisha baada ya kipindi chako kuanza. Chuchu kuuma ni mojawapo ya ishara za mapema za ujauzito. Ukihisi uchungu wa aina hii na kisha kukosa kipindi chako cha hedhi, hakikisha kuwa unachukua kipimo cha mimba.

2. Matibabu

antibiotics resistance

Ikiwa kuna dawa unachukua kutibu hali fulani ya kiafya, huenda ikawa dawa hizo zina sababisha athari hasi ya kuumwa na chuchu. Hasa kama dawa hizo zina homoni. Hakikisha kuwa una wasiliana na daktari wako akusaidie kufahamu dawa inayo sababisha mabadiliko ya homoni mwilini mwako.

3. Kunyonyesha

kuumwa na chuchu

Kunyonyesha mtoto ni chanzo kingine cha kuumwa na chuchu, kufuatia jinsi mtoto anavyo nyonya. Hasa katika siku za kwanza baada ya kujifungua, wanawake wengi hukiri kuwa siku za kwanza za kunyonyesha huwa na uchungu mwingi.

4. Saizi ya sindiria

Sababu Kwa Nini Chuchu Zako Zinauma Zisizo Husika Na Saratani

Kutofahamu saizi ya bro unayo paswa kuvalia kutafanya ununue saizi ndogo zaidi. Unapo valia saizi ndogo kukuliko, nafasi kubwa ni kuwa utahisi uchungu kwenye chuchu kwa sababu sindiria hiyo ina kubana.

Ni muhimu sana kwa kila mwanadada kufahamu saizi inayo mfaa. Ili uwe na starehe unapo fanya kazi zako za kila siku, na pia kuepuka kuhisi uchungu wa aina hii. Kuna duka za mavazi ya ndani zinazo wapima wanawake kuwasaidia kufahamu saizi itakayo wafaa zaidi.

Kumbuka kuwa ikiwa una hisi uchungu kwenye chuchu zako, hizi ni baadhi ya vyanzo vinavyo sababisha. Hakikisha kuwa una wasiliana na daktari wako ili ufanyiwe vipimo vinavyo faa. Vipimo vitakusaidia kuwa na uhakika wa chanzo na pia utafahamu jinsi ya kutatua tatizo hilo.

Chanzo: WebMD

Soma pia:Jinsi Ya Kufungua Chuchu Za Mama Zilizo Ziba

Written by

Risper Nyakio