Vyanzo Vya Kuumwa Na Kitovu Katika Mimba

Vyanzo Vya Kuumwa Na Kitovu Katika Mimba

Sababu kwa nini una hisi uchungu kwenye kitovu chako huenda kukalingana na umbo la mwili wako.

Wanawake wanaweza shuhudia maumivu na kukosa starehe tofauti katika safari yao ya ujauzito. Kama vile kuumwa na kitovu katika ujauzito. Tuna kueleza kwa nini kitovu chako huenda kikauma, jinsi ya kutuliza uchungu huu na wakati unapo stahili kwenda hospitalini.

Unayo tarajia

Unapokuwa mjamzito, mwili wako hupitia mabadiliko tofauti kila mwezi. Kuna wanawake ambao kamwe hawashuhudii kuumwa na kitovu katika mimba. Huku wengine waki hisi uchungu huo katika ujauzito mmoja na kukosa katika huo mwingine. Hata kama uchungu huu hauna starehe, usiwe na shaka, kwani ni kawaida katika mimba. Mara nyingi, huanza tumbo yako inapo anza kunenepa, na mara nyingi katika trimesta yako ya pili ama ya tatu.

Kinacho sababisha

Sababu kwa nini una hisi uchungu kwenye kitovu chako huenda kukalingana na umbo la mwili wako, unavyo beba mimba na uwezo wa kunyoosha wa mwili wako. Ama matatizo ya kiafya. Mara nyingi, uchungu huu hauna athari hasi na huisha baada ya wakati ama unapo jifungua.

Sababu za kuumwa na kitovu katika ujauzito

kuumwa na kitovu katika mimba

Kunyooka kwa mwili

Ngozi na misuli yako imenyooshwa hadi mwisho unapo wadia mwisho wa ujauzito wako. Unaweza pata alama za kunyooka, kuhisi kujikuna na uchungu unapo pitia katika hatua hizi za ukuaji wa kasi. Na kwa sababu kitovu kiko katikati, kita athiriwa na mabadiliko haya yote.

Shinikizo kutoka kwa uterasi

Katika trimesta yako ya kwanza, uterasi bado huwa ndogo na huwa haifiki kwa mfupa wa pubic. Inapo zidi kumea, na kuanza kuonekana, shinikizo kutoka ndani ya mwili wako husukuma kitovu chako nje.

Unapofika trimesta yako ya tatu, uterasi huwa juu ya kitovu chako. Ina sukuma mbele uzito wa mtoto.

Kutatua kuumwa na kitovu katika mimba

kuumwa na kitovu katika mimba

Uchungu kwenye kitovu chako huja na kuisha unapo zidi kushuhudia hatua za ukuaji wa kasi. Baadhi ya wanawake huenda waka zoea shinikizo na kunyooka mapema. Kwa wengine, uchungu huwa mwingi katika wiki za mwisho ambapo tumbo yako ni kubwa zaidi. Jaribu kulala kwa upande ama kuegemeza tumbo yako na mto. Kuna mishipi ya kujiegemeza ambayo inaweza kusaidia kupunguza uchungu kwa mgongo na tumbo ukiwa umesimama. Kuna mafuta ya kusugua ujauzito iliyo salama kwa ngozi unapo hisi kujikuna.

Wasiliana na daktari unapo:

  • Hisi joto jingi
  • Kuhisi kutapika
  • Kuvimba
  • Kuumwa na tumbo
  • Kuvuja damu

Chanzo: WebMD

Soma Pia: Kukwazwa Kimawazo Ukiwa Na Mimba Na Matibabu Yake

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio