Kuumwa Na Miguu Katika Ujauzito Unapokuwa Umelala

Kuumwa Na Miguu Katika Ujauzito Unapokuwa Umelala

Kuumwa na miguu katika ujauzito ni kawaida sana hasa katika trimesta ya pili na ya tatu. Mama Mjamzito anaweza epuka uchungu huu kwa kunywa maji moto.

Huenda ikawa umeanza kushuhudia kuumwa na miguu katika ujauzito ukiwa umelala. Lakini jaribu usitie shaka. Mwili wako unapitia mabadiliko mengi katika ujauzito na huenda ukahisi uchungu kwenye misuli yako ya miguu.

Maumivu huenda yaka anza kukuandama katika trimesta ya pili na ya tatu ya ujauzito wako, na hasa usiku. Kila kipindi huenda kikaa kwa angalau sekunde 10 hadi 15. Kutatua tatizo hili la kuumwa na miguu katika ujauzito, ni vyema kwanza kwako kuelewa kinacho sababisha maumivu haya.

Sababu za kuumwa na miguu katika ujauzito ukiwa umelala

Wataalum wa kimatibabu bado wanafanya utafiti wa kinacho sababisha maumivu ya miguu katika ujauzito. Walakini, baadhi ya wakunga hudhania kuwa maumivu haya yana sababishwa na shinikizo kwenye misuli, mara nyingi inayo sababishwa na uzito wa mtoto. Huenda ikawa pia ni kwa sababu ya mabadiliko katika mzunguko wa damu. Na usisahau kuwa, fetusi inayo endelea kukua ina shinikiza mishipa ya damu na neva inayo elekea kwenye miguu.

Masomo ya utafiti pia ina laumu kukosa kalisi mwilini kusababisha tatizo hili. Hata kama wataalum wanasema kuwa huenda ikawa ni kwa sababu ya mabadiliko kwenye njia ambayo mwili wa mwanamke huchakata kalisi.

Vidokezo vya kuepuka maumivu ya miguu unapokuwa na mimba

Kwa bahati nzuri, kuna hatua zilizo dhibitika na salama za wanawake kuchukua kuepuka maumivu haya. Hizi ni kama vile:

  1. Kula lishe yenye afya

Wataalum wa lishe wana shauri nafaka nyingi, wanga, matunda, njugu, mboga, samaki yenye ufuta na protini za mimea. Epuka chakula kilicho chakatwa na sukari ya kuongeza. Hakikisha kuwa unapata virutubisho tosha kuepuka nafasi za kuugua maumivu ya miguu unapokuwa mjamzito katika usingizi wako. Lengo ni kula vyakula vyenye afya na kuepuka matatizo katika safari yako ya ujauzito na kujifungua.

2. Kula nyongeza za lishe

Baadhi ya wakati, huenda ikawa vigumu kupata nyongeza muhimu za virutubisho na kubadili mahitaji ya mwili. Hii ndiyo sababu kwa nini kliniki na hospitali huwashauri wanawake wajawazito kula nyongeza za virutubisho. Tembe hizi huimarisha afya ya mwanamke kwa kupunguza nafasi za kukosa damu tosha mwilini. Kalisi na magnesium huwa muhimu katika kuepuka na kutibu maumivu ya miguu ukiwa umelala.

3. Husisha mazoezi kwenye ratiba yako ya kila siku

mazoezi ya trimesta ya tatu ya ujauzito

Hii ni mojawapo ya njia rahisi zaidi za kuepuka maumivu haya ya miguu katika safari yako ya mimba. Mazoezi yana imarisha mzunguko wa damu kwenye misuli ya miguu. Wataalum wa mazoezi wana shauri mazoezi mepesi kama vile kutembea, kujinyoosha na kuchuchuma.

Kwa sababu utahisi maumivu ya miguu mara nyingi wakati wa usiku, unapaswa kutenga wakati wa kufanya mazoezi machache kabla ya kuingia kitandani. Hakikisha kuwa una fanya mazoezi na mtaalum na pia kuwasiliana na daktari wako.

4. Valia stockings nzuri

Zinasaidia na mzunguko wa damu kwenye miguu. Kuvalia kwa njia inayo faa kutasaidia kuepuka maumivu ya miguu unapo tarajia.

5. Chukua hatua kubadili unavyo keti na kusimama

Kukaa na kusimama kwa muda mrefu kunaweza sababisha maumivu ya miguu. Hakikisha kuwa unabadilisha kati ya kukaa na kusimama baada ya kila dakika 15.

6. Kunywa maji tosha

maji tosha mwilini ukiwa na mimba

Kiwango kinacho shauri kwa wanawake wajawazito ni glasi nane kila siku. Kwa nyakati nadra kama vile kesi za shinikizo ya chini ya damu, daktari anaweza shauri hadi lita 5 za maji. Maji ni tiba nzuri ya maumivu ya miguu katika ujauzito. Hakikisha kuwa maji yako ya kunywa ni safi na salama ya kunywa.

7. Oga kwa kutumia maji moto

Kuoga kwa maji moto ni njia bora ya kuboresha mzunguko wa damu mwilini na pia kuifungua mishipa yako ya damu kwenye miguu. Na kuepusha maumivu ya miguu ukiwa umelala.

Kuumwa na miguu ukiwa na mimba huenda kukawa kama ndoto mbaya usipo tatua tatizo hili vyema. Kwa bahati nzuri, unaweza suluhisha shida hii kwa kufuata vidokezo muhimu tulivyo angazia kwenye makala haya. Hizi ni njia zilizo jaribiwa na kudhibitishwa kusaidia kupunguza maumivu ya miguu katika mimba.

Chanzo: Research Gate

Soma Pia:Matatizo Ya Ujauzito Yanayo Wakumba Wanawake Afrika

 

Written by

Risper Nyakio