Kuumwa Na Miguu Katika Ujauzito Ukiwa Umelala

Kuumwa Na Miguu Katika Ujauzito Ukiwa Umelala

Maumivu ya mwili katika ujauzito mara nyingi hushuhudiwa katika trimesta ya pili ama ya tatu. Na mara nyingi wakati wa usiku.

Wanawake hupitia mambo tofauti katika safari zao za ujauzito. Mojawapo ya vitu wanavyo vipitia ni kuumwa na miguu katika ujauzito ukiwa umelala. Lakini je, hili ni jambo la kuwatia wasiwasi ama la? Usiwe na shaka. Kwani mwili wako unapitia mambo mengi katika ujauzito na huenda utahisi uchungu na kuumwa kwenye misuli ya miguu.

Maumivu ya mwili katika ujauzito mara nyingi hushuhudiwa katika trimesta ya pili ama ya tatu. Na mara nyingi wakati wa usiku, kwa angalau sekunde kumi na tano hadi dakika 10. Ili kukabiliana na tatizo hili la maumivu, ni vyema kwako kufahamu kinacho sababisha maumivu haya.

Vyanzo vya kuumwa na miguu katika ujauzito ukiwa umelala

kuumwa na miguu ukiwa umelala katika ujauzito

Wataalum wa matibabu wanazidi kufanya utafiti zaidi kudhibitisha vyanzo vya maumivu ya miguu katika ujauzito. Walakini, kuna baadhi ya wakunga na madaktari wanao amini kuwa hali hii ina sababishwa na uzito mwingi unao shinikizwa kwenye miguu. Pia, ukosefu wa viwango vya kalisi tosha mwilini huenda vika sababisha tatizo hili.

Vidokezo vya jinsi ya kupunguza maumivu kwenye miguu katika ujauzito

  1. Kula chakula bora chenye afya

kuumwa na miguu ukiwa umelala katika ujauzito

Wataalum wa lishe wana shauri kuwa, mama mjamzito ana stahili kula nafaka nzima, wanga zenye fiber ya juu, matunda, njugu, mboga, samaki na protini zinazo tokana na mimea. Epuka kula chakula kilicho chakatwa na chenye sukari na ufuta mwingi. Hakikisha kuwa chakula chako kina virutubisho tosha ili kuongeza nafasi zako za kuepuka maumivu ya miguu katika ujauzito ukiwa umelala.

2. Kunywa tembe za virutubisho

Ni vyema wakati wote kuhakikisha kuwa una kula chakula chenye virutubisho bora. Kuna nafasi kuwa huenda chakula hicho kikakosa aina ya virutubisho na idadi inayo hitajika mwilini mwako hasa ukiwa na mimba. Ni vyema kuwasiliana na daktari wako atakaye kushauri tembe bora za kuongeza kwenye lishe yako. Tembe za virutubisho vya kalisi na magnesium vitasaidia kutibu na kuepuka maumivu ya miguu ukiwa na mimba.

3. Fanya mazoezi mepesi

Hii ni njia rahisi na yenye uhakika ya kupunguza uchungu unaohisi kwenye miguu katika mimba. Mazoezi yana boresha mzunguko wa damu mwilini hadi kwenye misuli ya miguu yako. Na kukusaidia kulala vyema zaidi wakati wa usiku. Kumbuka kufanya mazoezi mepesi katika kipindi hiki. Kama vile kutembea kwa angalau dakika 30 kila siku. Wasiliana na mtaalum wa mazoezi akuongoze.

Kumbuka kunywa maji tosha kila siku, koga kwa maji ya vuguvugu kutuliza misuli ya mwili wako na utumie mito mizuri, ili kupunguza kuumwa na miguu ukiwa umelala katika ujauzito.

Chanzo: Research Gate

Soma PiaJe, Ni Yapi Ungependa Kujua Kuhusu Ujauzito?

Written by

Risper Nyakio