Ishara Kumi Za Kuungua Nishati Kwa Wazazi Ambazo Unaweza Kuhusiana Nazo

Ishara Kumi Za Kuungua Nishati Kwa Wazazi Ambazo Unaweza Kuhusiana Nazo

Like job burnout, parental burnout comes with a set of specific symptoms. But what makes the problem worse is that parents are often ashamed and guilty about it.

Malezi ni jambo mojawapo ngumu sana duniani.  Na pia inaweza kupita kiasi wakati mwingine, hii ndio sababu kuna kitu kama kuungua nishati kwa wazazi. Kulingana na ScienceDaily, kuungua nishati kwa wazazi ni “machovu makali ambayo huwafanya wazazi kuhisi kuwa mbali na watoto wao na kutokuwa na uhakika juu ya uwezo wao wa kulea.” Ishara za kuungua nishati kwa wazazi hutokea mara nyingi na pengine hukaribiana na tukio lililompata mama huyu.

Mama mmoja ameweza kukiri kuwa alikuwa amechanganyikiwa kwenye haraka ya kuwapeleka watoto shule ata akajipata ameenda shuleni bila watoto. Huyu mama asiyejulikana alijichukua video huku akicheka akionyesha viti vya nyuma ya gari lake vilivyokuwa bila watoto; akieleza kuwa alikuwa ‘bado usingizini hiyo asubuhi’ na akaendesha gari hadi shuleni bila watoto.

Kuungua nishati kwa wazazi

Watoto hawako kwenye gari,’ akasema kwa video iliyosambaa hapa chini. ‘Naendesha gari kuelekea shuleni bila watoto wangu! ‘Nawapeleka watoto shuleni na hata siko nao kwenye gari. Lazima nilirudi nyumbani kuwachukua.’

 

Huyu mama anaitikia kuwa aliingia tu kwa gari na akaenda. Si wazi ilichukua muda gani kwake kugundua kuwa hakuwa amebeba watoto.

Kila mzazi anafaa kuelewa ishara za kuungua nishati na aweze kupata msaada haraka iwezekanavyo. Hii ndio maana tumeweka pamoja orodha ya ishara za kuungua nishati kwa wazazi ili uweze kuziona. Ebu ziangalie hapa chini:

Angalia Ishara Hizi Kumi Za Kuungua Nishati Kwa Wazazi

Kuungua nishati kwa wazazi

Ishara moja ambayo huweza kuonekana mapema ni machovu makali ya kimwili na kiakili. Ishara zingine za kuungua nishati ni kama zifuatazo:

 • Mawazo ya kujiua na akili ya kukimbai; kujihisi umefungwa
 • Kuongezeka kwa tabia za uraibu
 • Matatizo ya kiafya
 • Nafasi kubwa ya wasiwasi na mkazo wa akili
 • Hisia za kuungulika
 • Kukasirika upesi na Kukosa furaha
 • Ukosefu wa usingizi
 • Kuongeza kwa mafurukano kati ya wazazi
 • Hisia za upungufu; kupoteza ule uwezo wa kupata utimilifu kwenye ulezi
 • Nafasi kubwa ya kutojali watoto ama tabia jeuri kwa watoto

Hizi hisia huwa mbaya haswa kama zinaharibu uwezo wako wa kufurahia watoto wako na kuwa na imani kwako kama mzazi. Pia, utafiti umeonyesha kuwa kuungua nishati kwa wazazi kunaweza kusababisha mkazo wa akili, hatari ya uraibu na kuzorota kwa afya. Cha mno, inaweza kuathiri uhusiano wako na watoto.

Kulingana na utafiti wa hivi majuzi, kiini cha kuungua kwa nishati kwa wazazi ni usawaziko katika ya mahitaji ya ulezi na mafanikio yake.  “Mara tu huu usawaziko unapoegemea kwa upande hasi ama wa maafa (i.e athari zinapita manufaa), wazazi wanaanza kukubwa na ishara za kuungua kwa nishati kwa kila siku,” wakaandika waandishi wa utafiti wa 2018.

Ingawaje, “mom burnout” huwa kawaida sana kwani kina mama ndio Kimsingi watunzaji wa watoto, kina baba pia wako katika hatari ya kuungua nishati wanapohusishwa katika maswala ya ulezi. Katika utafiti mmoja wa wazazi 2000, asilimia 63 walisemekana kukubwa na kuungua nishati kutokana na malezi.

 Nini unachoweza kufanya iwapo umeungua nishati kutokana na malezi

Kuungua nishati kwa wazazi

Tafuta amani

kwa kweli, ratibisha matembezi. Kwa usiku mmoja ama mbili – ama masaa tu. Kumekuwa na utafiti mwingi unaoonyesha manufaa ya afya kwa akili unapotembea nje na marafiki kwa siku mbili kila wiki. Kwa hivyo sahau hatia na mwache baba mtoto amshughulikie ili uweze kupata mwanya wa kupumzika. Iwapo huwezi  kuponyoka usiku, basi kunywa glasi ya divai na utembee nje ili kupata wakati peke yako. Tunasisitiza.

Punguza mambo unaofanya

Iwapo haileti furaha, iweke mbali nawe. Ni wakati wa kwenda Marie Kondo katika maisha yako na upunguze hayo mambo ambayo huleta mkazo wa akili. Hili linaweza kumaanisha kupunguza mazoezi ya watoto wako ama kutojihusisha na chama cha P&F. Ni sawa kutokaa kwa hio mikutano. Ata zaidi, ni bora kuliko sawa!

Tafuta msaada wa nje

Ratibisha kuwa na mtu wa kusaidia kusafisha nyumba, tafuta magari kwa kina mama wengine ili isiwe lazima uendesha gari unapoenda na kurudi kutoka mazoezi, tafuta watu wanaotengeneza chakula ili kupunguza kupika chakula na kwenda kununua chakula.

Angazia jinsi ulivyo sawa kama mama

Badala ya kuwa na wasiwasi  juu ya kile ambacho hukuweza kutimiza ama kilichoenda mrama, fikiria juu ya mambo  yanayoweza kukusaidia. Je, watoto waliweza kupewa chakula leo? Walipendwa? Waliweza kumaliza siku kama hujawauuza? Hivyo basi ulifanya vizuri, mama.

Tafuta usaidizi

Iwapo unahisi machovu kila wakati na unasikia kama hili jambo la uzazi limekuwa ngumu sana (we feel ya!), zungumza na GP wako kulihusu. Unaweza kuwa unahitaji zaidi ya usiku mmoja na marafiki zako, na iwapo hii ndio hali, GP ndiye mtu wa kwanza unafaa kuzungumza naye.

Kina mama wote hupoteza utulivu wao mara kwa mara. Haswa kama watoto wana tabia mbaya. Lakini iwapo ni mbaya zaidi, onyesha bendera nyeupe na utafute msaada. Ama, kwa uchache kabisa tafuta usiku nje, kwenye hoteli. Peke yako.

Nini huongeza hatari ya kuungua nishati katika malezi?

kuungua nishati kwa wazazi

 • Kuwa sawa katika kila jambo : kuhisi kuwa unafaa kuwa “perfect” kama mzazi kila wakati
 • Ukosefu wa msaada kutoka kwa mzazi mwenzi
 • Wazazi wote kufanya kazi nje ya nyumbani
 • Matatizo ya kifedha
 • Ukosefu wa msaada wa kutosha kutoka nje ya familia.(watunzi watoto na Jamii, na mengineyo)
 • Kupata wakati mgumu kutafuta msaada
 • Watoto wenye mahitaji mengi
 • Historia ya wazazi wenye matatizo ya kutojali

Daily Mail UK Psychology Today

Soma Pia: ‘Smiling depression’ is very real, and it’s more dangerous than you think

Written by

Risper Nyakio