Sababu Zinazosababisha Maumivu ya Kichwa Baada ya Kuvaa Miwani Mpya

Sababu Zinazosababisha Maumivu ya Kichwa Baada ya Kuvaa Miwani Mpya
Je, kuvaa miwani mpya kuna athari zozote?Je, unahisi maumivu ya kichwa kila wakati unapovaa miwani mpya? Hizi ndizo sababu zinazo sababisha maumivu ya kichwa unapovaa miwani mpya, na njia za kuzuia maumivu haya.
Sababu zinazo sababisha maumivu ya kichwa baada ya kuvaa miwani mpya.
 
kuumwa na kichwa kufuatia kuvalia miwani
Ni jambo la kawaida iwapo miwani yako inasababisha maumivu ya kichwa (fashion Eyeglass world)

Miwani ni muhimu kwa kusaidia mtu kuona, lakini wakati mwingine unapatwa na maumivu ya kichwa baada ya kuvaa miwani na kusababisha usumbufu wakati mtu anapofanya kazi yake

Watu wengi wanaovaa miwani iliyo amuriwa na daktari wanafanya hivi kwa sababu ya makosa ya kinzani, kama wataalum wa macho wanavyosema, haya ni makosa ya umbo la jicho na  hii huadhiri au kupunguza nguvu ya kuona kwa jicho hilo.

kuvaa miwani mpya

Ni jambo la kawaida kama miwani yako mpya inasababisha maumivu ya kichwa (Fashion Eyeglass World)

Utafiti unaonyesha kwamba macho yetu yatazoea kwa urahisi sana kuona kutumia miwani ambayo umetumia kwa muda mrefu. Lakini ni tofauti ukilinganisha na miwani mpya. Kama unavaa miwani mpya kwa wakati wako wa kwanza, ama unatumia miwani tofauti ya ile ambayo uliashauriwa na daktari, hapo awali. Macho yako yatasahau mbinu ambazo yalikuwa yanatumia hapo awali, ili kuona ulimwengu kwa urahisi na vizuri bila matatizo iwezekanavyo.

Kubadilisha na kutumia miwani mpya kama ulivyoshauriwa na daktari ni jambo ambalo ni rahisi sana. Wakati ambapo uzoefu wako wa miwani mpya unakua unaeza pata mtazamo usiodhahiri. Dalili hii haiwezi epukika kwa kusababisha maumivu ya kichwa. Wanaovaa miwani wanaweza chukua muda wa wiki mbili ili kuzoea miwani hii mpya. Mahali unapoeka fremu zako panaweza sababisha maumivu haya ya kichwa. Daktari wako wa macho anapaswa kutengeza fremu za miwani vizuri ili kutoshea usoni mwako vizuri na kuwa na nafasi ya kutosha kutoka kwa macho yako.

kuvaa miwani mpya

Maumivu madogo ya kichwa kutokana na miwani mpya ambayo huisha baada ya siku za kwanza kadhaa hounekana kuwa dalili ya kawaida. Lakini si jambo la kawaida unapopatwa na maumivu haya kisha yaongezeke, ama upate shida ya kuona vizuri.

Jinsi ya kutatua shida ya kuumwa na kichwa

Hauwezi epuka kutumia miwani kufuatia kuhisi usumbufu wa aina fulani unapoivaa .Unapaswa kupatwa na urahisi wa kuvaa miwani mpya kila wakati. Kama inavyoshauriwa, kuvaa miwani kwa muda wa masaa matatu au manne kisha kuchukua muda wa mapumziko kwa siku kadhaa itasaidia uzoefu wako kwa miwani mpya.

 

This article was republished with permission from Pulse.Ng

Written by

Risper Nyakio