Kuvimba Kwa Wajawazito: Kilicho Na Kisicho Kawaida

Kuvimba Kwa Wajawazito: Kilicho Na Kisicho Kawaida

Hadi hivi juzi, kuvimba ilikuwa mojawapo ya ishara zilizo tumika kutambua ugonjwa wa preeclampsia, hali ya shinikizo la juu la damu katika mimba.

Walikuonya kuhusu kichefu chefu. Ulifahamu kuwa unge ongeza uzito. Lakini hakuna lililo semwa kuhusu vidole vilivyo fura. Na mashavu, mashavu ya miguu na vifundo vya miguu. Kuvimba kwa wajawazito na wakati wa kuwa na shaka, ni kawaida kuliko unavyo fikiria.

Mbali na mtoto wako, placenta yako na ongezeko la hifadhi la ufuta, mwili wako una jitihada kazini. Unatengeneza damu zaidi na viowevu kusaidia kuegemeza ukuaji wa mtoto. Ukihusisha mabadiliko yote mwili wako una shuhudia. Viowevu hivi zaidi vinaweza kufanya ukae, na uhisi ume vimba. Hali ambayo madaktari huita edema.

Mtoto wake anaye kua na uterasi zina shinikiza mfumo wako wa mzunguko na wa lymphatic. Na huenda kukachangia kuvimba pia. Baadhi ya wanawake huanza kushuhudia kuvimba kule mapema, lakini mara nyingi hushuhudiwa katika trimesta ya pili na ya tatu. Hata kama tuna uwezo wa kudhibiti kidogo kufura huku, baadhi ya vitu ambavyo vinaweza ongeza kuvimba katika mimba ni kama vile:

 • Kusimama kwa muda mrefu
 • Kufanya kazi kwa muda mrefu
 • Joto jingi
 • Kula sodium nyingi (chumvi)
 • Viwango vya chini vya potassium
 • Viwango vya juu vya kaffeini

Wakati ambapo kuvimba kwa wajawazito kunapaswa kuwa jambo la kuhofia

kuvuja damu kwa wajawazito

1.Preeclampsia

Hadi hivi juzi, kuvimba ilikuwa mojawapo ya ishara zilizo tumika kutambua ugonjwa wa preeclampsia, hali ya shinikizo la juu la damu katika mimba. Sio mojawapo kati ya hali zinazo tumika kugundua ugonjwa huo - ilihali wanawake wengi walio na shinikizo la juu la damu wana vimba. Ukifikiria kuwa uso wako una nenepa, tafuta picha yako muda kabla kupata mimba na umwonyeshe daktari wako. Na ikiwa kuvimba kwenye mikono na miguu yako kuna zidi, unaweza gundua pitting edema (unapo finyilia kidole chako cha gumba kwenye ngozi yako, alama inabaki kwa sekunde chache) ama miguu yako kukosa rangi. Unapo gundua aina hii ya edema, mjulishe daktari wako.

2. Kuganda kwa damu

Kuganda kwa damu kwenye mishipa kunako fahamika kwa kimombo kama deep vein thrombosis (DVTs) kuna hatari za kuongezeka katika mimba. Hii ni kwa sababu mwili unatoa bidhaa zaidi zinazo husishwa na kuganda kwa damu. Ishara zingine za kuganda kwa damu ni kama vile uchungu, ugumu na kuwa nyekundu. Pia unaweza gundua kuwa mguu mmoja ume vimba kuliko mwingine. Uki shuku kuwa una ugua ugonjwa huu, wasiliana na daktari wako.

3. Maambukizi ya ngozi

Ukiugua maambukizi ya ngozi yanayo fahamika kama cellulitis, huenda pia ukawa na uvimbe na uchungu. Tena, hii inaweza kuwa sababu ya kupata huduma za kimatibabu bila kukawia.

Shaka zingine

Kuna matatizo mengine ambayo ni nadra ambayo yanaweza sababisha kuvimba, kama vile matatizo ya moyo na mafua. Ukiwa na shaka, ni vyema kuwasiliana na daktari kuhakikisha kuwa wewe na mtoto wako mko salama.

Jinsi ya kupunguza uvimbe

maji tosha mwilini ukiwa na mimba

 • Kunywa maji tosha kila siku kuhakikisha kuwa mwili wako haukosi maji (glasi 10 kwa siku) zinaweza saidia
 • Hakikisha kuwa una badilisha mtindo wa kukaa na kupumzika ikiwa unatembea ama kusimama kwa muda mrefu
 • Inua miguu yako mara nyingi kwa siku
 • Kula lishe yenye afya iliyo na viwango vichache vya sodium na chakula kilicho chakatwa.

Inapofika kwa kuvimba kwa wajawazito, wakati wa kumwona daktari?

 • Uchungu, kugeuka kuwa mwekundu na kuvimba sehemu fulani ya mwili
 • Mguu mmoja umefura kuliko mwingine
 • Kuvimba kwenye mikono na uso
 • Kuumwa na kichwa
 • Kuhisi kizungu zungu
 • Kuumwa na tumbo
 • Matatizo ya kupumua
 • Joto jingi

Soma PiaMatatizo Ya Ujauzito Yanayo Wakumba Wanawake Afrika

Written by

Risper Nyakio