Kumtunza mtoto baada ya kufanyiwa upasuaji huwa jambo gumu kwa mama. Ila, mara nyingi hana jambo lingine la kufanya. Siku za kwanza chache baada ya upasuaji wa c-section, mama huwa katika uchungu mwingi. Anastahimili uchungu huu ili aweze kumlisha mtoto wake. Mama anastahili kutunzwa na kujitunza na kuhakikisha kuwa anajitenga na mambo yatakayo shinikiza kidonda chake kingali kinapona. Kuvimbiwa hufanya uchungu wa kidonda chake uongezeke. Tazama jinsi ya kukabiliana na tatizo la kuvimbiwa baada ya upasuaji wa c-section.
Sababu za mama kuvimbiwa baada ya upasuaji wa c-section

Kutohisi haja ya kwenda haja baada ya kujifungua kwa njia ya upasuaji husababishwa na mabadiliko katika viwango vya homoni mwilini, kukosa maji tosha ama fiber kwenye lishe ya mama. Sababu zaidi ni kama vile:
- Dawa za kugandisha zinazotumika katika upasuaji
- Dawa ambazo mama anapatiwa kutuliza uchungu baada ya kujifungua
- Misuli ya pelviki kukosa nguvu
- Kukosa maji tosha mwilini baada ya kumnyonyesha mtoto
- Kuogopa kuhisi uchungu
Jinsi ya kupunguza kuvimbiwa baada ya upasuaji
Kuvimbiwa baada ya kujifungua huwa kwa siku tatu ama nne. Hivi ni baadhi ya vitu ambavyo vitakifanya kipindi hiki kisiwe kigumu sana kwa mama kwa kupunguza uchungu.
- Kunywa vinywaji vya vuguvugu

Kunywa kikombe kimoja cha maji ya vuguvugu yaliyo wekwa ndimu kila anapo amka. Kuna baadhi ya chai kama za chamomile ama zinginezo za mitishamba kuna saidia. Chai hizi husaidia kupunguza kuvimbiwa, gesi tumboni na kuongeza utoaji wa maziwa. Ni muhimu kwa mama kujitenga na unywaji wa maji baridi.
- Hakikisha lishe yako ina fiber

Fiber inasifiwa kwa uwezo wake wa kulinda dhidi ya kuvimbiwa. Baadhi ya vyakula vilivyo na fiber ni kama vile matunda, mboga za kijani na bidhaa za wanga ama nafaka nzima.
Mama aliyefanyiwa upasuaji wa c-section anastahili kula vyakula vingi vyenye iron kama vile kuku, nyama nyekundu, na maharagwe.
Ikiwa uchungu wako sio mwingi sana, jaribu kutembea kadri uwezavyo. Kwa dakika chake kwa siku. Kufanya hivi kunasaidia kupunguza gesi na kuvimbiwa. Iwapo daktari wako atakubalisha kulingana na kiwango cha uchungu wako, unaweza kujinyoosha kwa upole.

Kuwa na wasiwasi mwingi kunamfanya mama avimbiwe. Fanya mambo ya kupunguza mawazo kama kutembea, kujaribu meditation ama kusikiliza muziki. Ni vyema kwa mama kuhakikisha kuwa ana lala vya kutosha.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Mbinu Asili Za Kuondoa Michirizi Baada Ya Kujifungua