Watoto wanaozaliwa hulishwa maziwa ya mama. Ni rahisi kwao kuchakata kwani hawana meno na pia maziwa yana virutubisho vyote vinavyohitajika katika ukuaji wao. Ni vigumu kwa watoto wanaolishwa maziwa ya mama peke yake kutatizika na hali ya kuvimbiwa. Hii sio kumaanisha kuwa jambo hili haliwezi kufanyika. Kipi kinachosababisha kuvimbiwa katika watoto?
Dalili za kuvimbiwa katika watoto anayelishwa maziwa ya mama

Njia maarufu ya kufahamu iwapo mtoto anatatizika na kuvimbiwa ni kwa kuangalia mara ambazo anaenda msalani, yani mara ambazo mama anam-badili nepi. Hata hivyo, hii sio njia kamili ya kubaini tatizo hili katika watoto. Mtoto kuonekana kana kwamba anasukuma anapokunya, wakati wote, mtoto huonekana akifanya hivi na kukunja uso anapopitisha kinya.
Ishara bora kuwa mwanao anatatizika na kifunga choo ni kama vile:
- Kupitisha kinya sawa na mawe madogo magumu
- Tumbo gumu
- Kulia anapopitisha kinya
- Kukataa kula
- Kinya cha mtoto kuwa na damu
Vyanzo vya kifunga choo katika watoto
Mara nyingi, tatizo hili huanza katika watoto wanapofikisha miezi sita wanapoanzishiwa chakula kigumu. Baadhi ya vyanzo vya hali hii katika watoto ni kama vile:
Kunywa maziwa ya ng'ombe. Mara nyingi, watoto huanza kunywa maziwa ya ng'ombe wanapofikisha mwaka mmoja
Ndizi. Kumwanzisha mtoto ndizi huenda kukasababisha hali ya kufunga choo. Iwapo ungependa kumlisha mtoto wako chakula hiki punde tu baada ya kumuanzishia chakula kigumu, anza kwa kukichanganya na maji ama kumpa sharubati ya matunda pamoja na ndizi
Lishe isiyo na fiber. Fiber huchangia pakubwa katika kupitisha kinya kwa urahisi. Hakikisha kuwa lishe ya mtoto ina fiber tosha. Vyanzo bora vya fiber ni kama vile, mboga za rangi ya kijani kama mchicha na kienyeji
Jinsi ya kupunguza kufunga kinya katika watoto
Kutompa mtoto maji na viowevu tosha. Mama anapaswa kumnyonyesha mtoto kabla ya kumpa vyakula vigumu. Viowevu vinasaidia kinya cha mtoto kiwe rahisi
Mawazo mengi. Kubadili mazingira ya mtoto ama mazingira yake kuwa na joto kuliko ilivyokawaida yake huenda kukafanya afilisike kimawazo na kusababisha kuvimbiwa kwake
Maradhi. Mtoto kugonjeka wadudu wa tumboni wanaosababisha kutapika na kuendesha humfanya akose maji tosha mwilini na kuwa chanzo cha kufunga choo
Jinsi ya kulinda dhidi ya kifunga choo katika watoto

Lishe yenye fiber. Mlishe mtoto chakula chenye fiber kama mboga ama oats hasa unapomwanzishia chakula kigumu
Mpe viowevu tosha. Viowevu vinasaidia kinya cha mtoto kisiwe kigumu wala kumtatiza anapokipitisha
Kumpa mtoto masi ya tumbo. Kumpapasa mtoto chini ya kitovu chake kwa angalau dakika 2 mara kwa mara
Wakati wa kuwasiliana na daktari wa afya ya watoto
Mama anapaswa kumwona daktari kwa kasi anapogundua mtoto ana:
- Joto jingi
- Anakataa kula
- Kutapika ovyo
- Bado anavimbiwa na choo
- Ana tumbo iliyofura
Soma Pia: Vidokezo 5 Vya Kuwa Na Ujauzito Salama Na Wenye Afya