Kuvuja damu katika mimba ni suala nyeti na lisilo faa kupuuzwa wakati wowote ule. Mama mjamzito ana himizwa wakati wote kuwasiliana na daktari wake ama kutembelea kituo cha matibabu anapo shuhudia kuvuja damu katika mimba. Hata kama baadhi ya wakati huenda likawa sio jambo sugu, ni vyema kuwa na uhakika.
Sababu kuu za kuvuja damu katika mimba

Kuvuja damu katika trimesta ya kwanza hushuhudiwa kwa angalau asilimia 20 ya wanawake. Hizi ndizo sababu ambazo huenda zika sababisha hali hii:
Yai kujipandikiza kwenye kuta za uterasi:
Huenda uka shuhudia kiasi kidogo cha damu katika siku za kwanza sita hadi 12 baada ya kutunga yai. Katika wakati huu, yai linajipandikiza kwenye kuta za uterasi. Ni kawaida kwa wanawake kudhania kuwa hiki ni kipindi chao cha hedhi cha kawaida. Tofauti ni kuwa, damu hii huwa nyepesi zaidi ikilinganishwa na kiwango cha damu kinacho toka mwilini wakati wa hedhi. Tofauti nyingine ni kuwa, huenda ukashuhudia damu hii kwa masaa machache ama siku moja hadi 3. Gundua kuwa, damu hii haijazi pedi yako.
Kuharibika kwa mimba/ kupoteza mimba:
Mama huenda aka vuja damu katika mimba anapo poteza mimba aliyo kuwa amebeba. Mara nyingi hushuhudiwa katika wiki za kwanza 12 za ujauzito na huwa hofu kubwa zaidi katika kipindi hiki. Hii si kumaanisha kuwa kuvuja damu katika trimesta ya kwanza mara nyingi ni kufuatia kupoteza mimba. Mama aliye poteza mimba ata hisi uchungu mwingi tumboni na kupitisha tishu kwenye uke wake.

Mimba ya ectopic:
Mimba ya aina hii huwa nadra sana na hushuhudiwa katika asilimia 2 za ujauzito. Ni hatari sana kwa maisha ya mama. Katika aina hii ya ujauzito, yai lililo rutubishwa hujipandikiza nje ya uterasi na kwenye mirija ya mimba. Yai hili linapo zidi kukua, huenda mirija hii ika pasuka na kumhatarisha mama. Ishara zingine za aina hii ya mimba ni kuumwa sana na tumbo ama kuhisi kizungu zungu.
Ni vyema kuwa makini na afya na mwili wako katika kipindi hiki. Unapo gundua matokeo yasiyo ya kawaida, hakikisha kuwa una wasiliana na daktari wako kwa kasi.
Chanzo: healthline
Soma Pia:Jinsi Ya Kuongeza Nafasi Zako Za Kutunga Mimba