Sababu 6 Za Kuvuja Damu Mapema Katika Mimba

Sababu 6 Za Kuvuja Damu Mapema Katika Mimba

Kufanya ngono katika mapenzi kunaweza kuwa kwa kusisimua sana- na kuna himizwa! Lakini ukiona unatoa damu, huenda ikawa sio jambo kubwa

Unapokuwa na mimba, ishara yoyote ya kuvuja damu mapema katika mimba inatia wosia kwa kweli. Lakini usiwe na shaka: Kuvuja damu katika ujauzito ni kawaida kuliko unavyo dhania, na wakati mwingi sio jambo la kukutia wasiwasi. Kwa mfano huenda ukawa unafikiria,

Niko wiki ya nane ya ujauzito na kuona damu ninapo enda msalani, nitafanya nini? Tulia. Hicho ndicho unacho stahili kufanya.

kuvuja damu mapema katika mimba

Hata kama kuvuja damu mapema katika mimba ni kawaida na huenda kukawa kawaida kabisa, kunaweza kutia wasi wasi rohoni mwa mama anaye tarajia. Kuvuja damu katika mimba kuna tarajiwa katika visa vingi na kunaweza kuwa kawaida kabisa. Wakati mwingine, kuna ashiria mimba inayo toka, kupoteza mimba, tatizo la placenta ama uchungu za uzazi usio komaa.

Ni vyema kumtembelea daktari wako wakati wowote unapo shuhudia kuvuja damu. Unataka kuhakikisha kuwa wewe na mtoto wako mko salama. Lakini kabla ya kufikiria mabaya yoyote, hapa kuna baadhi ya vyanzo vya kuvuja damu katika mimba.

"Wiki 8 katika mimba na bado navuja damu ninapo enda msalani": Sababu za kuvuja damu mapema katika mimba

  • Kiinitete kinaji pandikiza

Sababu 6 Za Kuvuja Damu Mapema Katika Mimba

Mojawapo kati ya ishara za mapema za mimba ni kutoa damu kidogo. Kwa hivyo ikiwa una tarajia kutunga mimba lakini unapata kuwa unatoa damu kidogo wakati unapo tarajia kipindi chako cha hedhi, kuna uwezekano umefaulu. Kutoa damu huku ni kwa sababu kiinitete kina jipandikiza kwenye kuta za uterasi karibu siku 10-12 baada ya kurutubishwa. Kupevuka kwa yai hufanyika katikati mwa kipindi cha hedhi cha mwanamke cha siku 28. Na kujipandika hufanyika siku 10-12 baadaye. Kwa hivyo kutoa damu kunaweza dhaniwa kuwa hedhi. Tofauti ni kuwa huwa nyepesi zaidi na huwa siku moja ama mbili badala ya siku 5 hadi 7.

  • Una hedhi nyepesi

Hata kama inaweza onekana sio kawaida, huenda ukawa na hedhi ukiwa na mimba. Kuvuja damu kunaweza fanyika katika wiki 6 ama 8. Huu ndiyo wakati ambapo mwanamke huwa akitarajia kipindi chake cha hedhi. Hata baadhi ya wanawake waliofikisha umri wa ugumba huzidi kushuhudia vipindi vya hedhi. Sawa na mimba, mwili huendelea kuvuja damu kwa sababu ulikuwa umezoea hivi. Lakini, tofauti na hedhi ya kawaida, damu hii huwa nyepesi na yenye rangi ya hudhuringi.

  • Umefanya ngono

Kufanya ngono katika mapenzi kunaweza kuwa kwa kusisimua sana- na kuna himizwa! Lakini ukiona unatoa damu, huenda ikawa sio jambo kubwa. Ujauzito unapo zidi kukua, wanawake wengi wata vuja damu baada ya kufanya mapenzi. Hii ni kawaida na hutendeka kwa sababu kizazi hubadilika.

  • Umefanyiwa kipimo cha pelviki

Ikiwa una shaka kuhusu kuvuja damu baada ya kumtembelea daktari, usiwe na shaka. Kuvuja damu kunaweza fanyika baada ya sonogram ama kipimo cha pelviki na daktari wako ama na mtaalum wa afya. Kufuatia ongezeko la mzunguko wa damu kwenye uterasi na kizazi.

  • Una maambukizi

Wakati ambapo kuvuja damu wakati mwingine hakuna shaka, huenda pia kuwa na maana kuwa kuna suala nyeti. Kutoa damu kufuatia kupoteza mimba huanza katika wiki ya 6 ama 8 ya ujauzito. Huanza na damu kidogo, kuumwa na tumbo sana, kisha kipindi kizito kuliko cha kawaida.

Wakati wa kuwa na shaka

Kuvuja damu kwa ujumla, huwa na shaka kama ni damu nyingi, kuliko kipindi cha hedhi cha kawaida na kufuatiwa na kuumwa na tumbo.

Ni vyema kukumbuka kuwa kuvuja damu mapema katika mimba sio wakati wote ambapo kuna husishwa na kupoteza mimba.

Vyanzo: NHS,

 

Soma Pia:Kuumwa Na Miguu Katika Ujauzito Unapokuwa Umelala

Written by

Risper Nyakio