Mambo Ya Kutarajia Maji Yanapo Vuja Kabla Ya Kushuhudia Uchungu Wa Uzazi

Mambo Ya Kutarajia Maji Yanapo Vuja Kabla Ya Kushuhudia Uchungu Wa Uzazi

Kuna baadhi ya wanawake ambao huingia kwa uchungu wa uzazi kabla ya maji kuvuja. Katika kesi hii, daktari anaweza kuvujia maji. 

Unapo kuwa mjamzito, kuvuja  maji katika mimba kuna maana kuwa gunia la viowevu linalo mzingira limetoboka. Gunia la amniotic fluid linashikilia mtoto na kumweka salama anapo kua tumboni. Gunia hili linajulikana pia mkoba wa maji linalo tengeneza nafasi ya mwanao kukua, kumpa temprecha inayo faa na kulinda kitovu kutokana na kusukumwa.

Kuvuja maji katika mimba hutendeka lini?

Mambo Ya Kutarajia Maji Yanapo Vuja Kabla Ya Kushuhudia Uchungu Wa Uzazi

Mwili unapo jitayarisha kujifungua, maji ya mimba yana vuja na kutoka kupitia kwa uke wako. Mchakato huu unaweza fanyika kabla ya uchungu wa uzazi ama baada. Mchakato huu unapo fanyika, utahisi kizazi chako kina kuwa chembamba kisha kuwa kinene ili mtoto aweze kupita.

Maji yako yaki vuja kabla ya kubanwa huku kuanza, unashuhudia kupasuka kwa utando kabla ya uchungu wa uzazi (PROM). Mwanamke ataanza kuhisi kutamani kula ice cream baada ya maji yake kuvuja kwa kasi kabla ya kupitia kubanwa. Mara nyingi, huanza kwa kiasi kidogo na ila sio kama dimbwi la maji. Pia kunaweza fanyika baada ya uchungu wa uzazi kuanza. Bado ni muhimu kwa mama kujua ishara anazo tarajia.

Ishara za kuvuja maji katika mimba

Mchakato huu huhisi tofauti kwa kila mwanamke. Unaweza kugundua mambo haya:

  • Kutoka kwa kasi kana kwamba umejikojolea
  • Kutiririka kusiko isha
  • Kutoka maji kidogo
  • Kutiririka kunako anza na kukoma

Pia, mama anaweza hisi kuenda haja kubwa, lakini, kumbuka kuwa maji haya hayana harufu sawa na mkojo.

Mama anapaswa kufanya nini akivuja maji?

Ukishuku kuwa maji yako yame vuja, valia pedi(sawa na ya hedhi) kisha uwasiliane na mkunga wako ama daktari anaye kushughulikia. Ata kushauri kwenda ofisini mwao ama kufika kwenye kituo cha afya. Kama hawana uhakika kuhusu kutoboka kwa gunia lako la amniotic, watafanya vipimo kudhibitisha.

Ikiwa umebakisha wiki tatu kujifungua, mkunga wako atangoja masaa machache kuona kama utaanza kushuhudia uchungu wa uzazi peke yako. Usipo, wana weza kuanzishia uchungu wa uzazi kwa kukudunga sindano. Kwa kawaida, wanawake wengi huingia kwa uchungu wa uzazi masaa kumi na mawili bila kusaidiwa.

Utafiti uliofanywa unadhibitisha kuwa watoto walio zaliwa kwa mama aliye anzishiwa uchungu wa uzazi bila kukawi wana nafasi za chini za kupata maambukizo, hawa hitaji utunzi mwingi katika kitengo cha dharura na wana achiliwa kwenda nyumbani bila kukawia ikilinganishwa na watoto ambao mama zao hawaku anzishiwa uchungu wa uzazi. Wasiliana na daktari anaye kusaidia kujifungua kuhusu jambo litakalo kufaa.

Kuvuja maji mapema

Mambo Ya Kutarajia Maji Yanapo Vuja Kabla Ya Kushuhudia Uchungu Wa UzaziMambo Ya Kutarajia Maji Yanapo Vuja Kabla Ya Kushuhudia Uchungu Wa Uzazi

Asilimia ndogo ya wanawake (3) hushuhudia kuvuja maji katika wiki ya 37 ya ujauzito wao PROM. Husababishwa na mambo haya:

  • Mama kuwa na uzani wa chini
  • Uvutaji sigara
  • Kupitia PROM katika ujauzito mwingine
  • Kuvuja damu katika mimba
  • Matatizo na kizazi chake katika mimba

Ikiwa uko angalau wiki 34 katika safari yako ya mimba, huenda daktari aka penda ujifungue ili kupunguza hatari za mtoto kupata maambukizi.

Ikiwa uko katika kati ya wiki ya 23 hadi ya 34 ya ujauzito, mara nyingi huwa vyema kukawia kujifungua ili mtoto wako awe na wakati tosha wa kukua. Huenda ukashauriwa kubaki hospitalini hadi ujifungue.

Kuna baadhi ya wanawake ambao huingia kwa uchungu wa uzazi kabla ya maji kuvuja. Katika kesi hii, daktari anaweza kuvujia maji.

Soma piaKupanga Kujifungua Kwa Mapema Huenda Kukahatadharisha Maisha Ya Mwanao

Written by

Risper Nyakio