Kuna magonjwa ya ujauzito kama kichefu chefu, maumivu ya mgongo na kuchoka yanayo fanya iwe vigumu kufuatilia lishe yenye afya, mazoezi na kubaki na shepu nzuri katika mimba. Walakini, manufaa ya ujauzito wenye afya yanapiku matatizo utakayopatana nayo. Kama vile kupunguza uzito, uchungu wa uzazi rahisi, mtoto mwenye afya na nishati katika safari yako ya mimba. Tazama yote unayostahili kujua kuhusu jinsi ya kuwa fit katika mimba.
Jinsi ya kuwa fit katika mimba

Inahitaji uwe na nidhamu ili uweze kuwa na afya na fit katika ujauzito. Baadhi ya wakati, unataka kubugia chokoleti na switi unapopaswa kuwa ukikula chakula chenye protini nyingi. Wakati mwingi unapotaka kufanya mazoezi, kama kutembea, unahisi uchovu ama kichefu chefu. Itasaidia kujikumbusha manufaa kwako na kwa mwanao. Tazama baadhi ya njia za kudumisha afya katika ujauzito.
- Jitenge na vyakula vyenye sukari na wanga nyingi
Vyakula vyenye wanga nyingi ni kama vile mikate na vyakula vya kuoka. Kuvitia mwilini hutumika kwa njia sawa na sukari mbichi. Mwili usipo choma sukari hizi zaidi, mwili huzibadilisha na kuzihifadhi kama ufuta kwenye mikono, matiti, mapaja na tumbo.
Maji husaidia kukuza placenta na kiowevu cha amniotic zote ambazo ni muhimu katika ukuaji wa mtoto. Mama mwenye mimba anashauriwa kuchukua angalau glasi kumi za maji kwa siku.
Wanawake wengi wenye mimba huteseka na kufanya mazoezi kufuatia uchovu na kichefu chefu. Walakini, mazoezi sio lazima yakuwe magumu. Hata kutembea kwa dakika chache, kufanya kazi za kinyumbani, kujichukulia chombo fulani badala ya kutumana ama hata kuogelea. Hata hivyo, kuna mazoezi ambayo mama mwenye mimba hapaswi kufanya kwani yatahatarisha maisha yake na ya mtoto.
Ujauzito huwa muda wenye mawazo mengi katika maisha ya mwanamke. Akili yako itakuwa na shaka kuhusu mambo yote ambayo huenda yakaenda mrama kabla ya kujifungua. Ni kawaida ila sio nzuri kwako. Tuliza akili yako ili uweze kulala na kupumzika vyema usiku.

Wanawake wengi hujitenga mbali na ufuta kwani wanadhani kuwa ufuta ndio unaowafanya waongeze kilo. Vyakula vyenye ufuta wenye afya kama parachichi na mafuta ya nazi ni muhimu. Chagua vyakula bora kama nyama laini, mayai na bidhaa za maziwa nzima. Kula vyakula vya protini husaidia kupunguza kuhisi njaa wakati wote.
Kufuata tuliyoangazia kutakusaidia kuwa fit katika ujauzito wako. Mtoto wako atakua vyema na uchungu wa uzazi utakua rahisi zaidi.
Soma Pia: Vyanzo Vikuu Vya Kuvuja Damu Katika Ujauzito