Kwa kawaida kina mama hujulikana kuwa wenye mapenzi na wanyenyekevu. Ilihali hili sio kweli kwa kila mama. Na pia hizi sio tosha kumwelezea mama bora. Hivyo basi ni mambo gani humthibitisha kuwa mama bora?
Kuwa Mama Bora

Kwa sababu ya nafasi yake katika Jamii kuna yale mambo ambayo hutarajiwa kutoka kwa mama. Haya huwa tofauti na ya baba kwa upana sana. Mama ndiye huwa na uwezo wa kubeba mtoto kabla kufika duniani hivyo kumpa nafasi bora kama mlezi. Hivyo kama mlezi kuna mambo aliyoubika nayo ili kuwezana na hili jukumu. Haya ni kama vile:
Mama amepewa uwezo wa kulinda watoto. Mapenzi ya mama huwa ya kitofauti sana na ya wale wengine. Kuweza kuwalinda watoto kutokana na hatari yoyote na pia mambo yasiyofaa kama vile njaa na pia baridi. Hili ni jambo lisilokuwa wazi sana kwa kina baba. Kuweza kuwalinda watoto ni jambo ambalo humtofautisha mama kwa umbali.

Kuwa mama lazima uwe na roho yenye upendo. Huu si upendo wa muda tu ama wakati kila kitu ki shwari mbali tu kila wakati. Watoto hawatakuwa kwa mienendo mizuri mara nyingi. Hivyo kuwa mama bora ni kuhakikisha kuwa uko upande wa watoto kila wakati. Na pia kuwaeleza watoto wako kuwa unawapenda.
Kuwa mama bora ni kuhakikisha kuwa unaangalia hasira yako. Watoto kila siku ama wakati watafanya mambo ya kukasirisha. Watagombana ama kuchapana na kama mama ni mwepesi kila wakati hataweza kuwarekebisha watoto. Kuna kurekebisha watoto kwa hasira ambako huwa hakuna faida yoyote na kuna kule ambako huleta mabadiliko yanayofaa.
Watoto watundu ni aibu kwa wazazi. Mama huwa na jukumu la kuhakiksha kuwa watoto wanakua kwa njia zinazozingatia heshima kwa Jamii. Sio kila mama ambaye huchukua hili jukumu kwa mikono miwili. Hivyo kuwa mama bora ni kuhakikisha kuwa watoto wana nidhamu. Mazoea ya wengi kutowaadhibu watoto husababisha tabia potovu kwa watoto.
Kwa dhana za wengi mama huwa hana dosari yoyote. Kwani huonekana wadhaifu na wakati mwingine wanyonge ila la. Kina mama pia wana hulka ya kuwa na tabia zisizo njema na hivyo kuvutiwa hasira kutoka kwa Jamii. Kuwa mama bora ni mchakato wa mambo mengi na ukweli ni kuwa haya mambo hayana kikomo.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Je, Ni Wakati Upi Ulio Bora Kwa Mama Kupima Mimba?