Sababu Kwa Nini Unapaswa Kuwa Na Muda Zaidi Na Watoto Wako

Sababu Kwa Nini Unapaswa Kuwa Na Muda Zaidi Na Watoto Wako

Zawadi bora sana unaweza mzawadi mtu yeyote, ikiwemo familia yako, ni wakati wako. Baadhi ya wakati, wazazi hulazimika kuwa na wakati mdogo sana na familia yao kufuatia matatizo ya kikazi na majukumu mengine. Ila, ulifahamu kuwa kuna faida nyingi sana za kuwa na wakati wa watoto wako? Kuna faida nyingi sana kwako na kwa mtoto wako. Tazama baadhi ya sababu kwa nini unapaswa kuwa na wakati na mtoto wako.

kuwa na wakati wa watoto wako

Tuna angazia sababu kwa nini kila mzazi anapaswa kutazamia kuwa na wakati zaidi na watoto wake na jinsi ya kuhakikisha kuwa anatimiza lengo hili hata kama ana wakati mdogo sana.

Kwa Nini Unapaswa Kuwa Na Wakati Mwingi Zaidi Na Watoto Wako?

Bila shaka, kwa sababu ya sababu nyingi sana! Muda bora ni muhimu sana kwa kila familia. Hizi ndizo sababu kwanini unapaswa kuhakikisha kuwa uko na watoto wako kwa muda mrefu:

1. Mtoto wako atasoma jinsi ya kutengeneza marafiki

Kuwa na wakati na mtoto wako kunaweza msaidia kukuza uwezo wa kuingiliana. Watoto watafurahia kuwa na wewe na pia kusoma mambo mengi ambayo wata tumia wanapo tengeneza marafiki wapya. Na cha zaidi, watafahamu jinsi ya kutengeneza wakati ili wawe na marafiki wao.

2. Kuna fungua mazungumzo ya njia mbili kati ya wazazi na wanao

Mojawapo ya faida za kuwa na wakati na mtoto wako ni kujenga imani kati yako nao. Watoto watajua jinsi ya kukuongelesha kuhusu kitu chochote. Mazungumzo wazi yana jukumu katika usalama wa mwanao. Iwapo ungependa watoto wako waje kwako kwanza wanapo pata tatizo ama shida yoyote, unapaswa kuhakikisha kuwa unatumia muda zaidi nao.

3. Ina saidia familia yako kutangamana zaidi

Utangamano wa familia yako utakuwa wa karibu zaidi unapo anza kujaribu kufurahikia faida za kuwa na wakati na mtoto wako. Kuja pamoja kama familia na kujua vitu ambavyo mwanafamilia mwingine anapenda, vyakula na hata kupiga ngumzo kuna saidia familia kuwa na utangamano wa karibu zaidi.

4. Inaweza boresha kujiamini kwa mtoto wako

When your child sees how eager you are to spend time with them, they will appreciate how much you value them. This feeling of acceptance and love is great for their self-esteem. Mtoto wako anapo ona kuwa una haja ya kuwa na wakati naye, atahisi kupendwa. Hisia hizi za kukubalika na mapenzi ni muhimu katika kujiamini kwake.

Masomo yame dhibitisha kuwa watoto wanao toka kwa familia zilizo na utangamano wa karibu huwa wana jiamini zaidi ikilinganishwa na watoto wanao toka kwa familia zisizo na utangamano.

5. Sababu moja nzuri ya kuwa na wakati wa watoto wakoni kuwa inakusaidia kuwa elewa zaidi

Watoto wanaweza ugua kutokana na kukwazwa kiakili na matatizo mengine ya afya ya akili, na wakati mwingi, matatizo haya huenda yakakosa kujulikana ikiwa watu wazima walioko kwenye maisha ya mtoto huyu hawako makini. Pia, watoto wanao dhalilishwa shuleni kwa mara nyingi hawana ujasiri wa kuongea na kuwajulisha wazazi wao kinacho endelea. Pia kuna swala la kudhalilishwa kimapenzi ama kifizikia na huenda kukatendeka bila ya mzazi kujua.

Habari njema ni kuwa ukiwa na wakati na watoto wako, itakuwa rahisi zaidi kugundua iwapo kuna jambo lisilo sawa nao.

kuwa na wakati wa watoto wako

6. Kuna himiza tabia chanya

Watoto wenye umri zaidi wako katika hatari ya kupata shinikizo la wana rika na kujihusisha katika tabia hasi kama vile uvutaji wa sigara, kulewa na kutumia mihadarati. Ni vigumu zaidi kwa watoto wanao toka kwa familia zilizo na umoja na zenye wazazi wanao wapenda na kuwalinda kupotoka kwa njia zinazo faa.

Pia, kula chakula na watoto wako mara kwa mara na kuwafunza nidhamu ya kula.

7. Watoto wako watakuwa wanajamii wenye tabia njema

Mojawapo ya faida za kuwa na wakati tosha na mtoto wako ni kuwa inamkubalisha mtoto kukua na ujasiri na mienendo miema. Iwapo una taka kuwalea watoto watakao kufanya uhisi fahari popote unapo enda, unapaswa kuanza kutumia wakati wako na watoto wako.

8. Watoto wanao tumia wakati zaidi na wazazi wao wana fuzu katika masomo yao

Iwapo wakati wote uko na watoto wako na kuwasaidia na kazi zao za ziada na kujadili wanavyo endelea shuleni, itakuwa rahisi kutambua sehemu ambazo mtoto wao ana tatizika kimasomo. Ukijua sehemu hizo, kuna uwezekano wa kuwasaidia kufanya kazi ili kuwa bora katika sehemu hizo.

Jinsi ya kutumia wakati na mtoto wako

  • Punguza wakati wa kutazama televisheni kwa kuzima televisheni na simu
  • Tafuta njia ya kuhusisha watoto wako katika shughuli zako za kila siku kama vile kuosha nguo na vyom
  • Mnaweza kuwa na usiku wa familia angalau mara moja kwa wiki
  • Panga kuwa pamoja wikendi nyingi
  • Wasomee watoto wako vitabu kabla walale
  • Panga kuwa nao wakati wa likizo za shule: unapaswa kupunguza nambari ya wakati wanao tumia na jamii wengine.

Kutumia wakati pamoja kuna faida kwa watoto na wazazi. Faida zilizo orodheshwa kwenye makala haya zita hakikisha mna utangamano bora zaidi wa kifamilia; ila zitasaidia kukuza watoto walio na hisia bora zaidi.

Kumbukumbu: Goodtherapy.org

NHS

Telegraph.co.uk

Soma pia: Parenting For Dummies: Useful Tips For The Accidental Parent

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio