Maarifa kuhusu fedha ni muhimu ili kuwa na maisha yenye mafanikio. Fedha ni sekta muhimu na inayostahili kupatiwa kipao mbele hata masomoni. Cha kusikitisha ni kuwa, kama jamii, hatuzungumzi vya kutosha kuhusu fedha. Hata kwa watu walio na uhusiano wa karibu, hawana mazungumzo haya. Darasa za maarifa kuhusu fedha zinapaswa kuanza mapema maishani. Katika makala haya, tuna angazia jinsi ya kuanza kuwafunza watoto mapema kuhusu fedha.
Jinsi ya kuwafunza watoto kuhusu fedha
- Anzia kuwaelimisha kuhusu pesa

Anza kwa kuwapatia watoto shillingi 5, 10 ama 20. Wafunze dhamani ya pesa na uwahimize kuzihifadhi kwenye kijibenki cha watoto almaarufu kama piggy bank. Katika hatua hii, tumia kijibenki kilicho na rangi wazi inayo wawezesha kuona ndani ili waone kiwango cha pesa kinavyo ongezeka. Unaweza kuwa na vijibenki viwili, cha kuhifadhi na cha kutumia. Cha kutumia ni cha kufanya manunuzi madogo na cha kuhifadhi ni cha kununua manunuzi makubwa.

Watoto hawafuati maneno ya wazazi wao, ila wanafanya wanacho waona wazazi wao wakifanya. Mweleze unachofanya unapo andika cheki na kulipia vitu. Epuka kufanya ununuzi ambao haujaupangia, na uwaambie watoto unangoja baada ya siku moja kuona iwapo kwa kweli uungependa kufanya ununuzi huo. Watoto husoma mengi kwa kuzingatia na kufuata wanacho waona wazazi wao wakifanya.
- Mhusishe mtoto wako katika uamuzi wa kifedha
Mnapo enda kufanya ununuzi, mwambie kwanini unapenda kununua vitu kutoka kwa kampuni hii badala ya ile. Mweleze kuhusu kuangalia bei ya bidhaa anaponunua na umuhimu wa kununua vitu vingi kwa pamoja ikilinganishwa na kununua kitu kimoja kimoja. Mweleze kwa nini ni vyema kununua vitu unavyo vihitaji peke yake.
- Mfunze mwanao jinsi ya kufanya bajeti

Anapokwambia kuwa angependa umnunulie kitu fulani, mfunze jinsi ya kufanya bajeti kabla ya kufanya ununuzi. Pia, mpe kazi ndogo kama vile kufanya bajeti ya sherehe zake kama vile siku ya kuzaliwa kwake. Kwa kusisitiza hivi anapokuwa mdogo, atakua na maarifa haya hata anapokuwa uzimani wake.
Kutosheleka huanzia moyoni. Wafunze kuwa, sio lazima wawe na mavazi na vidoli vipya kila mara. Na umuhimu wa kuvitumia vitu kwa muda kabla ya kununua vingine. Wanunulie vidoli mara kwa mara wanapofanya kitu cha kupongezwa na katika siku za kusherehekea kuzaliwa kwao.
Chanzo: Balance
Soma Pia: Njia Bora Zaidi Za Kumwadhibu Mtoto Kwa Kuiba Pesa