Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Jinsi Wazazi Wanavyo Weza Kuwalinda Watoto Wao Katika Kipindi Cha Lockdown

3 min read
Jinsi Wazazi Wanavyo Weza Kuwalinda Watoto Wao Katika Kipindi Cha LockdownJinsi Wazazi Wanavyo Weza Kuwalinda Watoto Wao Katika Kipindi Cha Lockdown

Kuna mengi ambayo yamekuwa yakitendeka katika kipindi hiki cha lockdown na wazazi wanapaswa kuwalinda watoto wao wakati wote.

Kumekuwa na mambo mengi yaliyo tendeka na yanayo endelea kutendeka hasa kwa watoto wa shule walio nyumbani katika kipindi hiki cha karantini iliyoko katika sehemu nyingi za dunia. Ni jukumu la wazazi walio na watoto katika kipindi hiki kuwachunga na kuhakikisha kuwa hakuna jambo mbaya linalo wapata. Je, kwanini wazazi wanapaswa kuwalinda watoto wao katika lockdown?

kuwalinda watoto katika lockdown

Sababu kwa nini wazazi wanapaswa kuwalinda watoto wao katika kipindi hiki cha lockdown

  1. Maradhi ya Covid-19

Mojawapo ya sababu kuu kwa nini wazazi wanapaswa kuwalinda watoto wao katika kipindi hiki cha karantini ni ile wasiambukizwe maradhi ya Covid-19 ambayo imesababisha kudhoofika kwa afya kwa watu wengi na hata vifo. Maradhi haya yana ambukizwa kupitia hewa na mtu aliye mgonjwa akiwa karibia watoto wako iwapo hawaja jikinga ipasavyo, wata  ambukizwa maradhi haya. Ni jukumu la kila mzazi pia kuhakikisha kuwa watoto wake wanapata lishe bora yenye afya ili mfumo wao wa kinga uwe na nguvu wakati wote na uwezo wa kupigana dhidi ya magonjwa.

2. Kupotoka kwa nidhamu

Baadhi ya mambo ambayo yame shuhudiwa katika kipindi hiki cha lockdown tangu kilipo anza mwezi wa Machi ni ongezeko la mambo hasi kama vile wizi, utumiaji wa madawa ya kulevya na vinginevyo. Baadhi ya visa vya wizi vilivyo ripotiwa vilifanywa na watoto wa shule hasa wa sekondari. Mzazi asipo wachunga watoto wake, ni rahisi sana kupotoka njia hasa wanapo patana na kuandamana na vijana wa rika lao walio mea pembe na hawajali kuhusu maisha yao. Njia bora zaidi kwa mzazi kuhakikisha kuwa kijana wake hatangamani na watu wabaya ni:

kuwalinda watoto katika lockdown

  • Kuwahimiza kucheza na marafiki zao wakiwa nyumbani na unaweza wachunga
  • Kuhakikisha kuwa anawafahamu marafiki wa watoto wake
  • Kuwa wazi na watoto wake na kuanzisha mijadala kuhusu marafiki wazuri na wabaya
  • Kuwaruhusu watoto wake kuwaleta marafiki zao nyumbani ili uweze kuona wanacho fanya na utambue iwapo watamsaidia mtoto wako ama wata fanya aanze mambo mabaya
  • Kuwashauri watoto kuhusu masomo, maisha na maswala ya kijumla
  • Kuhakikisha kuwa watoto hawana wakati mwingi wa ziada, hakikisha kuwa wakati wote wana mambo ya kufanya wakiwa nyumbani, kama vile kusafisha nyumba na vyombo

3. Kujiingiza katika kufanya ngono

Katika kipindi cha miezi chini ya mitano, idadi kubwa ya watoto wa shule wamepata mimba. Huku kuna maana kuwa watoto hawa hawatarudi shuleni shule zinapo funguliwa kwani watakuwa wana wachunga watoto wao. Ni jambo la kuhuzunisha kuwa watoto wa shule ya msingi na sekondari wana jihusisha katika ngono wangali wachanga. Hata kama hatungependa kuwalaumu wazazi kwa jambo hili, wazazi wana shauriwa kuongea kwa wazi na watoto wao kuhusu ngono na athari zake.

facebook privacy checkup

Ni jukumu la wazazi kuwalinda watoto wao kutokana na watu ambao huenda waka wadhalilisha kingono, japo wakubwa ama hata wa rika lao. Katika tamaduni na jinsi tulivyo kua, sio wazazi wengi ambao hukua na mjadala huu na watoto wao, ila usipo wafunza wataenda kufunzwa na wanarika wao wasio kuwa na maarifa tosha. Ni vyema kwa wazazi kufahamu kuwa usalama wa watoto wao uko mikononi mwao na wasipo walinda mambo mabaya yatawakumba. Waeleze kuwa wanapaswa kungoja hadi wanapo funga ndoa kufanya ngono, na iwapo wanajipata katika hali ambapo lazima wafanye ngono kama vile kudhalilishwa ama kushikwa kwa nguvu, wanapaswa kutumia kondumu ili wajilinde kutokana na maambukizi ya kingono ama kupata mimba.

Wanajamii wanapaswa kushikana mikono ili kuwalinda watoto katika lockdown na kuhakikisha kuwa wako salama na wana maarifa yote kuhusu somo la ngono.

Soma pia: Jinsi Ya Kutunza Watu Walio Na Covid-19 Nyumbani Bila Kuambukizwa Maradhi Haya

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Parenting
  • /
  • Jinsi Wazazi Wanavyo Weza Kuwalinda Watoto Wao Katika Kipindi Cha Lockdown
Share:
  • Mitindo 10 Ya Kufanya Mapenzi Katika Kipindi Hiki Cha Lockdown Na Mwenzio

    Mitindo 10 Ya Kufanya Mapenzi Katika Kipindi Hiki Cha Lockdown Na Mwenzio

  • Je, Kuna Tatizo Katika Ulezi wa Kisasa Nchini Kenya?

    Je, Kuna Tatizo Katika Ulezi wa Kisasa Nchini Kenya?

  • Covid-19: Jinsi Ya Kuishi Iwapo Kuna Lockdown Ya Homa Ya Korona Kenya

    Covid-19: Jinsi Ya Kuishi Iwapo Kuna Lockdown Ya Homa Ya Korona Kenya

  • Umuhimu Wa Kuwa Na Watoto Wako Kwa Muda Mrefu

    Umuhimu Wa Kuwa Na Watoto Wako Kwa Muda Mrefu

  • Mitindo 10 Ya Kufanya Mapenzi Katika Kipindi Hiki Cha Lockdown Na Mwenzio

    Mitindo 10 Ya Kufanya Mapenzi Katika Kipindi Hiki Cha Lockdown Na Mwenzio

  • Je, Kuna Tatizo Katika Ulezi wa Kisasa Nchini Kenya?

    Je, Kuna Tatizo Katika Ulezi wa Kisasa Nchini Kenya?

  • Covid-19: Jinsi Ya Kuishi Iwapo Kuna Lockdown Ya Homa Ya Korona Kenya

    Covid-19: Jinsi Ya Kuishi Iwapo Kuna Lockdown Ya Homa Ya Korona Kenya

  • Umuhimu Wa Kuwa Na Watoto Wako Kwa Muda Mrefu

    Umuhimu Wa Kuwa Na Watoto Wako Kwa Muda Mrefu

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2022 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it