Umuhimu Wa Kuwa Na Watoto Wako Kwa Muda Mrefu

Umuhimu Wa Kuwa Na Watoto Wako Kwa Muda Mrefu

Utafiti umedhibitisha kuwa wazazi wanao kuwa na wakati mwingi na watoto wao huwa saidia watoto wao kupasi shuleni na pia kuwa watu wakarimu.

Mambo yame badilika sana ikilinganishwa na siku za hapo awali. Huenda ikawa vigumu kupata wakati tosha wa kuwa na familia yako hasa watoto na ni muhimu sana. Kuwapa watoto wakati tosha ni mojawapo ya vitu vikuu zaidi ambavyo tunaweza wapatia. Haijalishi kazi unayo fanya ama hata uwe unasoma ungali mzazi, ni vyema kuhakikisha kuwa kila wiki unapata wakati tosha wa kuwa na watoto wako. Hizi ndizo sababu kwa nini unapaswa kuwa na watoto wako kwa muda tosha.

kuwapa watoto wakati tosha

Umuhimu wa kuwapa watoto wako wakati tosha

  • Inasaidia kukuza kujiamini kwao

Watoto wanao kuwa na wakati tosha na wazazi wao na kufanya mazoezi pamoja husaidia kukuza uwezo wao wa kujiamini. Watoto wanapo hisi kuwa wana thaminiwa na wazazi wao, wana kuwa na hisia chanya kujihusu. Matendo ama mazoezi ya kifamilia sio lazima yawe ya bei ghali, kitu cha maana ni kuwa pamoja. Mnaweza tembelea buga la wanyama.

  • Kukuza utangamano wa familia

Familia zinazo kuwa na wakati tosha pamoja huwa na utangamano wa karibu na usio rahisi kuvunja. Utafiti umedhihirisha kuwa familia zinazo fanya matendo ya vikundi huwa na utangamano wa karibu na pia kuaminiana katika kufanya vitu kama familia. Fanyeni vitu mnavyo furahia kama familia kama vile kusoma vitabu, mazoezi ya fizikia, kutizama sinema na vitu vingine.

kuwapa watoto wakati tosha

  • Ina kuza tabia chanya kwa watoto

Watoto na watu wazima wanao kuwa na wazazi wao kwa muda mrefu ni vigumu kuhusika katika tabia halifu. Kulingana na utafiti uliofanyika na National Center on Addiction and Substance Abuse, watoto walio jiingiza katika uraibu wa kutumia madawa ya kulevya huwa wa familia ambazo hawana wakati na wazazi wao na hawa hisi kana kwamba wako katika familia hiyo.

  • Ina himiza mazungumzo

Unapokuwa na watoto wako kwa muda mrefu, una himiza mazingira ya kuwa na mazungumzo wazi kuhusu mijadala yoyote. Kuwa na mazungumzo wazi na watoto kuna wasaidia kuhisi kuwa wana weza kwambia kitu chochote kinacho endelea maishani mwao. Kuuliza swali kama jinsi siku yao ilivyo kuwa ina tofauti kubwa.

Umuhimu Wa Kuwa Na Watoto Wako Kwa Muda Mrefu

  • Watoto wana pasi shuleni

Kufanya mazoezi kama kusoma na watoto wako hasa wanapo kuwa wangali wachanga kutawasaidia shuleni. Mnapo fanya kazi ya ziada pamoja, huenda akapasi shuleni.

  • Watoto wako watakuwa marafiki wako

Watoto hufuata matendo yako sio maneno yako. Kuwa mwangalifu na tabia zako unapo kuwa karibu na watoto wako kwani watafuata unacho fanya. Kuwa mfano wa kuigwa na watafuata tabia zako hata wanapo wasiliana na watu wengine. Mambo madogo kama kucheza michezo nao kutasaidia kuwafunza kuwa wakaribu na kuwasaidia watu ambao hawana.

Wakati wa familia ni muhimu sana kwani unapata kuwaelewa watoto wako zaidi na pia wanajua kuwa wanaweza kuamini na kukwambia wanapokuwa wakitatizwa na shida yoyote ile.

Written by

Risper Nyakio