Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Baba Kuwasomea Watoto Hadithi Za Wakati Wa Kulala: Kwa Nini Ni Bora Kwa Ukuaji Wa Mtoto Wako!

2 min read
Baba Kuwasomea Watoto Hadithi Za Wakati Wa Kulala: Kwa Nini Ni Bora Kwa Ukuaji Wa Mtoto Wako!Baba Kuwasomea Watoto Hadithi Za Wakati Wa Kulala: Kwa Nini Ni Bora Kwa Ukuaji Wa Mtoto Wako!

Utafiti mpya umevumbua kuwa watoto hufaidika zaidi kutoka kwa baba zao kuwasomea hadithi za wakati wa kulala ikilinganishwa na mama.

Unajua picha ilivyo: watoto hukoga, kuvalia mavazi yao ya kulala kisha kuingia kitandani, huku wakingoja mama awasomee hadithi ya wakati wa kulala. Mama, huenda ukataka kumpa baba kazi ya kuwasomea watoto hadithi za wakati wa kulala baada ya kusoma makala haya!

Baba wako bora zaidi katika kuwasomea watoto hadithi za wakati wa kulala

Baba Kuwasomea Watoto Hadithi Za Wakati Wa Kulala: Kwa Nini Ni Bora Kwa Ukuaji Wa Mtoto Wako!

Utafiti mpya ulio ongozwa na daktari Elisabeth Duursma kutoka Chuo Kikuu cha Harvard huko Umarekani umevumbua kuwa watoto hufaidika zaidi kutoka kwa baba zao kuwasomea hadithi za wakati wa kulala ikilinganishwa na mama.

Kulingana na matokeo ya somo hilo, "mazungumzo bunifu" hutendeka na lugha zaidi kukua kwa sababu njia ya kufikiria ina patiwa mwito wa kushindana baba anapo wahadithia.

Wasichana wali nufaika zaidi wanapo somewa na mwanamme.

Daktari Duursma alisema, "Manufaa ni mengi- hasa wazazi wa kiume wanapo anza kuwasomea watoto walio katika umri wa miaka miwili. Kusoma kuna onekana kama tendo la kike na watoto wanaonekana kuwa makini zaidi baba zao wanapo wasomea - ni spesheli."

Ni nini baba hufanya tofauti?

the benefits of paternity leave

Ripoti iliyo tolewa kwenye Telegraph kuhusu utafiti huu ili gusia kuwa wanaume na wanawake hufanya tendo la kusoma tofauti.

Wanawake huuliza maswali wazi kama vile, "Unaona tufaha ngapi?"

Wakati ambapo wanaume hupendelea kuuliza maswali fiche yanayo fanya ubunifu wa watoto kutumika na uwezo wao wa lugha kuhusishwa na kukua.

Daktari Duursma anasema, "Wazazi wa kiume wana nafasi zaidi za kusema kitu kama, "Angalia, ngazi. Unakumbuka wakati ambapo nilikuwa na ngazi hiyo kwenye gari yangu?"

Ana eleza kuwa jambo hili ni bora katika ukuaji na maendeleo ya lugha ya mtoto kwa sababu ina tia mwito wa kushindana kwa uwezo wao wa kiakili. Kwa lugha rahisi, watoto wanahitaji kutumia akili zao zaidi kujibu swali kama hilo.

Kwa hivyo wazazi, jibu letu ndilo hilo. Kwa sasa, chukua usukani wa kuwa somea watoto wako hadithi za wakati wa kulala. Wewe ndiye afisaa. Chukua kitabu hicho cha hadithi kisha uanze kazi!

Soma Pia: Sababu Kwa Nini Unahitaji Utaratibu Wa Kulala Yako Na Watoto Wako

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Parenting
  • /
  • Baba Kuwasomea Watoto Hadithi Za Wakati Wa Kulala: Kwa Nini Ni Bora Kwa Ukuaji Wa Mtoto Wako!
Share:
  • Sababu Kwa Nini Unahitaji Utaratibu Wa Kulala Yako Na Watoto Wako

    Sababu Kwa Nini Unahitaji Utaratibu Wa Kulala Yako Na Watoto Wako

  • Kuwa Makini Kuona Mabadiliko Haya Katika Mtindo Wa Kulala Wa Mtoto Wako

    Kuwa Makini Kuona Mabadiliko Haya Katika Mtindo Wa Kulala Wa Mtoto Wako

  • Utafiti Wa Kisayansi Waonyesha Faida Za Kiafya Za Kulala Mchana

    Utafiti Wa Kisayansi Waonyesha Faida Za Kiafya Za Kulala Mchana

  • Sababu Kwa Nini Unapaswa Kuwa Na Muda Zaidi Na Watoto Wako

    Sababu Kwa Nini Unapaswa Kuwa Na Muda Zaidi Na Watoto Wako

  • Sababu Kwa Nini Unahitaji Utaratibu Wa Kulala Yako Na Watoto Wako

    Sababu Kwa Nini Unahitaji Utaratibu Wa Kulala Yako Na Watoto Wako

  • Kuwa Makini Kuona Mabadiliko Haya Katika Mtindo Wa Kulala Wa Mtoto Wako

    Kuwa Makini Kuona Mabadiliko Haya Katika Mtindo Wa Kulala Wa Mtoto Wako

  • Utafiti Wa Kisayansi Waonyesha Faida Za Kiafya Za Kulala Mchana

    Utafiti Wa Kisayansi Waonyesha Faida Za Kiafya Za Kulala Mchana

  • Sababu Kwa Nini Unapaswa Kuwa Na Muda Zaidi Na Watoto Wako

    Sababu Kwa Nini Unapaswa Kuwa Na Muda Zaidi Na Watoto Wako

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it