Hakuna wakati sawa wa kuwatenganisha watoto wako kiumri, lakini kuna vitu ambavyo wazazi wanapaswa kuangazia wanapojitayarisha kupata mimba ingine. Unapoamua kuwa ungependa kuwa na watoto zaidi ya mmoja, kufanya uamuzi wa umri wa kuwatenganisha watoto wako ni jambo kubwa. Kuna hasara na faida za kuwatenganisha watoto kwa muda mrefu ama mfupi.
Watoto walioachana na mwaka mmoja

Faida
- Watoto wana utangamano wa karibu na kuwa marafiki wa dhati
- Hakuna mtoto atakaye tarajia kuwa na wakati zaidi na mzazi
- Mzazi anapata wakati zaidi wa kuwa na watoto wake
Hasara
- Ni vigumu kwa mwili kustahimili kubeba mimba punde tu baada ya kujifungua. Mwili haujapata wakati tosha wa kupona. Hasa kama mama alipata mtoto wa kwanza kupitia upasuaji wa c-section
- Ni kazi nyingi. Usiku bila kulala, kubadilisha nepi, uchovu, na pia kunyonyesha
- Mama ana kazi nyingi ya kuwatunza watoto wawili chini ya miaka miwili
- Mama ana gharama zaidi ya kununua mavazi ya kila mtoto
Umri wa miaka miwili kati ya watoto

Faida
- Mwili wa mama umepona na ako tayari kubeba mimba ingine
- Kupata mtoto baada ya miaka miwili kunapunguza hatari ya kupata matatizo yanayo husiana na ujauzito. Kuna punguza hatari ya mtoto wa pili kuzaliwa na uzani wa chini
- Mama ana maarifa tosha ya kumlea na kumtunza mtoto
Hasara
- Vita kati ya watoto vitakuwa zaidi ikilinganishwa na watoto walio na umri wa miaka michache kati yao
- Watoto huenda wakachukiana, kwani wanaona wazazi wao wanapenda mwingine zaidi
Umri wa miaka mitatu kati ya watoto

Faida
- Uzazi wa kujifungua utakuwa salama
- Ujauzito utakuwa na hatari ya chini zaidi kwa mama na mtoto
- Ni rahisi zaidi kwa mama kubeba mimba tena. Katika wakati huu, mwili wake umepona itoshavyo na ana nishati tosha ya kubeba mimba tena
Hasara
- Una mambo mengi ya kufanya. Kifungua mimba bado anahitaji kusaidiwa kufanya vitu, na mara nyingi mzazi atakuwa akimchunga mtoto mdogo
- Huenda mtoto mkubwa akamuonea mdogo wivu na kuona kana kwamba wazazi wake hawampendi tena. Mbali wanapenda mtoto mdogo
Umri zaidi ya miaka mitatu, mama huenda akawa katika hatari ya kupata matatizo ya kujifungua, ikilinganishwa na wanawake wanaojifungua tena kwa muda chini ya miaka minne. Watoto watakuwa na tofauti kubwa na huenda wasiwe na uhusiano wa karibu kwani wana miaka tofauti.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Madhara Ya Kutoa Mimba Kwa Kutumia Vidonge Kwa Afya Ya Mama!