Vifo vya ghafla kati ya watoto walio zaliwa sio muda mrefu huwa maarufu sana. Ni vyema kukumbuka kuwa vifo hivi sio lawama kwa mzazi yeyote, mbali, ajali hutendeka kila mara na wakati mwingi, hatuna nguvu za kudhibiti kilicho tukia. Na kwa sababu hii, ni muhimu sana kuzingatia usalama wa mtoto anapo lala. Kwa kawaida, mama huwa amechoka na kuishiwa na nguvu anapo toka chumba cha kujifungua. Muda mrefu katika uchungu wa uzazi kisha kujifungua ambako ni safari ndefu, itamfanya mama awe amechoka sana baada ya kumleta mtoto duniani.
Vidokezo Vya Kuzingatia Usalama Wa Mtoto Anapo Lala

Kwa sababu hii, ni vyema kuhakikisha kuwa mama aliye jifungua tu hatakuwa chumbani na mtoto wake peke yake. Huenda akasinzia na kumuacha mtoto peke yake bila mtu yeyote wa kumchunga. Hakikisha kuwa una msaidizi chumbani hicho baada ya kujifungua. Mama anahitaji muda mfupi wa kupumzika kabla ya kuanza kushuhudia usiku mrefu bila kupata usingizi wa kutosha huku akimnyonyesha mtoto.
Kitanda cha mtoto kinapaswa kuwa mahali salama pa mtoto wako kulala bila usumbufu wowote. Hivi ni vitu unavyo paswa kuangazia.
- Hakikisha kuwa wakati wote, mtoto wako analala kwa mgongo ili kuepuka hatari ya kifo cha ghafla cha watoto.
- Hakikisha kuwa kitanda chake hakija legea. Epuka kuweka madoido na vitu zaidi kwenye kitanda chake kama blanketi laini za kujifunikia unapo safiri.

- Matandiko inapaswa kutoshea kwenye godoro
- Godoro linapaswa kutoshea vyema kwenye kitanda bila kuwacha nafasi yoyote kati ya mwisho wa kitanda na mwisho wa godoro upande wa chini na wa juu
- Usiongeze mito, vidoli ama blanketi zaidi karibu na uso wa mtoto wako
Mbali na kitanda cha mtoto, chumba chake kinapaswa kuwa salama na kutengenezwa kwa umakini kwa njia ambayo hakuna kitu chochote ambacho kinaweza kumwumiza mtoto. Ukuta na sakafu zinapaswa kuwa laini ili mtoto asiumie anapo anguka akitembea.
Ikiwa utafanya uamuzi wa kuweka kioo kwenye chumba chake, hakikisha kuwa kingo zake haziwezi mkata mtoto anapo zigusa.
Soma Pia: Mama Aliye Choka Amlalia Mtoto Kwa Bahati Mbaya Na Kusababisha Kifo Chake