Kuna vifaa vingi vya kuzuia kupata mimba. Njia za uzazi wa mpango zimezidi, ila zingine huwa na nafasi za juu za kulinda dhidi ya kupata mimba ikilinganishwa na zingine. Kabla ya kutumia njia yoyote ya uzazi wa mpango, wanandoa wanapaswa kuwasiliana na mtaalum wa afya. Atafanya vipimo na kubaini njia ya uzazi wa mpango iliyo bora kwa kila mmoja.
Mbinu za kuzuia kupata mimba
1. Mbinu za kudumu
Njia ya uzazi wa mpango ya daima iliyo na ufanisi zaidi ni kufunga mirija ya ovari kwa kizungu tubal ligation kwa wanawake ama vasectomy kwa waume. Mirija ya ovari inapofungwa, inazuia manii kupatana na yai lililokomaa. Kwa wanaume, mirija inayobeba mbegu za kiume hukatwa na kufungwa ili mbegu zisipite kwenye shahawa. Baada ya utaratibu huu kufanyika, mwanamme hana shaka ya kumpa mwanamke mimba.
Mbinu zinazoweza kugeuzwa
Iwapo wanandoa hawako tayari kufanyiwa utaratibu wa kupanga uzazi wa kudumu, wanaweza kutumia mbinu za kupanga uzazi zinazoweza kugeuzwa na kuwawezesha kupata mimba wakiwa tayari. Mbinu hizi huwa za homoni ya progestin inayozuia manii kuingia kwenye kizazi na pia inasimamisha kupevuliwa kwa yai. Mbinu hizi ni kama vile:

2. IUD: Kifaa cha umbo la T huingizwa kwenye uterasi na kuzuia manii kuingia. Mbinu hii hudumu kwa kipindi cha kati ya miaka mitatu hadi kumi.
3. Implants ama vipandikizi: Kifaa kidogo huwekwa chini ya mkono na hudumu kwa miaka mitatu.
4. Mipira ya kondomu

Mipira ya kondomu inapovaliwa ipasavyo hulinda dhidi ya kupata ujauzito na magonjwa ya zinaa. Ili kuwa na ufanisi, inapaswa kuvaliwa vizuri, kutumia saizi inayotosha, kutotumiwa tena na kutumiwa kabla ya kuharibika kwake.
5. Tembe za uzazi wa mpango

Tembe za kupanga uzazi huwa na homoni za estrogen na progesterone zinazofanya kizazi kutoa uchafu ukeni mnene unaozuia manii kupita kwenye kizazi. Ili kufanya kazi vyema, tembe hizi zinapaswa kuchukuliwa wakati fulani kila siku.
Njia zaidi za kupanga uzazi

Sindano. Huwa na homoni ya progestin, hudungwa kwenye mkono na humlinda mwanamke dhidi ya kupata mimba kwa kipindi cha miezi mitatu.
Ring ama mpira wa wanawake.
Tembe za dharura ama emergency pills. Zinapaswa kuchukuliwa ndani ya masaa 72 baada ya kufanya mapenzi bila kinga.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Wakati Bora Wa Kufanya Mapenzi Ili Kupata Mimba Baada Ya Hedhi