Mbinu 5 Kuu Za Kupanga Uzazi Na Kuzuia Mimba Baada Ya Ngono

Mbinu 5 Kuu Za Kupanga Uzazi Na Kuzuia Mimba Baada Ya Ngono

Mwanamke anaweza tumia mbinu hizi kuzuia mimba baada ya ngono. Utumiaji wa kondomu na kujitenga na ngono hata hivyo ndizo mbinu kuu.

Mwanamke anaweza kuzuia mimba baada ya ngono kutumia njia zipi? Kuna baadhi ya mbinu ambazo zinamlinda mwanamke kuto pata mimba. Tazama!

Mbinu kuu za kupanga uzazi

Kondomu

kuzuia mimba baada ya ngono

Hii ndiyo kinga dhabiti ya kukulinda dhidi ya maambukizi ya ngono pamoja na mimba. Inatumika wakati watu wanapo jihusisha katika tendo la ndoa pekee, ni rahisi kubeba wakati wowote na haina homoni zozote. Kuna aina mbili za kondomu, za kike na za kiume.

Kondomu ya kiume inavaliwa kwenye kibofu na kuzuia manii kupita kwenye sehemu za kike wakati wa ngono. Kumlinda mwanamke kutokana na kupata mimba baada ya ngono.

Tembe za kupanga uzazi

kuzuia mimba baada ya ngono

Mwanamke anahitajika kumeza tembe moja kila siku. Kuna aina tofauti ya tembe ambazo mwanamke anaweza chagua kutoka, ili apate itakayo mfaa zaidi. Kuna tembe zilizo na vichocheo viwili, estrogen na progestin na zilizo na homoni moja peke yake, ya, progestin.

Ina manufaa mengi, hata ingawa lazima mwanamke aichukue kila siku. Kuto ichukua huenda kukamfanya atunge mimba. Ina wasaidia wanawake walio na upele kwenye uso, kupunguza uchungu wa hedhi hata ingawa hailindi dhidi ya maambukizi ya kingono.

Intrauterine Device (IUD)

kutoa IUD

Kifaa hiki kina umbo la 'T' na kina ingizwa kwenye mlango wa uke wa mwanamke na daktari aliye na umahiri. Huenda kikawa cha copper ama homoni ya progesterone. Baada ya kufanya ngono bila kinga, mwanamke anaweza wekwa kifaa hiki kabla ya siku tano ili kumlinda dhidi ya kutunga mimba.

IUD zina uwezo wa asilimia 99% wa kukulinda dhidi ya kupata mimba. Hata hivyo, zina athari hasi, kama vile kutoa matone ya damu yasiyo ya kawaida miezi ya kwanza sita baada ya kuweka. Lazima kifaa hiki kiwekwe na kitolewe na daktari na hakikulindi dhidi ya maambukizi ya kingono.

Sindano ya kupanga uzazi

Sindano hii huwa na homoni ya progesteron. Hudungwa kwenye kiungo cha mkono ama makalio ya mwanamke na kichocheo hiki huendelea kutolewa kwenye mfumo wa damu  katika muda wa wiki 12 zinazo fuata. Sindano hii hudumu kwa muda wa miezi mitatu. Ni muhimu kwa mwanamke kukumbuka siku ili asipitishe miezi mitatu bila kupata sindano nyingine.

Tembe ya asubuhi (Morning After)

antibiotics resistance

Tembe hii hutumika kuzuia mimba baada ya kufanya ngono ikiwa hakuna mbinu yoyote ya kupanga uzazi iliyo tumika. Ama ikiwa kondomu iliyo tumika ili pasuka. Mwanamke anahitajika kuichukua kabla ya siku tano kupita kutoka siku alipo fanya kitendo cha ndoa.

Hata hivyo, mwanamke hapaswi kuchukua zaidi ya mbili kila mwaka.

Chanzo: Healthline

Soma Pia:Mambo Ya Kutarajia Maji Yanapo Vuja Kabla Ya Kushuhudia Uchungu Wa Uzazi

Written by

Risper Nyakio