Mwanamke anapokuwa na mimba, huenda akawa ameambiwa mara nyingi kuwa kunyonyesha ni aina ya uzazi wa mpango. Je, imani hii ni kweli? Tuna dadisi zaidi kuhusu kunyonyesha kama njia ya uzazi wa mpango na kuzuia mimba mama anaponyonyesha.
Mama anaponyonyesha peke yake bila kumlisha mtoto kitu kingine na kumnyonyesha kwa muda mrefu, nafasi zake za kupata mimba zinapungua. Mbinu hii kama njia ya kupanga uzazi huwa na ufanisi zaidi katika miezi ya kwanza sita baada ya kujifungua. Ili kufuzu, mama anastahili kunyonyesha mtoto baada ya kila masaa manne.
Ni vyema wakati wote kuzungumza na daktari wako baada ya kujifungua kuhusu njia bora za kuzuia mimba unaponyonyesha. Kuna baadhi ya njia za uzazi wa mpango zinazo punguza utoaji wa maziwa na kuathiri lishe ya mtoto.
Tazama baadhi ya njia za uzazi wa mpango unaponyonyesha
- Kutumia mipira ya kondomu

Mipira ya kondomu huwa salama kwa mama na ina uwezo wa kukinga dhidi ya kupata maambukizi na mimba kwa asilimia 98. Isipokuwa pale mpira unapovunjika katika tendo. Inapotumika ipasavyo, wanandoa hawana shaka ya kupata maambukizi ama mimba. Kuna aina tofauti ya kondomu, kuna za kike na za kiume na zilizo na lubricant na zile zisizo kuwa nayo.

Zinafahamika kuwa na ubora wa asilimia 99 ya kukinga dhidi ya kupata mimba. Kuna aina mbili ya IUD, iliyo na homoni na isiyo na homoni. IUD zilizo na homoni huwa na kichocheo cha progesterone kinachofanya kamasi kutoka kwa kizazi kuwa kinene na kuzuia manii kutofika kwenye uterasi. Njia hii ya kupanga uzazi ni bora kwa wanawake walio na mchumba mmoja wa kimapenzi. Kuwa na wachumba wengi kunawaweka katika hatari ya kuugua maambukizi ya kingono. IUD zenye homoni humfanya mwanamke kukosa kupata hedhi yake ama ikawa nyepesi zaidi.

Tembe za jadi huwa na mchanganyiko wa vichocheo vya estrogen na progestin. Homoni ya estrogen inasemekana kuathiri utoaji wa maziwa na kumfanya mama kutoa maziwa iliyopunguka na kunyonyesha kwa muda mfupi zaidi.
Kuna tembe zilizo na homoni ya progestin peke yake na huwa bora zaidi kwani haziathiri utoaji wa maziwa. Mwanamke anapofanya uamuzi wa kupata mimba tena, huenda rutuba ikarudi punde tu anapokoma kutumia tembe hizi. Hata hivyo, ni vyema kuwasiliana na daktari wake.
Ina pachikwa chini ya mkono baada ya upasuaji mdogo. Ina uwezo wa kuzuia mimba kwa miaka minne. Implant zina homoni ya progestin inayo saidia kuzuia ovari kuachilia mayai. Ni vigumu mimba kufanyika pasipo na yai.
Mama anapaswa kuzungumza na daktari kuhusu njia za kuzuia mimba mama anaponyonyesha kabla ya kwenda nyumbani baada ya kujifungua.
Soma Pia: Jinsi Ya Kupanga Uzazi Kwa Kutumia Mbinu Za Kiasili!