Sababu Kwa Nini Mungu Humleta Mwanamke Na Mwanamme Pamoja

Sababu Kwa Nini Mungu Humleta Mwanamke Na Mwanamme Pamoja

Mungu hafanyi mambo kwa kiholela. Kuna sababu kwa kila jambo.

Mungu amekuwa kwa biashara ya kuwaleta wachumba pamoja kutoka siku za Adamu na Eva. Iwapo hauna mchumba na unashangaa iwapo Mungu huwaleta watu pamoja, huenda hili lisiwe swali la kipekee unalo kuwa nalo akilini. Huenda ukawa pia unajiuliza iwapo utawai patana na mchumba kutoka kwa Mungu ama iwapo utawai shuhudia mapenzi. Unapaswa kuamini kuwa Mungu anaweza na atakupeleka kwa mtu aliye sawa kwako. Kwa swali, kwa nini Mungu humleta mwanamke na mwanamme pamoja? Jibu la kawaida ni kuwa Mungu ni Mungu wa maksudi. Ana kusudi la kila jambo afanyalo.

why does God bring a man and woman together

Kwa nini Mungu humleta mwanamme na mwanamke pamoja?

 Kwa nini Mungu humleta mwanamke na mwanamme pamoja? Baadhi ya mifano ya kibibilia

  1. Adamu na Eva

Mungu mwenye aligundua kuwa alipaswa kuumba mchumba wa Adamu, kwa hivyo akamlaza kwa usingizi na kisha kuumba Eva. Adamu hakumwuliza Mungu ampe bibi, ila katika bibilia kitabu cha kwanza 2:18, Mungu aliamua kuwa maisha ya Adamu yangekuwa na utajiri zaidi iwapo angekuwa na ‘msaidizi bora.’

2. Isaka na Rebekah – Genesis 24: 1 – 67

kwa nini Mungu humleta mwanamke na mwanamme pamoja

Isaka alipo fikisha umri wa kuoa, babake Ibrahimu alimtuma mtumwa wake kwa jina Haran kumtafutia Isaka bibi. Mtumwa huyu alijua umuhimu wa kuto tafuta mchumba tu ila pia kutafuta bibi mzuri. Mtumwa huyu aliomba na kumwuliza Mungu ampe ishara: mwanamke yeyote ambaye angempatia maji yake na ya mifuko wake angekuwa mwanamke bora kwa Isaka.

Baada ya safari ndefu, mtumwa huyu alifika kisiwani. Alikuwa amechoka na pia mifugo wake. Alipatana na Rebekah kisiwani na akampa maji na pia mifugo wake. Hapo Haran alitambua kuwa huyu ndiye alikuwa mchumba aliyefaa.

3. Kwa nini Mungu huwaleta watu pamoja? Ruth na Boaz

Iwapo unashangaa kwa nini Mungu huleta mwanamme na mwanamke pamoja wakati ambapo mmoja wao alikuwa ameolewa hapo awali; unapaswa kusoma kutokana na hadithi ya Boaz na Ruth. Hadithi hii ina ashiria kuwa kuna uwezekana wa kupata mapenzi hata baada ya kumpoteza mchumba kupitia talaka ama kifo. Kitabu cha Ruth kina ashiria kidokezo hiki.

Ruth alikuwa mwenye bidii na Boaz aliona jambo hili alipo mwona akifanya kazi kwenye kiwanja. Halikuwa kusudi lake kupata uangalifu wake, kusudi lake lilikuwa kufanya kazi ili wapate chakula yeye na mama mkwe wake Naomi.

4. Rachel na Yakobo

Hadithi ya wanandoa hawa ni mfano mzuri wa mapenzi yasiyo isha. Yakobo alienda kumtafuta bibi kwa familia ya babake. Alipatana na Rachel kisimani na kumpenda. Kitabu cha Genesis:29 kinaeleza kuhusu hadithi hii na kueleza kuwa yao yalikuwa mapenzi baada ya kuonana kwa mara ya kwanza. Yakobo alilia alipo mwona.

Kwa bahati mbaya, Yakobo alidanganywa na kumuoa dada mkubwa wa Racheal kwa jina la Leah, kwani ilikuwa mila dada wa kwanza kuolewa kabla ya wa pili. Yakobo alilazimika kufanya kazi kwa miaka 14 kabla ya kumuoa mpenzi wake.

kwa nini Mungu humleta mwanamke na mwanamme pamoja

Mungu anaweza kuunganisha na mchumba unaye mtamani

Mambo ya kufanya iwapo una matumaini ya kuwa na mchumba

Does God Bring People Together

Mwanzo, jibu la swali lako jinsi Mungu anavyo waleta watu wawili pamoja ni rahisi sana. Mungu hufanya kazi kwa njia zisizo eleweka! Unapaswa kuwa na imani na kuamini kuwa litakutendekea.

1. Omba

Omba mwenyezi Mungu kuhusu matakwa yako ya kutaka kuwa na mtu. Wanandoa wetu wa kibibilia waliomba kabla ya kuanza kutafuta. Na mwelekezo wa Mungu, unaweza elekezwa mahali panapo faa na wakati unaofaa pia.

2. Zingatia kazi yako

Haupaswi kuyasimamisha maisha yako yote kwa sababu una ngoja mchumba. Jikuze. Timiza malengo yako ya maisha na utie kazi kufika mahali ambapo unataka kufika maishani. Wachumba wengi walipata kuwa wenzi wao walipo kuwa kazini. Rebekah na Rachel wote walikuwa wanafanya kazi kwenye kisima walipo patana na mabwana zao.

3. Familia na wazazi wenu wanaweza kuwaunganisha

Kuwauliza marafiki wako wakuunganishe na watu wasio na wachumba sio ishara ya kukata tamaa. Badala yake, ni njia bora ya kujiweka katika nafasi ambayo utapatikana. Katika kesi ya Ruth, mama mkwe wake alimpatia vidokezo vya kumfanya Boaz awe na hamu yake, linalo jibu swali la, jinsi Mungu anavyo waleta watu wawili pamoja. Kujulikana kwa Naomi kulimsaidia Ruth kujulikana na kuwa bibi ya Boaz.

4. Kuwa mtulivu

Jacob alidanganywa kumuoa Leah, na akalazimika kungoja miaka 14 kumwoa Rachel- mwanamke ambaye alikuwa anamtamani kwa muda mrefu. Vitu huenda vikakosa kutendeka mbio unavyo vitamani, ila ukiwa mtulivu, mambo yote yatakuwa salama mwishoni.

Mungu hufanya kazi njema sana katika kuwaleta wageni wawili pamoja ili waanze uhusiano wa mapenzi. Unapaswa kuamini kuwa utapata nafasi yako katika mapenzi!

Vyanzo: thescriptures.co.uk

Soma pia: You will fall in love with these breathtaking vacation spots in Nigeria

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio