Kwa Nini Watoto Hukoroma

Kwa Nini Watoto Hukoroma

Kwa nini watoto hukoroma wakiwa wamelala? Napaswa kuwa na shaka ama ni jambo la kawaida? Makala haya yana angazia zaidi kuhusu kukoroma kwa watoto.

Watoto hufanya aina zote za mambo uzizo tarajia wakiamka na hata wakilala. Ambayo huenda ukakosa uhakika iwapo unapaswa kuwa na shaka ama la. Watoto wachanga hufanya kelele nyingi kutoka kupumua kwa nguvu wakiwa wamelala, kucheka, kutabasamu na kadhalika. Pia, watoto hukoroma kwa njia inayo pendezwa ikilinganishwa na watu wazima. Kwa hivyo, unapaswa kuwa na shaka mtoto anapo koroma na kwa nini watoto hukoroma?

Kwa Nini Watoto Hukoroma?

Watoto wadogo huwa na mapua yaliyo jazwa na viputo. Wanapo pumua , hewa inayo pitia kwa viputo hivi hutoa sauti. Na kusababisha kukoroma kwao.

Wanapo endelea kukua, mapua huendelea kupanuka, na mtoto anasoma jinsi ya kumeza mate zaidi, na kukoroma kwao kuna punguka.

Kukoroma kule kukiendelea, huenda ikawa ishara kuwa mfumo wao wa kupitisha hewa una fanya kupumua kwao kutatizike.

Jinsi ya kupunguza kukoroma kwa watoto

kupata mtoto wa kike

  1. Safisha mapua yao

Sio lazima uende hospitalini ili mapua ya mtoto wako yasafishwe. Unaweza fanya hivi ukiwa nyumbani. Unacho hitajika kufanya ni kumwaga matone machache ya maji ya chumvi kwenye mapua ya mtoto wako, mara moja ama mbili kwa siku.

Pia, unaweza pata kwenye duka la dawa, kisha utumie nasal aspirator kutoa uchafu.

2. Tumia mvuke

Unajua unavyo weza kupumua kwa urahisi unapo oga kwa maji moto? Fanya vivyo hivyo na mtoto wako. Enda kwenye bafu pamoja na mtoto wako kabla ya kulala. Na uwache mvuke upunguze uchafu ulioko kwenye mapua yake.

3. Toa vitu vinavyo sababisha mzio kwenye chumba chake

mtoto kutoa jasho jingi akiwa amelala

Mojawapo ya sababu zinazo fanya mfumo wa kupumua wa mtoto wako ufungane ni vumbi na vitu vinavyo sababisha mzio. Toa vitu vinavyo kusanya vumbi kama vile vidoli laini na zulia.

4. Tumia kisafisha hewa (air-purifier)

Nunua kifaa hiki na ukiweke kwenye chumba cha kulala cha mtoto wako. Ili kisafishe hewa na hata lala kwenye chumba kilicho na hewa chafu.

5. Badili mtindo wa kulala wa mtoto wako

Mojawapo ya sababu kwa nini mtoto wako ana koroma ni unavyo mlaza. Baadhi ya watoto huenda waka koroma sana anapo lala kwa tumbo, na kukosa kukoroma wanapo lazwa kwa mgongo. Hakikisha kuwa mtoto wako analala kwa mgongo kuepusha kisa cha kifo cha ghafla cha watoto.

Japo mtoto anavyo endelea kukua, kukoroma kutapunguka. Asipo acha kukoroma akiwa amelala, ni wakati wa kumwona daktari. Ili adhibitishe ikiwa kuna jambo la kiafya linalo msumbua.

Chanzo: Healthline

Soma piaJinsi Ya Kufunza Watoto Mtindo Wa Maisha Wenye Afya Shuleni Na Nyumbani

Written by

Risper Nyakio