Wakati unapofika wa kuanza familia, kila mtu huwa na hamu na furaha ya kuanzia safari hii. Walakini, sio kila mwanamke anayetunga mimba kwa urahisi, wengine huchukua muda, huku ikibidi wengine kutunga mimba kupitia usaidizi wa njia za teknolojia. Kwa nini ni vigumu kupata mimba?
Jinsi mimba inavyofanyika

Mimba hufanyika pale ambapo yai kutoka kwa ovari hupatana na manii ya mwanamme na kurutubishwa. Uterasi huandaa kuta maalum maarufu kama endometrium ili yai lililorutubishwa kujipandikiza. Ujauzito usipofanyika, kuta ya endometrium humomonyoka na kutoka kama hedhi.
Mwanamke anapofanya mapenzi bila kinga siku ya, ama siku chache kabla ya siku ya kupevuka kwa yai, manii hufika kwenye kizazi na kuingia kwenye uterasi ya mwanamke. Na kupatana na yai lililokomaa linalongoja kurutubishwa. Baada ya yai kurutubishwa, koti hukua nje ya yai na kuepusha seli zingine za manii kuingia. Yai hili hukaa kwenye mirija ya ovari kwwa siku tatu kisha kuanza kusafirishwa kwenye uterasi. Na kujipandikiza kwenye kuta za uterasi. Katika wakati huu, kuna baadhi ya wanawake wanaoshuhudia kuvuja damu nyepesi. Safari ya ujauzito inaanza.
Sababu zinazo fanya iwe vigumu kutunga mimba

Safari ya kutunga mimba huwa tofauti kwa kila mwanamke. Kuna baadhi ya wanawake ambao hutunga mimba punde tu wanapokoma kupanga uzazi. Huku wengine wakichukua muda zaidi. Kipi kinachofanya iwe vigumu kutunga mimba?
Katika mzunguko wa hedhi wa kila mwezi, mwanamke huwa na kipindi anapokuwa na rutuba zaidi na chanya kikubwa cha kushika mimba. Ili kushika mimba kwa urahisi, mwanamke hushauriwa kufanya ngono bila kinga katika siku hizi.
Ikiwa vipindi vya hedhi vya mwanamke sio vya kawaida, ni vigumu kwake kufahamu siku anapokuwa na rutuba zaidi na kupunguza nafasi zake za kushika mimba. Kwa wanawake walio na tatizo hili, ni vyema kuwasiliana na daktari ili akusaidie kurekebisha hali hii na kufahamu siku zake za rutuba.
Ni vigumu kutunga mimba mwanamke anapokuwa na mawazo mengi. Vichocheo vinavyo athiri kupevuka kwa yai. Mwanamke anapokuwa na mawazo mengi, huenda ovari ikakosa kuachilia mayai.
Huenda wanandoa pia wakakosa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Ikiwa wachumba wana fikira nyingi, ni vyema kung'amua chanzo cha mawazo yale na kutafuta suluhu lake.
Kadri na siku za hapo awali ambapo wanadada wangepata watoto wangali wachanga, siku hizi wanawake wengi wanafanya uamuzi wa kungoja zaidi. Hadi wanapotimiza malengo yao ya kimasomo na kikazi kabla ya kuanza kurasa ya kulea. Jinsi wanavyozidi kungoja kupata watoto, ndivyo inavyokuwa vigumu kwao kupata mimba. Hata hivyo, wanawake bado wanaweza kutunga mimba, kupitia kwa mbinu za teknolojia ya kisayansi zinazo ibuliwa kila uchao. Ikiwa mwanamke angependa kutunga mimba kwa njia asili, ni vyema kufanya hivi angali mchanga.
Mbali na sababu hizi, ni vyema kwa wanandoa wanaolenga kuwa wazazi kuwa makini na mitindo yao ya kimaisha. Kwa kupunguza utumiaji wa vileo na sigara ili kuongeza nafasi zao za kutunga kwa urahisi. Kufahamu kwa nini ni vigumu kupata mimba kunawasaidia wanandoa kujua wanachostahili kufanya.
Ikiwa umri wenu ungali mchanga na hata baada ya kufanya ngono bila kinga kwa mwaka mmoja bado hamjapata mimba, ni vyema kuwasiliana na daktari afanye vipimo na kudhibitisha tatizo ni gani.
Soma Pia: Kufanya Mapenzi Katika Mimba Ni Salama Kwa Mtoto? Maswali Kuhusu Ngono Katika Mimba