C-section ni aina ya upasuaji inayotumika kujifungua mtoto. Mama anakatwa upande wa chini wa uterasi ili kuwawezesha madaktari kumtoa mtoto. Ni aina ya upasuaji ulio maarufu. Upasuaji huu unaweza kuepukwa kabla ya wiki ya 39 ya ujauzito. Katika wakati huu, mtoto huwa na wakati tosha wa kukua kwenye uterasi. Baadhi ya wakati, matatizo huenda yakaibuka katika ukuaji wa mtoto kabla ya kufikisha wiki 39 na kumlazimisha mama kufanyiwa upasuaji wa c-section. Je, kwanini upasuaji wa c-section hufanyika?
Sababu kwanini upasuaji wa C-section hufanyika

Mara nyingi, upasuaji wa aina hii hufanyika mama anapopata matatizo katika safari yake ya ujauzito. Matatizo ya kiafya yanayo hatarisha maisha ya mama ama ya mtoto huenda yakamfanya mama kufanyiwa upasuaji wa C-section ili kuyanusuru maisha ya mama na mtoto ama mmoja wao.
Huenda upasuaji huu ukapangwa katika safari ya ujauzito ama kufanywa dakika ya mwisho mama anapokaribia kujifungua kama suluhu la dharura. Kuna baadhi ya sababu za upasuaji huu, kama vile:
- Mtoto anayekua kwenye uterasi anapokuwa na matatizo ya ukuaji
- Matatizo katika safari ya ujauzito
- Mtoto kutoka asivyopaswa, miguu kwanza badala ya kichwa kwanza

- Kichwa cha mtoto kuwa kikubwa sana
- Matatizo ya kiafya kwa mama kama shinikizo la juu la damu
- Kujifungua hapo awali kwa njia ya upasuaji wa c-section
- Matatizo na placenta
- Matatizo ya kitovu
- Mtoto kutopata hewa tosha
Mama kukawia muda mrefu kabla ya kujifungua ama kuwa kwa uchungu wa uzazi kwa muda mrefu
Hatari za upasuaji wa c-section

- Kutokwa damu nyingi
- Mtoto kutatizika kupumua hasa anapofanyiwa upasuaji kabla ya kufikisha wiki 39
- Mama ako katika hatari ya kupata maambukizi
- Mama huchukua muda mrefu kupona
- Damu kuganda na kuwa vigumu kusafiri mwilini
- Hatari zilizo ongezeka kwa mimba ya usoni
Mama anapoenda kliniki za ujauzito, anafanyiwa vipimo vinavyoonyesha hali ya ujauzito wake. Iwapo una afya ama la, na njia bora ya kujifungua kwa mama. Daktari atamshauri mama kuhusu anavyopaswa kujitayarisha kabla ya siku kuu ya kujifungua.
Chanzo: WebMd
Soma Pia: Jinsi Ya Kuhakikisha Kuwa Kidonda Chako Cha C-section Kinapona Mbio