Kunya: Kwanini Watoto Hushikilia Kinya na Jinsi ya Kuwasaidia

Kunya: Kwanini Watoto Hushikilia  Kinya na Jinsi ya Kuwasaidia

When your child keeps withholding poop, it could lead to them being very uncomfortable. However, it could be because of fear or constipation and you can help them through it.

Inaweza onekana kama jambo la kuchekesha, mtu anaposikia kuwa mtoto amekataa kunya. Lakini ni shida ya kweli na wazazi wanaweza kuwasaidia watoto wao. Kina fahamika kama kushikilia kinya ambacho kinajulikana kama woga wa kunya.

Kunya: kwani nini watoto hushikilia kinya

kunya

Kushikilia kinya kwa watoto ni jambo ambalo hutokea kwa mara nyingi na kwa hivyo ni kawaida.  Mtoto anaweza kuwa anakojoa vizuri lakini anafanya juu chini kushikilia kinya. Kwa hivyo si jambo geni kumpata mzazi akifanya kila awezalo kumfanya mtoto akunye. Ahadi za vitu za kuchezea na kwenda kutembea kwenye mbuga zitafanywa ilhali bado mtoto atakataa kunya.

Kuna sababu chache zinazo pelekea jambo hili kufanyika. Sababu kama vile kuwa na mtoto anayejua jinsi unavyohisi.  Anapo kataa kwenda choo. Unavyo litazama kuwajambo kubwa ndivyo linavyo endelea kushikilia nya. Pia watoto hawapendi wakati wao wa kucheza ukikatizwa. Mwanzo, wanaweza kuwa wanapenda kukaa kwa choo kwa sababu ni mpya. Lakini wakati unavyozidi kupita hilo hubadilika na wanaanza kushikilia nya. Hili huwezekana kwa kuwa mtu anapokosa kunya hio haja huweza kupita.  Vile mtoto anavyozidi Kukosa kunya ndivyo choo chake kinazidi kuwa kigumu. Na matokeo ni kuwa wakati atakapoitikia kunya huwa chunga ikimfanya mtoto kuwaza sitawai fanya hivi tena.

Kunya: Kwanini Watoto Hushikilia  Kinya na Jinsi ya Kuwasaidia

Hata hivyo, shida nyingine yaweza kuwa tatizo la kudumu la kufunga choo. Iwapo mtoto wako ana hii shida anaweza kuwa hatapatwa na kwenda haja kubwa. Mwishowe yaweza toka bila yeye kutarajia ikimfanya mtoto kujiendea choo. Kukomesha hili kutahitaji kukomesha kufunga choo ambayo itafanyika tu kwa usaidizi wa daktari.  Hizo ndizo sababu watoto hupatwa na kufungika kwa choo.

  • Maji huweka nya ikiwa nyepesi. Kwa hivyo mtoto asipokunywa maji ya kutosha choo huweza kuwa kigumu.
  • Mkazo wa mawazo. Hili hufanyika wakati ambapo mtoto wako ana wasiwasi juu ya kitu ambacho hajafanya kama vile kazi ya ziada.
  • Tumbo la mtoto wako laweza enda pole kwa kutokuwa na nyuzinyuzi kwa lishe lake. Punguza chakula chenye sukari na wanga na uongeze chakula chenye nyuzinyuzi nyingi.

Ni nini chakufanya wakati mtoto wangu anashikilia kinya?

kinya

Bahati ni kuwa kuna njia nyingi za kumsaidia mtoto wako anaposhikilia kinya. Vidokezo vifuatavyo vitakusaidia.

  • Kuwa mvumilivu

Ata katika watu wazima, twajua kuwa choo kwa wakati mwingine huchukua wakati wake mzuri. Kuna wakati choo huja haraka na wakati mwingine huwa mchakato. Ata hivyo, ni vigumu kuto fadhaishwa  na mtoto wako kutonya. Lakini lazima uelewe kuwa kuharakisha kwako hakutamfanya mtoto atake kunya. Kama chochote, kutamfanya mtoto azidi kushikilia nya. Kwa hivyo kukaa kama jambo hilo halikusumbui husaidia sana.

  • Ongelesha mtoto wako

Vile ambavyo mtoto anazidi kushikilia nya ndivyo mambo yanavyozidi kuwa magumu kwake. Ingawa mtoto haoni hivyo. Unaweza kuongea na mtoto wako ukimfahamisha  umuhimu wa kujaribu na kunya lakini kwa upole sana. Pia, jiepushe na kumshtua mtoto wako ama hilo litamfanya tu kuwa mwenye hofu. Usiseme kitu kama vile, “ kama hautanya huu wakati utaanza kumwaga choo.” Ila angazia manufaa ya kunya. Sema kitu kama vile “Huwezi zidi kula chakula unachopenda bila kwenda choo  kwani hii ni sehemu muhimu kwa siku yenye afya.

  • Thibitisha desturi

Hii ni sawai na unavyothibitisha desturi ya kulala. Unaweza tenga nyakati ambazo wamtaka mtoto kujaribu kunya. Jinsi tu unavyomfanya mtoto kwenda haja ndogo kabla alale.  Lakini kwenda haja kubwa kwaweza kuwa baada ya kula chakula kwani hiki husaidia kukaza tumbo. Lakini lazima ukubali kuwa mtoto hatanya kila wakati utajaribu ila lazima uzidi kujaribu.

  • Badilisha lishe

Hili laweza kosa kukomesha hio shida lakini litasaidia. Kufunga choo ni sababu moja ambayo husababisha mtoto asinye. Kwa hivyo, kuongeza kula chenye nyuzinyuzi nyingi kwa lishe lake itasaidia kufanya choo chake kiwe laini. Nyuzinyuzi hupatikana kwenye matunda mengi na mboga. Ingawaje, kama kushikilia nya kwa mtoto wako si kwa sababu ya hii shida, hili litafanya kidogo sana kusaidia.

  • Mwache mtoto wako afanye uamuzi

Kuna nyakati ambazo mtoto atakataa kwenda haja kwa choo lakini ataenda kwa diaper. Hii hutendeka wakati ambapo unajaribu kumfanya atumie choo. Mara nyingi wakati hili linatokea, ni njia yake ya kukuambia kuwa hayuko tayari kutumia choo . Kwa hivyo usimlazimishe. Usitilie mkazo lazima mtoto atumia choo. Njia unayoweza kujaribu ni kutengeza shimo kwenye diaper. Hivi, mtoto atakuwa na diaper na bado anaenda choo.

Kwa hivyo, unapoona mtoto ana shida ya kwenda haja kubwa unafaa kumwona daktari. Daktari atamchunguza na kudhitibisha kama ana maumivu kwa tumbo lake.

 

Read also: Food Poisoning In Kids: All You Need To Know To Keep Your Kids Safe

Kids Health

Written by

Risper Nyakio