Kwa muda mrefu sasa, kumekuwa na imani zisizo za kweli kuhusu endometriosis. Tunafahamu zaidi kuhusu hali hii na jinsi inavyoathiri mimba.
Endometriosis ni hali sugu ambapo tishu zinazokuwa upande wandani wa uterasi hukua ndani ya fuko la uzazi. Na kumfanya mwanamke ahisi uchungu mwingi wakati wa tendo la mapenzi, hedhi ama anapoenda msalani. Hali hii katika wanawake huwafanya kuhisi uchovu mwingi, kuhisi kutapika, kusababisha matatizo ya uzalishaji ama hata kupata matatizo na afya yao ya kiakili.
Karibu asilimia 10 ya wanawake duniani kote walio katika miaka yao ya kujifungua hutatizika kutokana na endometriosis.
Sababu zinazoongeza hatari ya kupata endometriosis

- Kuwa na mama aliye na hali ya endometriosis
- Kuwa na vipindi vya hedhi vyenye mzunguko wa siku chache kuliko 27
- Kuanzia vipindi vya hedhi kabla ya umri wa miaka 11
- Kuwa na vipindi vya hedhi vichungu, kuvuja damu nyingi na kipindi kudumu zaidi ya wiki moja
Hakuna matibabu ya hali ya endometriosis. Tuna angazia baadhi ya imani zilizoko kuhusu hali hii na iwapo ni kweli ama la.
Kweli kuhusu endometriosis
1.Vipindi vya hedhi huwa chungu na vyenye damu nyingi
Asilimia kubwa ya wanawake huhisi uchungu wakati wa hedhi, lakini uchungu wa kupindukia katika hedhi huenda ikawa ishara ya endometriosis.
Hata kama vipindi vya hedhi kwa waliokuwa na endometriosis huwa vikali na vichungu lakini sio wakati wote. Kuna baadhi ya wanawake hata baada ya kuwa na endometriosis huwa na vipindi vyepesi na visivyo na uchungu mwingi.
2. Endometriosis huathiri sehemu za uzalishaji za kike
Vidonda vya endometriosis hukua kwenye sehemu ya tumbo ya chini na pelviki. Hata kama vidonda hivi vinaweza kupatikana katika sehemu tofauti mwilini. Ukweli ni kuwa endometriosis hujipandikiza kwenye upande wa ndani wa tumbo inayofahamika kama peritoneum na kusababisha uchungu. Mbali na sehemu hii, vidonda hivi vinaweza kupatikana kwenye mafua na ubongo.

3. Mimba huponya endometriosis
Mimba kamwe haiponyi endometriosis. Baadhi ya wanawake hushuhudia kupunguka kwa uchungu wanapokuwa na mimba wala sio wote. Mimba husababisha viwango vya homoni mwilini kubadilika na kufanya watu tofauti kuwa na viwango tofauti vya uchungu baada ya kujifungua.
4. Mwanamke aliye na endometriosis hawezi kujifungua
Asilimia 35-50 ya wanawake walio na endometriosis hutatizika kujifungua, lakini hali hii haimaanishi kuwa mwanamke hawezi kujifungua. Wanawake wanaokuwa na hali hii na wanataka kubeba mimba wanashauriwa kufanya kazi kwa karibu na madaktari ili kuhakikisha kuwa wana nafasi za juu kushika mimba.
5. Kutoa mimba husababisha endometriosis
Chanzo cha endometriosis kingali hakijadhibitika. Lakini kutoa mimba sio chanzo cha endometriosis katika mimba.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Vidokezo 5 Vya Kupata Mimba: Kuongeza Nafasi Za Kupata Mtoto Kirahisi