Kila tunapoanzia urafiki mpya na mtu ama watu fulani, tungependa udumu miaka na mikaka. Ila, mambo hubadilika na watu pia kubadilika. Fahamu kweli kuhusu marafiki na urafiki.
Kweli 5 Kuhusu Marafiki

1.Urafiki bora sio marafiki wengi
Kadri tunavyozidi kuzeeka, ndivyo tunavyofahamu kuwa, ni bora kuwa na rafiki mmoja aliye na manufaa maishani mwako. Kuliko kuwa na marafiki 10 wasiokuwa na manufaa yoyote maishani mwako. Kuna tofauti ya kuwa na watu wengi unaowajua na kuwa na marafiki. Kujua watu hakumaanishi kuwa wao ni marafiki wako. Unapowahitaji, huenda hawatakusaidia. Badala yake, kuwa na marafiki wachache wanaoongeza ubora wa maisha yako, na unaofahamu kuwa unapowahitaji watakusaidia.
2. Marafiki hukosana
Marafiki waliojuana kwa zaidi ya miaka 20 hukosana. Kuwa marafiki wa dhati leo ama kwa muda mrefu sio hakikisho kuwa mtakuwa marafiki maishani mwenu hadi kifo. La hasha. Huenda jambo likatokea na kuleta utofauti mkubwa kati yenu. Urafiki uliokubwa mkubwa ukaharibika kufuatia jambo kama hilo. Ni jambo la kawaida kwa marafiki kutengana na ni sawa.
3. Mahusiano huathiri urafiki
Unapoingia katika mahusiano, urafiki wako utaathiriwa na kubadilika. Wakati ambao ungekuwa na marafiki wako, utakuwa na mchumba wako. Hautakuwa na muda mwingi wa kuwa na marafiki wako kama ilivyokuwa hapo awali. Huenda baadhi ya marafiki wako wa hapo awali wasifurahishwe na jambo hili. Wakijitenga nawe, usiwe na shaka. Hata hivyo, ni muhimu kuhakikisha kuwa hauyapi mahusiano yako cheo kikubwa maishani hadi kuwapoteza marafiki wako.

4. Kuwa rafiki yako mkubwa
Kuwa rafiki yako mkubwa kabla ya kuwa rafiki kwa watu wengine. Wakati mwingi uko peke yako, kwa hivyo usipofahamu jinsi ya kujipenda kwanza, itakuwa vigumu kuwapenda wengine. Unapojipenda, itakuwa rahisi kwako kuendelea na maisha yako hata baada ya kutengana na marafiki wako wa dhati.
5. Kutengana kwa marafiki huumiza
Sawa na mahusiano mengine yale, urafiki unapoisha, marafiki husika huumia moyo. Huenda ukahisi kujitenga na watu wengine na kutotaka kupata marafiki wengine baada ya kutengana na marafiki wako wa hapo awali.
Chanzo: Africaparent
Soma Pia: Njia Za Kutengeneza Marafiki Wapya Katika Miaka Ya 30’s