Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Kweli Kuhusu Mimba ya Ectopic: Yote Unayopaswa Kujua

3 min read
Kweli Kuhusu Mimba ya Ectopic: Yote Unayopaswa KujuaKweli Kuhusu Mimba ya Ectopic: Yote Unayopaswa Kujua

Kweli kuhusu mimba ya ectopic, vyanzo na mambo yanayohatarisha mama kupata mimba hii kama vile uvutaji wa sigara kabla ya kushika mimba.

Kwa kawaida, ili mimba kufanyika, yai lililorutubishwa hujipandikiza kwenye kuta za uterasi. Ila, yai lenye rutuba linapojipandikiza mahali pengine pasipo uterasi, mimba hii inafahamika kama ectopic. Ambapo yai hujipandikiza nje ya uterasi, kwenye mirija ya ovari, hali inayofahamika kama mimba ya tubal. Sehemu hizi haziwezi egemeza ukuaji wa yai.

Mimba ya ectopic ni hali inayotishia maisha ya mwanamke. Huenda akavunja damu hadi akaaga dunia isipo dhibitika mapema na kutibiwa. Mara nyingi mimba ya aina hii husababishwa na viwango vya homoni kutokuwa sawa mwilini na ukuaji usiofaa wa yai lililorutubishwa. Tuna angazia kweli kuhusu mimba ya ectopic, vyanzo, ishara, hatari na kinga zake.

Jinsi mimba ya ectopic inavyotendeka

kweli kuhusu mimba ya ectopic

Baada ya yai kurutubishwa, linapaswa kusafiri kupitia kwenye mirija ya ovari hadi kwenye uterasi. Katika mimba ya aina hii, yai hujipandikiza kwenye mojawapo ya sehemu kabla ya kufika kwenye uterasi. Mara nyingi huwa katika mirija ya ovari.

Hatari za mimba ya ectopic

Hii ni hali dharura ya kimatibabu. Jukumu la uterasi ni kuegemeza ukuaji wa fetusi. Inaweza kupanuka kuegemeza fetusi inayokua. Ila, mirija ya ovari haina uwezo huu. Huenda ikalipuka yai linapokua na kusababisha kuvunja damu kutoka ndani. Hali inayomhatarisha mama.

Kweli Kuhusu mimba ya ectopic: Ishara zake

  • Kuvunja damu katika mimba
  • Uchungu mwingi kwenye sehemu ya tumbo na mgongo
  • Kuhisi kukosa nguvu ama kuhisi kuzirai

Hali zinazohatarisha kupata mimba hii

kweli kuhusu mimba ya ectopic

Upasuaji wa tubal. Aina ya upasuaji kurekebisha mirija ya ovari iliyokuwa na tatizo inaongeza hatari ya kupata mimba ya ectopic.

Kuvuta sigara. Uvutaji wa sigara kabla ya kupata mimba unaongeza hatari yako ya kupata mimba ya ectopic, kadri unavyovuta.

Maambukizi. Maambukizi ya kingono kama vile chlamydia huenda yakasababisha uvimbe kwenye mirija ya ovari na sehemu zingine na kuongeza nafasi za mwanamke kutunga mimba ya ectopic.

Kuwa na mimba ya ectopic hapo awali. Wanawake waliotatizika kutokana na hali hii hapo awali wako katika hatari ya kupata mimba hii tena.

Matibabu ya rutuba. Baadhi ya utafiti unaashiria kuwa, wanawake wanaofanyiwa matibabu kama in vitro fertilizatio (IVF) huwa katika nafasi za juu kupata mimba ya ectopic.

Njia za uzazi wa mpango. Ni nadra kupata mimba unapokuwa ukitumia njia ya uzazi wa mpango ya IUD. Hata hivyo, iwapo utapata mimba ukiwa na IUD, nafasi kubwa ni kuwa itakuwa mimba ya ectopic.

Kinga

Hakuna njia hasa ya kuepuka kupata mimba ya aina hii. Lakini mwanamke anaweza kupunguza hatari za kupata mimba hii kwa kufanya haya:

  • Usivute sigara. Koma uvutaji wa sigara muda kabla ya kupata mimba.
  • Dhibiti idadi ya wapenzi wa kingono ulio nao ili kupunguza hatari ya kupata maambukizi ya kingono.

Chanzo: WebMD

Soma Pia: Mabadiliko 10 ya Kufanya Kabla ya Kupata Mimba

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Pregnancy
  • /
  • Kweli Kuhusu Mimba ya Ectopic: Yote Unayopaswa Kujua
Share:
  • Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

    Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

  • Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

    Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

  • Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

    Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

  • Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

    Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

  • Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

    Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

  • Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

    Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it