Hic... Hic... Jinsi Ya Kukomesha kwikwi Katika Watoto

Hic... Hic... Jinsi Ya Kukomesha kwikwi Katika Watoto

This is your guide to the cause and treatment of baby hiccups after feeding. Hiccups are mostly a result of reflux, which may be normal sometimes.

Sisi sote tumekuwa nazo na twajua jinsi kwikwi hukasirisha. Lakini wakati mtoto wako ana kwikwi, huwezi mfanya anywe kutoka kwa glasi ama kumuuliza ashike pumzi yake, wala huwezi jaribu tiba zozote zile za ajabu na za kufurahisha. Na kwa kweli huwezi wafanya waruke. Kwa hivyo, waweza fanya nini ili kuzuia na kukomesha kwikwi katika watoto baada ya kuwapa chakula?

Mwanzo, kwikwi ni nini?

jinsi ya kuepuka kwikwi katika watoto

Kwikwi  ni kubana kusiokuwa kwa hiari kwa kiwambo(misuli ilioko chini ya mapafu). Unapopumua ndani kiwambo huvutika chini na unapopumua nje hutulia na hewa hutiririka nje ya mapafu yako. Wakati mwingine kiwambo hufyeruka na huvutika chini kwa mshtuko.  Hii inaweza kufanya ukaingiza hewa kwenye koo kwa ghafla. Wakati hewa inpogonga zoloto lako nyuzi zako za sauti hufungika kwa kasi.

Kwikwi kwenye watoto

Hic... Hic... Jinsi Ya Kukomesha kwikwi Katika Watoto

Kwikwi ni kawaida katika watoto wachanga na wale wenye umri wa chini ya mwaka mmoja. Hii kwa sababu mfumo wao wa kusaga chakula bado haujajengeka. Sababu zingine zinazosababisha wewe kuwa na kwikwi ni sawa na za mtoto. Kama wanyonyesha ama kulisha mtoto ukitumia chupa utagundua kuwa mtoto wako huingiza hewa kwa urahisi wakati anakula. Hii huongeza uwezo wa kupatwa na kwikwi. Unaweza kugundua kuwa mara nyingi mtoto wako hupatwa na kwikiwi baada ya kula chakula. Hii yaweza sababishwa na reflux. Reflux ni kawaida maadam mtoto wako yu mzima hupaswi kuwa na wasiwasi.

Ulijua kuwa watoto hupatwa na kwikwi ata katika tumbo la uzazi?  Kuhisi mtoto wako akipatwa na kwikwi kunaweza kufurahisha kama  vile kuhisi akipiga  mateke na akifanya mapindu. Haupaswi kuwa na wasiwasi – ni kawaida kabisa.

Angalia vidokezo vyetu juu ya jinsi ya kukomesha  kwikiwi  katika watoto wachanga hapa chini:

Jinsi ya kuzuia kwikwi kwenye watoto kabla hazijaanza.

 

 

kwikwi katika watoto

  • Usimpe mtoto chakula kingi kupita kiasi. Kuweka kwa urahisi, mpe mtoto chakula mara mbili zaidi ya kawaida na nusu ya kiwango ambacho yeye hukula. Iwapo tumbo la mtoto wako hujaa upesi hili linaweza kusababisha kiwambo kupata jansi. Yaweza kuchukua muda kuangalia kiwango cha chakula kinachowafaa wewe na mtoto wako ili kuzuia kwikwi.
  • Kama unanyonyesha jaribu kumnyonyesha polepole huku ukimpa wakati wa kupumua unapobadilisha matiti. Msikize mtoto wako anaponyonya. Iwapo utaskia sauti za kugugumia ama umskie akiingiza hewa,ina maana kuwa mtoto wako hajashikilia matiti yako vizuri. Tunajua kunyonyesha kunaweza kuwa kibarua kigumu lakini usikate tama. Unahitaji tu kuhakikisha midomo ya mtoto wako imefungika vizuri kwenye chuchu yako.
  • Kama unanyonyesha ukitumia chupa,weka chupa katika pembe ya digrii 45 ili hewa iweze kwenda chini ya chupa. Na uangalie kuwa unatumia mtirirko ulio sawa kutoka kwa titi lako. Ikiwa mtiririko wa titi lako ni kasi, tumbo la mtoto wako laweza jaa haraka na kusababisha maumivu. Ikiwa mtiririko wa titi lako ni polepole yaweza kumfanya mtoto wako aliye njaa kufadhaika na kujaribu kunyonya kwa nguvu huku akiingiza hewa kwa wingi.
  • Mlishe mtoto wako kama yuko wima, anapotulia na ni mwenye furaha. Pia teua mtoto wako zaidi wakati anakula ili kusaidia kuzuia kwikwi. Jaribu kumweka wima kwa dakika 20 baada ya kumpa chakula ili chakula kitulie tumboni. Hii pia itazuia hewa kutotulia tumboni mwake. Pia , pindi baada ya chakula sio wakati mwafaka wa michezo ya kuruka.

Jinsi ya kukomesha  kwikwi katika watoto wakati tayari zimeanza

kwikwi katika watoto

Iwapo kwikwi zitaanza wakati unampa chakula, kumtikisa mtoto kidogo ama kumsugua kwenye mgongo kunaweza komesha kwikwi. Lengo ni kujaribu kumfanya mtoto apumzike ili kiwambo kitulie na hatimaye kwikwi ziishe.

Kama kwikwi zitaendelea kwa dakika chache baada ya kuacha kumpa chakula, kuendelea kumpa chakula kunaweza saidia.

Kama tujuavyo, kwikwi zaweza tokea bila onyo, kwa hivyo kama mdogo wako  anapatwa na kwikwi bila yeye kupewa chakula au kula chakula hivi karibuni hakikisha ametulia. Jaribu kumpa maji kidogo ama umpe sanamu  anyonye.  Kumbuka hufai kumpa mtoto wako sanamu kama bado hajazoea kunyonya. Iwapo bado kwikwi hazijaisha usiwe na wasiwasi kwani zitaisha kwa urahisi tu kama zilivyoanza.

Unapaswa kutafuta msaada lini?

Vipindi vingi vya kwikwi katika watoto hukaa kwa dakika chache tu ingawaje hazifurahishi sio chungu au kutishia maisha ya mtoto wako.  Unafaa kutafuta matibabu hata hivyo ikiwa hivyo vipindi vitakaa kwa masaa mengi , havidhibitiki au vinatokea  mara nyingi na kwa mfululizo.  Chanzo chaweza kuwa rahisi na bila madhara yoyote lakini kama bado una wasiwasi  zungumza na mkunga wako au daktari wako.

Resource: Mothercare

Also read: Experts find even more health benefits from breastfeeding for more than 6 months

Written by

Risper Nyakio