Suluhu Bora La Kwikwi Kwa Mtoto Mchanga

Suluhu Bora La Kwikwi Kwa Mtoto Mchanga

Kwa kawaida, kwikwi huisha baada ya dakika chache. Ila, zinapo zidi masaa zaidi ya 48 na kutatiza mtoto kula ama kulala, ni vyema kuwasiliana na daktari wake.

Kwikwi kwa mtoto mchanga huwa maarufu na sote tuna chukia kuwa nazo hata kama kuna wakati ambapo hatuwezi jidhibiti. Kwikwi zinaweza shuhudiwa kwa watu wote, wakubwa kwa wadogo. Muda ambapo kwikwi zina dumu una tofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, huenda zikawa za dakika chache ama masaa machache.

Mambo yanayo sababisha kwikwi kwa mtoto mchanga

Kwikwi kwa mtoto mchanga

 • Kumeza hewa nyingi
 • Kukula kiwango kingi cha chakula
 • Mabadiliko ghafla kwenye mwili na temprecha za mazingira
 • Kunywa vinywaji vilivyo na carbon
 • Furaha
 • Fikira nyingi za kihisia

Kwikwi ni maarufu zaidi kwa watoto kwa sababu mifumo ya kudhibiti utendaji kazi wa viwango fulani vya mwili bado una zidi kukua.

Matibabu salama ya kwikwi

Hata bila ya kuingiliwa kati, kwikwi hupungua ama kuisha baada ya dakika chache. Lakini kuna mbinu chache za kiasili za kutatua tatizo hili la kwikwi katika watoto wadogo.

Kwikwi kwa mtoto mchanga

Tazama:

 • Chai ya chamomile, peppermint ama fennel. Hivi ni mojawapo ya viungo bora zaidi za kutuliza misuli inayo sababisha kwikwi hizi. Tengeneza chai kwa kutumia viungo hivi, kisha uweke kiwango kidogo kwenye mdomo wa mwanao hadi pale atakapo koma kutoa sauti za kwikwi.
 • Shinikizo ndogo kwenye upande wa juu wa tumbo. Kwa utaratibu, finyilia upande wa juu wa mtoto wako kwa mwendo wa chini na wa kasi. Mara sawa na anapo pata kwikwi. Hakikisha kuwa hutumii nguvu nyingi kufanya hivi.
 • Kuwa makini na kupumua kwake. Kuna suluhu tofauti zinazo husisha kupumua. Na kwa sababu katika kesi hii ni mtoto, unaweza jaribu kumshika pua kwa sekunde mbili ili atumie mdomo kupumua na kufanya hivi kutapunguza kwikwi.
 • Kunywa maji baridi. Kumpa mtoto kiwango kidogo cha maji baridi kunaweza tuliza misuli inayo sababisha kwikwi katika watoto.
 • Mpapase acheke. Kumfanya mtoto acheke kutamfanya awe makini na kusahau kuhusu kwikwi na mara nyingi hili huwa suluhu bora.

Mambo ya kutofanya

 • Kamwe usimpe mtoto maji yaliyo na pilipili. Chakula chenye pilipili kinatumika kumaliza kwikwi kwa watu wazima ila sio kwa watoto.
 • Usimpe mtoto chakula ama maji akiwa amelala kwa mgongo. Kufanya hivi kunamtia katika hatari ya kukabwa na chakula.

Kwa kawaida, kwikwi huisha baada ya dakika chache. Ila, zinapo zidi masaa zaidi ya 48 na kutatiza mtoto kula ama kulala, ni vyema kuwasiliana na daktari wake.

Soma Pia:Chakula Cha Mtoto Wa Mwaka Mmoja: Mwongozo Wa Lishe Ya Watoto

Written by

Risper Nyakio