La Kutia Moyo! Jinsi Mama Alivyo Pita Mitihani Muda Mfupi Baada Ya Kujifungua

La Kutia Moyo! Jinsi Mama Alivyo Pita Mitihani Muda Mfupi  Baada Ya Kujifungua

Ujauzito na baada ya kujifungua ni misimu ambayo huja na changamoto zake. Ni jambo la kutia moyo kuona mama huyu akipita mitihani baada ya kujifungua.

Kuna mambo mengi ambayo mwili unafaa kuwa unarejesha baada ya kubeba mtoto kwa kipindi cha miezi tisa na kujifungua. Mwili unahitaji wakati mwingi wa kupata nafuu. Kutana na huyu mama aliyefanya vyema kwenye mitihani yake muda mfupi baada ya kujifungua. Ndio maana anapata umaarufu sana kwenye vyombo vya habari.

Kutana na mama huyu mchanga aliyefanya vyema kwenye mitihani yake muda mfupi baada ya kujifungua

mitihani baada ya kujifungua

Picha: Kiera Nelson/Facebook

Kiara Nelson aliwaonyesha wote waliokuwa na shaka kuwa wenye makosa, akiwemo mkufunzi wake ambao hawakuweza kuliona kuwa jambo la busara kufanya  mitihani yake muda mfupi baada ya kujifungua. Huo msimamo wa never-say-never uliwatia moyo wengi waliompongeza kwa kutosikiza mawaidha ya waliomkatisha tamaa walionena naye kabla ya kuifanya mitihani yake.

Huyu mama aliweza kushiriki picha yake akiwa bado hospitalini alipojifungulia mtoto. Alieleza kuwa alikuwa na mitihani miwili ya kufanya muda mfupi  baada ya kujifungua. Kiara alijifungua awali kabla ya wakati uliotarajiwa wa wiki 35 kwa sababu aliweza kupatwa na preeclampsia. Kwa sababu ya hii hali, na swala la kujifungua kwake, mkufunzi wake alipendekeza awachane na masomo.  Hakuweza kufikiria jinsi huyu mama angeweza kufanya mitihani yake haraka hivyo. Ila la wazi ni kuwa, Kiara alimwonyesha kuwa mwenye makosa.

“Nilipita mitihani yangu kwa alama za juu baada ya kujulishwa kuwa ningetolewa kutoka kwa hilo darasa.” Akaandika kwa mtandao wa kijamii.

mitihani baada ya kujifungua

Picha: Kiera Nelson/Facebook

Kiara aliendelea kuelezea matukio yalitokea kabla ya kufanya mitihani. Alikuwa amefadhaika kwa sababu ata baada ya kujifungua kwa sababu ya preeclampsia  katika wiki ya 35, alikuwa na kazi za ziada mbili za siku hiyo na mkufunzi wake hakuwa anampa nafasi. Mkufunzi wake alimwambia aachane na lile darasa kwani alifikiria hangeweza kufanya mitihani yake baada ya kupata mtoto.

mitihani baada ya kujifungua

Picha: Kiera Nelson/Facebook

Ingawaje, sio ata kunyonyesha kungemkomesha mama huyu wa msichana mdogo,  aliyekuwa amejitolea kuifanya mitihani yake.

“Ningelitumia hili jambo kama kisingizio lakini hilo lingeninufaisha aje. Maombi hufanya kazi kila wakati, Asante kubwa kwake Mungu” akaandika kwenye mtandao.

Soma Pia:  The Inspiring Story Of Florence Muia Nyenya

Vyanzo: Pulse

Written by

Risper Nyakio