Linet “Toto” Chepkorir, mwanadada mchanga mwenye miaka 24 ameshinda tiketi ya kuwania kiti cha msimamizi wa wanawake huko Bomet. Amewapiga washindani wengine wote dhidi ya kumaliza shule juzi.
Jina toto lilitoka wapi? Betty Langat katika mahojiano na televisheni ya Citizen alisema kuwa mtoto wake alizaliwa akiwa mdogo sana, na kwa hivyo kupatiwa jina toto. Licha ya juhudi za kuwacha jina hili, imekuwa vigumu jina hili kusahaulika.
Picha: Linet Toto Facebook
Katika mahojiano baada ya kushinda tiketi ya kuwania kiti cha msimamizi wa wanawake na chama cha UDA, Toto kama anavyofahamika kwa sana. Alisema kuwa mamake hakumuunga mkono katika uamuzi wake wa kujiunga na siasa hapo mwanzoni. Badala yake, alimshauri aendeleze masomo yake katika ununuzi na usambazaji aliyokuwa anasomea katika shahada yake. Kwa mara ya kwanza, alimwambia babake, aliye muunga mkono kwani ana historia ya uongozi hapo shuleni.
Licha ya kuwa alisomea kwenye shule zilizoko mtaani mwake, hakukata tamaa kuwa siku moja angekuwa mwana siasa. Baadhi ya masomo aliyopendelea zaidi shuleni ni Hisabati na Sayansi.
Ujasiri wake kuwania kiti cha kisiasa licha ya kuwa mdogo wa umri, kukosa fedha tosha za kampeni na kuwa freshi baada ya kumaliza shahada yake kunawapa vijana ujasiri zaidi kujitosa kwenye siasa. Bila uwoga kuwa huenda wakakosa kuchaguliwa kufuatia umri wao, raslimali ama kujuana na watu wakubwa.
Picha: Linet Toto chepkorir Facebook
Mojawapo ya malengo yake anapoingia bungeni ni kupitisha muswada wa kuwasaidia wanawake na wasichana kupata pedi za usafi ama sanitary towels kila mwezi.
Tunamtakia Toto yote mema katika safari yake mpya na ushindi katika uchaguzi ujao. Ni matumaini yetu kuwa vijana zaidi watajitosa kwenye dimbwi la siasa ili wapiganie nafasi zaidi za vijana, matakwa ya vijana pamoja na kazi na raslimali zaidi kukidhi mahitaji ya vijana.
Hadithi ya Linet Toto Chepkorir inawapa watu motisha kufuata ndoto zao haijalishi wanakotoka, walichonacho na wanacho hofia kuwa hawana. Kwa maneno ya mkimbiaji maarufu Eliud Kipchoge, hakuna binadamu aliye na uchache, kwa kimombo, ‘no human is limited.’
Soma Pia:Hongera! Baada Ya Kungoja Miaka 10, Mwimbaji Evelyn Wanjiru Ana Mimba