Lishe Na Siha Ya Mama Mwenye Mimba: Vyakula Muhimu Katika Mimba

Lishe Na Siha Ya Mama Mwenye Mimba: Vyakula Muhimu Katika Mimba

Lishe bora kwa mama mjamzito ni muhimu ili kuboresha afya yake na ya mtoto aliye tumboni mwake. Hakikisha kuwa unakula vyakula hivi.

Lishe katika ujauzito ni muhimu kwa wote, mama na mtoto anaye kua tumboni mwake. Mama anapo kula chakula duni, afya ya mtoto ina athirika. Kwa hivyo, hakikisha kuwa unakula vyakula vyenye afya. Tuna angazia mambo muhimu katika lishe bora ya mama mjamzito. Inapaswa kuwa na vitu hivi:

Lishe katika ujauzito

kumlisha mtoto asiyependa kula

Mengi yamesemwa kuhusu umuhimu wa lishe bora katika ujauzito. Tungependa kusisitiza jambo hilo kwa mama anaye tarajia. Hakikisha kuwa una kula vizuri. Kuna maana kuwa, unapaswa kula vyakula kutoka kwa jamii tofauti na pia chakula cha kutosha. Chakula kinakusaidia:

  • Kukingana dhidi ya maradhi katika ujauzito na baada ya kujifungua
  • Kuwa na meno na mifupa yenye nguvu katika safari ya ujauzito
  • Kupata nguvu tosha ya kufanya kazi
  • Katika uendelezaji wa ukuaji wa mtoto tumboni mwa mama
  • Mama kurudisha siha na nguvu haraka baada ya kujifungua
  • Katika utoaji wa maziwa tosha ya mama baada ya kujifungua ili kustawisha mwanao

Kula chakula kingi

Mwanamke mjamzito na anaye nyonyesha anahitajika kula chakula kingi zaidi ya kawaida yake, kwa sababu sasa hivi ana kiumbe kinacho kua tumboni mwake. Mtoto anatarajia chakula ambacho mama anakula ili kupata nguvu na kuendeleza ukuaji wake.

Kichefu chefu ni kawaida katika kipindi hiki maishani mwa mwanamke. Kwa hivyo, anastahili kula chakula tosha, ikiwa ana tatizika sana na kichefu chefu, ana himizwa kula chakula kidogo mara kwa mara.

Athari za lishe duni

Mwanamke mjamzito asipo pata chakula kinacho mtosha, huenda akaanza kuhisi dhaifu, uchovu, kutatizika kupigana dhidi ya maambukizi na matatizo mengine ya kiafya. Mama pia ako katika hatari ya kuharibika kwa mimba ama kujifungua mtoto mwenye uzani mdogo. Katika kesi sugu, huenda mama ama mtoto akaaga baada ya kujifungua.

Lishe bora ya mama mjamzito

Ili kuwa na siha njema, mama mwenye mimba anapaswa kula vyakula hivi ili mwili upate virutubisho vinavyo hitajika.

Kabohidrati (wanga) 

Lishe bora ya mama mjamzito

Vinafahamika kama vyakula vikuu. Katika kila lishe lazima kuwe na angalau aina moja ya chakula kikuu. Huenda kikawa, wali, sima, mahindi, ngano, mihogo, ndizi, mtama ama ndizi. Vyakula hivi ni muhimu katika kuupa mwili nguvu.

Protini 

Vyakula vijenzi ama vya kuukuza mwili hasa misuli, mifupa na damu. Jamii hii ya vyakula huwa kama vile nyama ya kuku, ng'ombe, mbuzi, samaki, maharagwe, ndengu, njugu, kunde na kadhalika. Mama anapaswa kuhakikisha kuwa chakula hiki kimeiva sawasawa kwani huenda kikawa na vimelea. Na kuathiri afya yake na ya mtoto.

Sukari na mafuta

Vyakula vitoavyo nguvu na kuupa mwili nguvu tosha ya kufanya utendaji kazi wake wa kila siku. Kama vile baadhi ya matunda yenye sukari na asali.

Vitamini na madini 

Lishe bora ya mama mjamzito

Hivi ni vyakula vilinzi ambavyo vina usaidia mwili kupigana dhidi ya maambukizi. Vyakula hivi vina saidia kudumisha uwezo wa kuona, uthabiti wa ngozi na mifupa. Matunda kama vile ndizi, papai, tufaha, parachichi na kadhalika. Mboga kama spinachi, mchicha, kunde, kabichi na zinginezo.

Viowevu

Lishe bora ya mama mjamzito

Mbali na vyakula, mama anapaswa kunywa maji safi angalau glasi nane kwa siku. Sharubati ya matunda, maziwa ya ng'ombe ama mbuzi na maziwa ya bururu.

Mbali na kula vyakula tulivyo orodhesha, lishe bora ya mama mjamzito ina andamana na usafi. Mama mwenye mimba anapaswa kuwa mwangalifu sana na usafi wa kibinafsi na wa chakula anacho kula. Kufuatia ongezeko la homoni mwilini, mama ana paswa kuhakikisha anakoga angalau mara mbili kwa siku.

Hakikisha kuwa nyumba ni safi kwani uchafu na vumbi huenda ikasababisha maradhi. Katika kipindi cha mimba, kinga ya mwili huwa chini. Kwa hivyo, hakikisha kuwa unakula vyakula safi, kuoga mwili na pia kunawa mikono kwa kutumia maji na sabuni.

Hakikisha pia unaishi mtindo bora wa maisha. Pata usingizi tosha, lala kwa masaa nane kila siku. Tupilia mbali vileo na sigara. Na pia utunze afya yako.

Vyanzo: WebMd

Soma Pia:Jinsi Lishe Yenye Afya Itakavyo Epusha Mtoto Kukosa Maji Tosha Mwilini

Written by

Risper Nyakio