Kuzingatia lishe katika mimba ni muhimu. Lishe ya mama inapaswa kuwa na virutubisho vyote muhimu, inapaswa kuwa na wanga, protini, ufuta, fiber, mboga, matunda na maji. Mwanamke mjamzito huwa na shaka iwapo anapaswa kula vyakula vyote alivyokuwa akichukua hapo awali kabla ya kushika mimba. Hasa vyakula vya baharini kama shrimps.
Tazama mambo muhimu mwanamke kuzingatia kuhusu lishe anayochukua katika ujauzito.
Lishe katika mimba
Fanya Haya
- Kula vyakula vyenye omega-3 fatty acids

Omega-3 ina manufaa ya kusaidia fetusi kukua kwa njia ipasavyo, kukuza akili ya mtoto kabla ya kuzaliwa, kulinda dhidi ya kujifungua mtoto kabla ya wakati. Samaki ni chanzo kizuri cha omega-3, katika mimba mwanamke anapaswa kujitenga na king mackerel, swordfish na mackerel.
2. Zingatia sahani ya upinde mvua
Kula lishe yenye virutubisho vyote inasaidia afya ya mama na ya mtoto. Matunda kama tufaha, tikiti maji, parachichi, berries na ndizi ni bora kwa mama. Mboga za kijani zina wingi wa antioxidants muhimu katika mimba.
3. Kula vyakula vilivyokuzwa bila mbolea za kemikali

Mfumo wa kinga wa fetusi huwa nyeti. Ni rahisi kwa kemikali kupitishwa kwa mtoto. Mama mjamzito anashauriwa kupunguza ulaji wa vyakula vilivyokuzwa kutumia mbolea nyingi zilizo na kemikali. Kusafisha mboga na matunda baada ya kununua ni muhimu. Kwa njia sawa, mwanamke anapaswa kupunguza kufanya kazi zinazohusisha kemikali.
4. Usile chakula cha watu wawili
Imani kuwa mwanamke anapaswa kula chakula kingi anapokuwa na mimba sio ya kweli. Mwanamke anapaswa kula chakula kinachomtosha na chenye afya. Hata kama mwanamke hupata matamanio ya kula vyakula tofauti na hawezi jidhibiti. Anapaswa kuongeza uzito kwa njia yenye afya katika mimba. Kufanya mazoezi mepesi kutasaidia kudhibiti ongezeko la uzito.
5. Kunywa maji tosha

Maji katika mimba yanasaidia kulinda dhidi ya uchungu wa uzazi usiokomaa, kuepusha maumivu ya kichwa ama kuhisi kizungu zungu.
Mbali na haya, mama mjamzito anapaswa kupunguza ulaji wa wanga uliochakatwa. Vitu kama keki na mkate havipaswi kuliwa kila siku. Vinachangia katika ongezeko la kasi la uzito katika mimba. Safisha matunda na mboga vizuri kabla ya kupika ama kukula. Kisha wasiliana na daktari wako mara kwa mara kuhakikisha kuwa mimba yako inakua kwa njia ipasayo.
Soma Pia: Dalili 5 Za Mapema Za Ujauzito Mwanamke Anazopaswa Kufahamu