Jinsi Ya Kuboresha Lishe Na Siha Kwa Mama Mjamzito

Jinsi Ya Kuboresha Lishe Na Siha Kwa Mama Mjamzito

Kupigwa masi kutasaidia kutuliza mwili wako, maumivu yoyote na pia misuli yako. Haijalishi trimesta uliyoko.

Lishe na siha ni muhimu kwa kila binadamu. Na sio wakati unapo kuwa na mimba tu, mbali wakati wote. Mama mwenye mimba ana stahili kuhakikisha kuwa anapata angalau kalori 340-450 kila siku. Ni muhimu kula vyakula tofauti vyenye afya na vilivyo na virutubisho tosha kwake. Hakikisha kuwa chakula chako kina:

  • Wanga
  • Protini
  • Matunda na mboga
  • Nafaka
  • Ufuta wenye afya

Lishe na siha

faida za scent leaf unapokuwa na mimba

Ikiwa umekuwa ukizingatia kula lishe bora yenye afya, utahitajika kufanya mabadiliko machache kwenye chakula unacho kila kila siku. Wakati huu wa mimba, ni muhimu kuhakikisha kuwa chakula chako kina maji tosha na fiber.

Vitamini na madini

Mama mwenye mimba anapaswa kuhakikisha kuwa anakula kiwango zaidi cha vitamini na madini ikilinganishwa na mama asiye na mimba. Unaweza tumia tembe za kuongeza kiwango unacho kichukua, ila, ni vyema kupata virutubisho hivi kutoka kwa chakula.

Punde tu unapo gundua kuwa unatarajia, wasiliana na daktari wako akushauri vyakula na tembe bora kuhakikisha kuwa una kimu mahitaji yako ya madini na vitamini.

Mazoezi katika ujauzito

mazoezi ya mama mjamzito

Mazoezi ni muhimu sana kwa kila mtu. Mwili unahitaji mazoezi mara kwa mara ili kuboresha utendaji kazi wake. Ni muhimu kwa mama mjamzito kufanya mazoezi ili kuhimiza mzunguko wa damu mwilini, kupumzisha mwili na misuli na kupunguza uchovu. Jaribu kunyoosha mwili kila uwezapo. Fanya mazoezi mepesi kama vile kutembea kwa angalau dakika 20-30 kila siku ama kuogelea.

Kupigwa masi katika ujauzito

Hii ni mojawapo ya mbinu maarufu ya kuutuliza mwili. Na hasa ni muhimu kwa mama anapokuwa katika safari yake ya mimba. Utashuhudia kuwa na mawazo mengi na kubabaika kuhusu vitu tofauti ukiwa na mimba.

Kupigwa masi kutasaidia kutuliza mwili wako, maumivu yoyote na pia misuli yako. Haijalishi trimesta uliyoko, kwani masi ni salama katika kipindi chochote kila na hauko katika hatari ya kupoteza mimba.

Kuutunza mwili wako ni njia bora zaidi ya kuhakikisha kuwa unamtunza mwanao na afya yake.

Ikiwa una magonjwa yanayo kusumbua ni vyema kuwasiliana na daktari wako ili utibiwe kabla ama unapokuwa katika trimesta ya kwanza ya mimba. Kwani kuna baadhi ya hali za kiafya ambazo huenda zika ongeza hatari ya kupoteza mimba.

Chanzo: webmd

Soma Pia: Mwongozo Wa Mimba Wiki Baada Ya Nyingine

Written by

Risper Nyakio